MAP

2025.02.24 Kuabudu katika Kikanisa cha Gemelli. 2025.02.24 Kuabudu katika Kikanisa cha Gemelli.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Hospitalini Gemelli,sala kwa ajili ya Papa,Beccalli:kumweka katikati mtu na udhaifu wake

Kuabudu,Misa ya 7:00mchana na rozari ya alasiri kwa muda wote wa kukaa hospitalini kwa Papa:hii ni ahadi ya Hospitali ambapo Monsinyo Giuliodori alisisitiza kwamba:"imani ni tumbo la kukabiliana na kila tiba halisi.”Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Moyo Mtakatifu kwa vyombo vya habari vya Vatican:“imani hapa inaingiliana na shughuli za kiafya na kisayansi.Kukumbatia kwetu kwa Baba Mtakatifu ni kama ilivyo kwa wagonjwa wote.”

Na Antonella Palermo – Vatican.

Ombi lile la "niombee, ni kauli isiyoepukika katika kila mkutano na hotuba za Papa Francisko, na ambalo linakuwa mwili wa kusali, uthabiti, ulazima na shauku  ya pamoja.  Hiyo ilifanyika  pia tarehe 24 Februari 2025, katika Kikanisa cha Mtakatifu Yohane Paolo II katika ukumbi wa hospitali ya Gemelli, ambapo Papa amelazwa hospitalini kwa sababu ya  ugonjwa wa Mkamba(Bronchitis) ya pande mbili tangu tarehe 14 Februari 2025. Ilikuwa ni saa sita mchana, kuanza na ibada ya kuabudi iliyoongozwa na Padre na saa moja baadaye, iliadhimishwa Misa pamoja na Monsinyo Claudio Giuliodori, Msaidizi mkuu wa kikanisa cha Chuo Kikuu  Katoliki cha Moyo Mtakatifu na wa Chama cha Matendo ya Kikatoliki Italia.

Kuabudu huko Gemelli
Kuabudu huko Gemelli

“Tunataka kukaribisha mwaliko wa Baraza la Maaskofu wa Italia ili kuimarisha maombi: katika muda wote wa kukaa hospitalini, nyakati hizi zitarudiwa hapa kwa nia maalum kwa ajili ya Papa. Mchana pia, saa 10:30 mkusanyiko wa maombi utafanyika katika Uwanja mbele ya lango kuu, la Hospitali kwa ajili ya kusari Rozari,”alisema.

Giuliodori:Imani ni msingi kwa kila tiba halisi

Ombi kwa ajili ya Papa ili aweze kurudi kufanya kazi katika huduma ya Injili, na ili Bwana ampe afya na nguvu ya kutangaza furaha na huruma ya habari njema katika ulimwengu. ilisikika kwa uchangamfu wa dhati katika ukaribu wa Kanisa ambapo wanafamilia na wafanyakazi wa matibabu na wasaidizi kwa kawaida,  hukusanyika kwa muda wa kutafakari, kuashiria shughuli ya kazi au kuomba sala ya uponyaji. Jumatatu tarehe 24 Februari, kwa namna ya pekee mawazo  yalielekezwa kwa Papa  Francisko. Na itakuwa vivyo hivyo katika siku zijazo: kesho, 25 Februari, Ibada ya Ekaristi Takatifu itahudhuriwa na Padre Massimo Fusarelli, Mkuu wa Shirika la Ndugu Wadogo Wafransiskani(OFM,) ambaye pia yuko anamalizia kulazwa katika Hospitali  hiyo hiyo ya Gemelli, wakati huo huo  siku ya Jumatano 26 Februari, mshereheshaji atakuwa Makamu wa Papa wa Jimbo la Roma, Kardinali Baldo Reina.

Kuabudu na Misa
Kuabudu na Misa

"Imani daima hutusaidia kupunguza hekima ya sayansi, hivyo kazi ya Mungu inatimizwa", alisema Monsinyo Giuliodori katika mahubiri yake, ambaye alisisitiza njia muhimu ya maombi kwa wale wote wanaokabiliana na mtihani wa ugonjwa. "Bwana awape nguvu Baba Mtakatifu na madaktari uwezo wote unaohitajika kwa sababu  imani inakuwa kiini cha kukabiliana na kila tiba ya kweli.” Na kisha alikuwa na matumaini kwamba Papa anaweza kurudi hivi karibuni na kikamilifu katika huduma yake."

Beccalli:mtu anakuwa katikati na udhaifu wake wote

Makoti meupe ya madaktari na sare za wauguzi vilipamba mzunguko wa Kikanisa. Babammoja akiwa ameketi  katika kiti cha magurudumu, wanafunzi vijana  wa Chuo kikuu, waamini walei rahisi. Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Chuo Kikuu cha  A. Gemelli( IRCCS) inashiriki, iliyokutana pia Februari 24 katika  kikao cha kawaida na rais, Dk. Daniele Franco, na Mkuu wa Chuo Kikuu hicho , Profesa Elena Beccalli.  Alielezea  hayo kwa vyombo vya habari vya Vatican  maana ya kuwa huko: "Hiyo ya kuwa familia, familia ya Chuo kikuu ambayo pamoja na Hospitali inataka kukumbatia Baba Mtakatifu kwa sala." Na alikumbuka ziara ya Papa wakati wa maadhimisho ya miaka sitini ya Kitivo cha Tiba (kunako tarehe 5 Novemba 2021) alipozungumza kuhusu wito wa kutunza.

Kuabudi na misa
Kuabudi na misa

"Katika siku hizi, wito huu unajidhihirisha kwa uangalifu unaokumbatia utu wa Baba Mtakatifu, unapowakumbatia wagonjwa wote ambao wamelazwa katika hospitali ya Gemelli” alisisitiza a Mkuu wa Idara. Na kwa hivyo wazo ni lile la imani kuingiliana na shughuli za kiafya, na shughuli za kisayansi, hasa za kumweka mtu katikati ya kazi yetu kwa ukamilifu wake wote, pamoja na udhaifu wake wote, lakini pia na uwezo mkubwa wa madaktari wetu kufanya mema kwa wengine.".

Wanafunzi na familia:tunakosa wito wake wa amani

Nyimbo zimeimbwa kama katika parokia. Waliouhisha ni wafanyakazi na wanafunzi wa Chuo kikuu cha cha Gemelli. Wengine wanaishi katika shule ya bweni iliyo karibu: "Tulitoa kile tunachopata cha kupendeza zaidi, kucheza na kumwimbia. Kwa urahisi." Mtawa mmoja aliyewasindikiza alisema: "Sasa ni wakati wa kuwa karibu naye namna hii."  Vijana hawa wanaoishi mbali na nyumbani kwao daima wamekuwa wakishangazwa na dhamira ambayo Fransisko anatoa wito wake wa amani na ulinzi wa mazingira, kwa ajili ya mazingira, na wanaeleza, kueleweka kwa maana yake pana,  ya kitu ambacho kinakumbatia kila kitu na kila mtu.” Kwetu sisi, imani ni muhimu, tulichagua kusomea hapa kwa sababu inatusaidia katika elimu yet."Walisema wanafunzi hao. Kikanisa siyo kikubwa, wengi walifuatilia maadhimisho katika ukumbi, wakiwa wamesimama.  Familia moja ikitoa nje ilisema "Tunamkumbuka Papa, tunatumaini atapata nafuu hivi karibuni. Tunakosa nguvu zake katika kumtia moyo kwa kila mtu."

Kuabudu na misa
Kuabudu na misa
24 Februari 2025, 16:20