Papa Francisko kwa Kamati ya Kongamano la Seville:kuhakikisha heshima,mapendo na matunzo ya ndugu
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko, Jumamosi tarehe 8 Februari 2025, alikutana na Kamati Tendaji ya Kongamano la II la Kimataifa la Udugu na Ibada maarufu za Watu Mungu huko Seville nchini Hispania kuanzia tarehe 4-8 Desemba 2024. Katika hotuba yake alifurahi kuwapokea ndugu wapendwa Maaskofu, Mheshimiwa, Mkuu wa Mkoa wa Andalusia, mamlaka mashuhuri, Mabibi na mabwana, kama wanahija katika Mwaka wa Jubilei.
Kushuhudia upendo wa kufurika na kuonekana kichaa cha upendo
Papa alisema kuwa wamefika Roma kumshukuru Mungu kwa Kongamano la mwisho la Kimataifa la Udugu na Ibada maarufu za Watu Mungu. Walipomwambia kwamba wanakuja, Papa alisema "nilikuwa na wasiwasi kidogo, kwa sababu katika ujumbe uliotumwa na mimi wakati huo, niliwaita "vichaa" na labda ndiyo sababu mlikuwa na hamu ya kukutana nami." Akaongeza kusema: Lakini Askofu Saiz Meneses aliniambia kuwa mpango huo ulikuwa neema ambayo mwangwi wake bado unaweza kusikika na kwa hivyo nina amani zaidi.” Katika ujumbe wake kama wanakumbuka, alipendekeza kwamba waliishi tukio hilo kama sala ya sifa ambayo itaambatana na safari yao ya hapa duniani kama hija kuelekea kwa Mungu na kwa ndugu zetu. Kwa hivyo aliwaomba washuhudie pendo ambalo limefurika sana kiasi kwamba linaonekana kuwa "kichaa," cha mapendo.
Kusikia mapigo ya moyo wa upendo katika shughuli za hisani
Papa amekazia kusema kuwa ingesaidia kwa kiasi gani, katika hitimisho la tukio hilo, ikiwa kwanza ya kuwa mwangwi huo kusikika zaidi ya yote ndani ya familia. Ili kwamba isikike kama ukimya wa kiziwi cha sala inayofikiwa machozi, kwa sababu inatoka moyoni; iwe mbele ya picha ya kichwa cha udugu wao , anayezisimamia nyumba zao, iwe mbele ya hema la parokia yao au hekalu lao, iwe karibu na kitanda cha wagonjwa au katika kundi la wazee. Askofu mkuu wao alimwambia Papa kwamba mwangwi mwingine kati ya hizo, ambao tayari umegunduliwa ni kimbilio la wasio na makazi, ambalo kwa hakika ni onesho la upendo kwa Mungu, matunda ya upendo huo uliofichika ambao Papa alirejea katika ujumbe wake. Aliongeza kusisitiza kuwa “Daima tusikie mapigo ya moyo wa upendo katika kazi hiyo.”
Kuhakikisha njia ya heshima na mapendo katika nyumba za kukaribisha
Papa aliomba wahakikishe kwamba, kwa njia ya “heshima, mapendo na matunzo” katika nyumba hiyo, jamii na wale wanaokaribishwa wanaweza kutambua tena hadhi ya kipekee ambayo kila mtu anayo (taz. Dilexit nos, n. 169). Hatimaye amesisitiza kuwa Yesu awabariki na Maria, Mama wa Kanisa, awalinde. Na wasisahau kumuombea. Naye pia atawaombea.