Papa Francisko,Gemelli:Hali yake inaboreka lakini Dominika hataongoza Sala ya Malaika wa Bwana
Vipimo vilivyofanywa tarehe 15 Februari 2025 vya Papa vinaonesha "kuboresha kwa baadhi ya hali,kwa kuthibitisha hata hivyo maambukizi ya njia ya upumuaji ambayo, tangu Ijumaa 14 Februari,yalisababisha kulazwa kwake katika hospitali ya Agostino Gemelli,Roma."Ndivyo inathibitisha taarifa za jioni.
Vatican News
Kwa sababu hiyo, Baba Mtakatifu Francisko hataongoza Sala ya Malaika wa Bwana, Dominika tarehe 16 Februari 2025, kwa kufuatia agizo la “pumziko kamili” lililoombwa na timu ya madaktari wa matibabu ili “kumwezesha kupona.”
Hata hivyo taarifa kutoka Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican imeeleza marekebisho kidogo ya tiba inayoendelea. Kwa mujibu wa taarifa tunasoma kuwa: “Papa alipokea Ekaristi, na wakati wa kupumzika kwa sala na kujisomea. Papa Francisko, vile vile "anakusudia kutuma maandishi katika Sala ya Malaika wa Bwana," kwa mujibu wa taarifa za Ofisi ya Vyombo vya Habari na ambayo kwa kumalizia inasisitiza shukrani za Papa kwa "ujumbe mwingi wa ukaribu na upendo uliopokelewa" na anatualika "tuendelee kumuombea".
15 Februari 2025, 19:17