ĐÓMAP”Œșœ

2025.02.25Mkutano wa CEPROME nchini  peru, Amerika ya Kusini. 2025.02.25Mkutano wa CEPROME nchini peru, Amerika ya Kusini. 

Papa Francisko anatoa wito wa uwajibikaji na sio kutokujali katika matumizi ya AI

Papa alituma ujumbe mzito kwa washiriki wa Kongamano la IV la Amerika ya Kusini la CEPROME kuhusu kuzuia unyanyasaji Kanisani,akionya kwamba Akili Mnemba hurahisisha utayarishaji wa maudhui hatari na kufanya kuwa vigumu kuwalinda waathirika wanaoweza kuwepo.

Na Felipe Herrera-Espaliat huko Lima, Perù.

Baba Mtakatifu Francisko alitoa wito kwa wale wote wanaotumia Akili Mnemba (AI) kuwajibika, akieleza kwa mara nyingine tena nia yake ya kuimarisha ulinzi wa watoto dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia, na hivyo kutokomeza saratani hii katika jamii. Baba Mtakatifu alisema hayo kwa ukali wa kipekee kuhusu vitisho vinavyoletwa na baadhi ya sekta za maendeleo ya teknolojia na amefanya hivyo kwa kutuma ujumbe kwa watu zaidi ya mia tano wanaoshiriki katika Kongamano la IV la Amerika Kusini la Kituo cha Ulinzi wa Watoto(CEPROME) huko Lima, nchini Peru, kuanzia tarehe 25 hadi 27 Februari 2025. Chombo hiki kilianzishisha mafunzo ya mamia ya maafisa wanaohamasisha mazingira mazuri katika Kanisa na kuimarisha utamaduni wa kuzuia uhalifu huo.

Hisia ya kutokujali

Papa alianza kwa kusema kwamba mtandao wa Intaneti, kwa kufanya kila kitu kionekane kutoka katika dirisha, hujenga hisia ya kutokujali, kwa kuwa hurahisisha watu kukwepa wajibu wa ushiriki wao katika ulimwengu sambamba katika  mtandao. Walakini, kwa Papa Francisko, na Akili Mnemba(AI), hali hii ya kutokujali huongezeka sio tu kupitia kutazama, hukusanyaji au usambazaji wa nyenzo zisizofaa, lakini pia kupitia uundaji wa yaliyomo mapya, japokuwa yasiyofaa,  na yanayojumuisha nyenzo ambazo  tayari zilizopo kwenye mtandao. "Kwa mkono  wetu haumo katika kutengeneza nyenzo hizo, udanganyifu unaweza kuundwa kwamba ‘sisi sio tunafanya jambo la aibu’: kushambulia mtu, kuiba picha, kutumia wazo au wazo la mwingine, kufichua kitu cha karibu ambacho kinapaswa kubaki katika nyanja ya kibinafsi ya mtu tu. Lakini hiyo sio kweli, mashine inatekeleza maagizo yetu, inaunda, haifanyi maamuzi, lakini imepangwa kufanya hivyo", Baba Mtakatifu  alishutumu

Madhara ya matumizi mabaya ya Akili Mnemba(AI)

Ujumbe wa  Papa Francisko, uliosomwa na Balozi wa Vatican nchini Peru, Askofu Mkuu Paolo Rocco Gualtieri, uliorodhesha uharibifu unaoweza kutokea kutokana na matumizi mabaya na ya kutowajibika ya Akili Mnemba kama vile: “Uharibifu kwa wale ambao, wakiona kile tulichozalisha, wanataka kuiga; uharibifu kutokana na mtiririko mkubwa wa vifaa visivyofaa vinavyochafua mazingira; uharibifu unaotokana na ugumu unaopatikana na mamlaka katika kutofautisha kati ya nyenzo halisi na na zile za bandia ili kuhakikisha usalama wa waathirika wowote na mengine. Kwa mujibu wa Papa, walio na jukumu la kufanya teknolojia hizi kuwa salama zaidi ni wale wanaozitumia na walioziunda.

Kutoa sauti kwa Mungu na kwa waathirika

Akikabiliana na changamoto zinazoletwa na akili mnamba katika mapambano dhidi ya unyanyasaji ndani ya Kanisa, Baba Mtakatifu alisema, kuna kazi mbili za msingi: ya kwanza ni kutoa “sauti kwa Mungu na kwa wahanga wanaomwomba, ili kuwe na ufahamu wa maovu yanayofanywa” na, wakati huohuo, “kufichua uwongo uliofichika nyuma ya teknolojia ili kuweka dhamiri yetu iwe huru.” Kwa sababu hyo , Papa Francisko  alihimiza "kkuomba watu binafsi, kwa wabunifu wa teknolojia hizi na kwa mamlaka husika kuweka mipaka na sheria zilizo wazi na zinazoweza kupimika zinazoruhusu matumizi yao mabaya au ya jinai kushtakiwa.”

Shukrani kwa Baba Mtakatifu

Mkurugenzi wa Kituo cha Ulinzi wa Watoto (CEPROM), María Inés Franck alithamini sana ujumbe wa Papa Francisko, hasa kwa vile ulifika wakati afya yake ni dhaifu sana. “Baba Mtakatifu ameendelea kuhimiza na kuthibitisha juhudi zetu za kujenga utamaduni wa kuzuia katika Kanisa. Tafakari zake huongeza uelewa wetu wa ukweli huu mpya na kuakisi njia ya sisi kuendelea kupambana dhidi ya unyanyasaji na kuunda nafasi za kikanisa ambazo zinakuza ulinzi wa wote, hasa watoto na vijana Amerika ya Kusini yo,  wakili huyo wa Argentina alitoa maoni yake kwa shukrani.

Kongamano la IV CEPROME linaongozwa na mada:  â€œAkili Mnema na Unyanyasaji wa Kijinsia: Changamoto Mpya kwa ajili ya Kinga” na liliandaliwa pamoja na Tume ya Kipapa ya Ulinzi wa Watoto Wadogo ya Vatican. Tukio hilo la siku tatu litajumuisha wataalam wa kimataifa ambao wamefanya kazi na waathiriwa wa unyanyasaji katika mchakato wao wa uponyaji na kutafuta haki.

25 Februari 2025, 17:35