ĐÓMAPµĽş˝

2025.02.08 Jubilei  Vikosi vya Wanajeshi, Polisi na Usalama, (Hiki ni kikundi kutoka Poland.) 2025.02.08 Jubilei Vikosi vya Wanajeshi, Polisi na Usalama, (Hiki ni kikundi kutoka Poland.)  (ks. Marek Weresa )

Jubilei ya Majeshi,Maneno ya Mapapa kwa wapenda amani

Katika tukio la Pili kati ya matukio makuu ya Mwaka Mtakatifu 2025,tunarejea baadhi ya hotuba za Mapapa zilizoelekezwa kwa wanajeshi.Yohane Paulo II wakati wa Jubilei Kuu ya 2000,alisema “Wanajeshi,wanafaa kwa jukumu la askari,ambaye anatazama mbali ili kuepusha hatari.”

Vatican News

“Pontefice”katika  neno ambalo  maana  yake kwa  Kilatini hapo awali lilionesha mjenzi wa madaraja, ana washirika wa thamani wa kulinda na kukuza udugu. Hawa ni wajenzi wa amani, wakiwemo wanaume na wanawake wanaofanya kazi pamoja na watu wanaoishi katika mazingira magumu katika maeneo yanayotikiswa na mivutano na migogoro. "Amani duniani ni hamu kubwa ya wanadamu wa nyakati zote," aliandika Papa Yohane XXIII katika Waraka wake wa  â€“  Amani Duniani, inaweza kuanzishwa na kuunganishwa  kwa heshima kamili ya utaratibu uliowekwa na Mungu tu.” “Amani ya kweli – tunasoma zaidi katika hati hiyo – inaweza kujengwa  kwa kuaminiana tu.” Wapenda amani ndiyo watetezi wa amani hii na ndiyo chachu inayoweza kuifanya familia ya kibinadamu ikue katika udugu.

Mapapa na Vikundi vya Majeshi

Jeshi linaundwa na askari, wawakilishi wa mataifa mbalimbali lakini, zaidi ya yote, wanaume na wanawake wenye kiu ya Mungu na amani, zawadi ambayo hupata mzizi wake wa kweli katika Yesu pekee. Katika miaka ya Jubilei, maelfu ya wawakilishi wa vikosi vya kijeshi hushiriki katika sherehe na hija. Jubilei ya Wanajeshi, Polisi na Vikosi vya Usalama, iliyopangwa kufanyika tarehe 8 na 9 Februari 2025, iko ndani ya mfumo huo. Katika matukio haya tafakari ya Mapapa daima inaakisiwa na neno kuu: AMANI.

Wito wa udugu

Mnamo mwaka Mtakatifu wa 1950 ulikuwa ni Jubile ya kwanza baada ya maafa ya Vita vya Pili vya Dunia. Katika Ujumbe wa Radio katika fursa ya Noeli(, tarehe 23 Desemba  1949, Papa Pio XII, alitumaini kwamba Jubilei, baada ya nyakati kutikiswa na mapigano makali kati ya majeshi yaliyokuwa yapingana, itakuwa "mwaka mkuu wa toba,, mwaka wa msamaha mkuu.”

“Tunangojea katika Mwaka huu Mtakatifu kurejea kwa jumuiya ya kimataifa kwa mipango ya Mungu, ambayo kwa mujibu wake kwa watu wote, kwa  ajili ya amani na si kwa  ajili ya vita, kwa ushirikiano na si kwa kutengwa, kwa haki na si kwa ubinafsi wa kitaifa, wamepangwa kuunda familia kuu ya kibinadamu, kuelekea ukamilifu wa pamoja, katika kusaidiana na katika mgawanyo sawa wa mali, ambayo ni hazina ya Mungu iliyokabidhiwa kwa wanadamu. Wanangu wapendwa, ikiwa tukio fulani lilionekana kuwa zuri kwetu la kuwahimiza watawala wa watu wawe na mawazo ya amani. Huu ni Mwaka Mtakatifu unaonekana kufaa zaidi. Na  pia unataka kumaanisha ukumbusho wenye nguvu na wakati huo huo mchango kwa udugu wa watu.”

Uwajibu wa kulinda amani

Katika Mwaka Mtakatifu wa 1975, Papa Paulo VI aliongoza Ibada ya Misa Kuu Dominika tarehe 23  Novemba(,) katika Uwanja wa Mtakatifu Petro iliyohudhuriwa na zaidi ya wanajeshi 16,000. Waliunda uwakilishi mkubwa wa wanajeshi kutoka nchi ishirini. “Nyinyi ni askari; na bila shaka taswira inayowaonesha hivyo - Papa Montini alisisitiza - imeainishwa katika suala la nguvu, juhudi, nidhamu, uhodari, ujasiri na thamani.  Lakini askari si kwa sababu hii 'kujitosheleza', yaani, kujitosheleza kwa ujasiri wake wa ujana; anaweza kusali? kuomba msamaha kwa Mungu?" Kwa nini mlikuja Roma? - Papa Montini pia aliuliza. Kwa kujibu alieleza “Mmekuja, kwa sababu ninyi pia ni watu; na mwanadamu anamhitaji Mungu, Kristo, dini, wokovu; na anahisi uharaka wa kutosheleza kiu yake ya kuwasiliana na Mwana wa Mungu."

Mmekuja kwa sababu, zaidi ya mtu mwingine yeyote, mnahitaji amani; na mnataka na lazima mfanye kazi kwa amani. Na hapa kumbukumbu ya vita vya hivi karibuni - migogoro miwili ya dunia na mapigano ya mara kwa mara ya ndani -inakuwa chungu na kuungua kwa majeruhi waliosababisha, maisha ya vijana kupunguzwa, na kwa damu nyingi zisizo na hatia zilizomwagika! Kumbukumbu yetu iwe ya uaminifu na ya heshima kwa wengi waliokufa, na amani katika huruma ya Kristo Mwokozi iwe juu ya roho zao zisizoweza kufa! Kisha: kwa ajili yenu silaha hazitaki kuwa za kosa, lakini  na daima na kila mahali kwa ajili ya  ulinzi tu; na usalama, Mungu akipenda, ambao hauhitaji matumizi ya silaha, bali kuelekea kutoa nguvu kwa ajili ya haki na amani tu ( Rej. Rum. 13, 4; Luka 3, 14; 14, 31 ): yaani, katika kuzuia, kwa makubaliano ya uaminifu, kwa utunzi mkubwa, katika msamaha wa ukarimu..  Hapa basi, hatimaye, uwepo wenu unakuwa msamaha mkubwa:mmekuja kusherehekea haki, ambayo inahakikisha ustaarabu, utaratibu, heshima ndani ya watu binafsi na kati ya mataifa. Kwa haki hii, ambayo amani ni matunda yake, basi silaha zenu  ziwe ishara na ulinzi: na kwa mwanga huu kazi yenu  katika jumuiya ya kiraia ichukue maana yake kamili.

Juhudi za kila siku za amani

Mnamo 2000, maelfu ya wanajeshi walisherehekea Jubilei Kuu na Papa Yohane Paulo II ambaye alionesha amani kama "haki ya kimsingi ya kila mtu." Papa Wojtyla, mtoto wa mwanajeshi wa Poland, alikumbuka "kazi ya utulivu katika nchi zilizoharibiwa na vita vya kipuuzi" na misaada iliyotolewa "kwa watu waliokumbwa na majanga ya asili." Baba Mtakatifu katika mahubiri ( )aliyotamka tarehe 19 katika Mwaka huo Mtakatifu alisisitiza juu ya jitihada za kila siku kwa ajili ya amani:

Ni nani bora kuliko ninyi, wanajeshi na polisi wapendwa, wavulana na wasichana, wanaweza kushuhudia vurugu na kusambaratika kwa nguvu za uovu zilizopo ulimwenguni? Mnapigana nao kila siku: kiukweli mmeitwa kutetea wanyonge, kulinda waamini, kuhamasisha kuishi kwa amani kwa watu.  Kila mmoja wenu anafaa kwa nafasi ya ulinzi, ambaye anatazama mbele sana ili kuepusha hatari na kuendeleza haki na amani kila mahali. Ninawasalimu ninyi nyote kwa upendo mkuu, Ndugu wapendwa, ambao mmefika Roma kutoka sehemu nyingi za dunia kusherehekea Jubilei yenu maalum. Nyinyi ni wawakilishi wa majeshi ambayo yamekabiliana katika historia. Leo mnakutana kwenye Kaburi la Mtume Petro ili kumwadhimisha Kristo “amani yetu, aliyetufanya sisi sote wawili kuwa mmoja, na kuubomoa ukuta wa uadui uliogawanyika” (Ef 2:14). Kwake yeye katika  fumbo  na kiukweli katika Ekaristi, mmekuja kutoa nia yenu na ahadi yenu  ya kila siku kama wajenzi wa amani.

Madaraja na wapanzi

Kunako 2016 Papa Francisko akitoa salamu zake wakati wa Katekesi ya Jubilei,(,)kwa wawakilishi wa majeshi na polisi, waliokuja kutoka sehemu nyingi za dunia, kuhiji Roma katika hafla ya Jubilei  Maalum ya Huruma. Mada msingi ya tukio hilo ilikuwa: “Mlango Wake uko wazi daima,” ambapo alikumbusha kuwa huruma  ina nafasi kubwa ndani ya ukweli wa kijeshi. Baba Mtakatifu alisisitiza jukumu la msingi la jeshi katika kuhakikisha usalama wa watu na taasisi katika maeneo yote duniani.

“Dhamira ya utekelezaji wa sheria  kwa  jeshi na polisi, ni kuhakikisha mazingira salama, ili kila raia aweze kuishi kwa amani na utulivu. Katika familia zenu, katika maeneo mbalimbali mnayofanyia kazi, muwe vyombo vya upatanisho, wajenzi wa madaraja na wapandaji wa amani. Kiukweli mmeitwa sio  kuzuia, kusimamia, au kukomesha migogoro tu, bali pia kuchangia katika ujenzi wa amri iliyojengwa juu ya ukweli, haki, upendo na uhuru, kulingana na ufafanuzi wa amani wa Mtakatifu Yohane XXIII katika Waraka wake wa Kitume wa amani duniani(. Uthibitisho wa amani sio kazi rahisi, hasa kwa sababu ya vita, ambayo hukausha mioyo na kuongeza vurugu na chuki. Nawasihi msivunjike moyo. Endeleeni na safari yenu ya imani na fungua mioyo yenu kwa Mungu Baba wa huruma ambaye hachoki kutusamehe.  Katika kukabiliana na changamoto za kila siku, hebu tumaini la Kikristo liangaze, ambalo ni uhakika wa ushindi wa upendo dhidi ya chuki na wa amani dhidi ya vita.”

Jubilei ya Ulimwengu wa kijeshi 8 na 9 Februari 2025

Nguvu ya Amani

Tukio la kwanza kati ya Matukio makuu 36 ya Mwaka huu Mtakatifu lilikuwa ni Jubilei ya Ulimwengu wa Mawasiliano(Giubileo della comunicazione) lilitofanyika tarehe 24-26 Januari 2025. Hatua ya pili ya Mwaka wa Jubilei ni ile ya vikosi vya kijeshi, polisi na vya usalama tarehe 8 -9 Februari 2025.  Kwa njia hiyo maneno ya Mapapa kwa wawakilishi wa ulimwengu wa kijeshi daima ni mwaliko kwa  upande wa mwanadamu, wa haki, wa amani, ambapo ni  himizo linalosikika kwa nguvu pia katika Jubilei hii ya matumaini. Miongoni mwa wajenzi wa amani, zaidi  ya 76,000 ni wanaume na wanawake wa Umoja wa Mataifa na wanatoka zaidi ya nchi 120. Hawa wako katika Opesheni za amani (peacekeeping) katika maneno yaliyogubikwa na migogoro barani Afrika ,Asia, Ulaya na Mashariki ya Kati. Wanalinda raia, kutetea haki za binadamu na kuimarisha taasisi katika baadhi ya maeneo hatari na tete duniani. Tangu operesheni ya kwanza mnamo 1948, zaidi ya askari 4,300 wa walinda amani hawa wamekufa walipokuwa wakitekeleza misheni katika kambi ngumu za kimataifa. Hatuwezi kusahau mataifa yaliyosambaratishwa na migogoro ambayo ingali na umwagaji damu ulimwenguni leo hii. Na hatuwezi kusahau walinda amani ambao hulinda wingi wa wakimbizi wanaokimbia vita na mustakabali wa watu.

08 Februari 2025, 13:53