MAP

2025.02.24 Sala ya waamini kwa ajili ya Papa Francisko katika Hospitali ya Gemelli, Roma. 2025.02.24 Sala ya waamini kwa ajili ya Papa Francisko katika Hospitali ya Gemelli, Roma. 

Hospitalini Gemelli:Papa alilala salama usiku mzima

Katika taarifa iliyotolewa Jumanne tarehe 25 Februari 2025 kwa waandishi wa habari mjini Vatican,kuhusu Afya ya Papa Francisko,imebainisha kuwa:“Papa alilala salama, usiku mzima.”Kwa hiyo ndilo sasisho la saa 2.25 asubuhi saa za Ulaya na saa 4.25 saa za Afrika Mashariki na Kati,kutoka Ofsi ya Vyombo vya habari,kuhusiana na afya ya Papa ambaye alilazwa katika Hospitali ya Gemelli, Roma tangu tarehe 14 Februari 2025.

Vatican News

“Papa alilala vizuri, usiku kucha.”

Hii ni taarifa iliyotlewa asubuhi tarehe 25 Februari 2025, kutoka Ofisi ya Habari ya Vyombo vya habari Vatican kuhusu hali ya afya ya Papa Francisko, ambaye amelazwa katika hospitali ya A. Gemelli tangu Februari 14. Kulingana na kile ambacho kimefafanulia, Papa aliendelea na “matibabu baada ya kuamka. Hakukuwa na matatizo zaidi ya kupumua.”

Jana, tarehe 24 Februari katika Hospitali ya Gemelli, Papa alimpokea Katibu wa Vatican, Kardinali  Pietro Parolin na akiambatana na Katibu Msaizidi wa Sekretarieti ya Vatican, Askofu Mkuu Edgar Peña Parra, kwa kutia saini baadhi ya Amri kutoka Baraza la Kipapa la Kuwatangaza Watakatifu na Wenyeheri ambao majina yao yamechapishwa  leo hii tarehe 25 Februari 2025.

Taarifa ya jioni Februari 24

Katika taarifa ya matibabu ya jana jioni, Februari 24, ilinesha kuboresha kidogo kwa njia hiyo  kulionyeshwa kuwa; hakukuwa na matatizo mapya ya kupumua,  na mtiririko wa oksijeni ulikuwa umepunguzwa kidogo, vipimo vilikuwa vimeboreka. Zaidi ya hayo, "upungufu mdogo wa kufanyakazi kwa figo sio sababu ya kuwa na wasiwasi" Taarifa pia ilieleza kuwa “ Papa Francisko alirejea kazini jana na jioni aliita kwa simu parokia ya Gaza.

Afya ya Papa Francisko
25 Februari 2025, 11:07