Papa Francisko usiku amelala vizuri katika Hospitali ya Gemelli
Vatican News
"Kama ilivyo kuwa kwa siku hizi, usiku ulipita kwa utulivu na Papa sasa anapumzika." Ndivyo taarifa inasomeka ya Ofisi ya Vyombo Vya habari, Vatican Ijumaa asubuhi tarehe 28 Februari 2025 wakati Papa Francisko anaendelea kupata matibabu ya Mkamba ya pande mbili katika Hospitali ya Agostino Gemelli, Roma.
Katika sasisho nyingine ni kwamba Papa Francisko asubuhi baada ya kuamka alifungua kinywa na kusoma magazeti kama kawaida. Aliendelea na matibabu, ikiwemo mazoezi ya kupumua.
Taarifa 27 Februari
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari Alhamisi jioni, 27 Februari 2025 hali ya kliniki ya Afya ya Papa iliendelea kuimarika. Ofisi ya Vyombo vya Habari iliongeza kuwa utabiri wowote ule bado umehifadhiwa: "Hali ya kiafya ya Baba Mtakatifu imethibitishwa kuimarika tena leo. Alibadilisha matibabu ya oksijeni ya mtiririko wa juu kwa Ventimask. Kutokana na ugumu wa picha ya kliniki, siku zaidi za utulivu zinahitajika ili kufafanua wazi utabiri huo. Asubuhi, Baba Mtakatifu alifanyiwa mazoezi ya kupumua, akibadilishana na kupumzika. Alasiri, baada ya mazoezi ya ziada, alitumia muda wake katika maombi kwenye kikanisa cha nyumba yake ya kibinafsi kwenye ghorofa ya 10, ambapo alipokea Ekaristi. Kisha akajishughulisha na shughuli za kazi ndogo ndogo.”