Hospitalini Gemelli:Papa alilala salama usiku mzima
Vatican News
“Papa alilala vizuri, usiku kucha.”
Hii ni taarifa iliyotlewa asubuhi tarehe 25 Februari 2025, kutoka Ofisi ya Habari ya Vyombo vya habari Vatican kuhusu hali ya afya ya Papa Francisko, ambaye amelazwa katika hospitali ya A. Gemelli tangu Februari 14. Kulingana na kile ambacho kimefafanulia, Papa aliendelea na “matibabu baada ya kuamka. Hakukuwa na matatizo zaidi ya kupumua.”
Jana, tarehe 24 Februari katika Hospitali ya Gemelli, Papa alimpokea Katibu wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin na akiambatana na Katibu Msaizidi wa Sekretarieti ya Vatican, Askofu Mkuu Edgar Peña Parra, kwa kutia saini baadhi ya Amri kutoka Baraza la Kipapa la Kuwatangaza Watakatifu na Wenyeheri ambao majina yao yamechapishwa leo hii tarehe 25 Februari 2025.
Taarifa ya jioni Februari 24
Katika taarifa ya matibabu ya jana jioni, Februari 24, ilinesha kuboresha kidogo kwa njia hiyo kulionyeshwa kuwa; hakukuwa na matatizo mapya ya kupumua, na mtiririko wa oksijeni ulikuwa umepunguzwa kidogo, vipimo vilikuwa vimeboreka. Zaidi ya hayo, "upungufu mdogo wa kufanyakazi kwa figo sio sababu ya kuwa na wasiwasi" Taarifa pia ilieleza kuwa “ Papa Francisko alirejea kazini jana na jioni aliita kwa simu parokia ya Gaza.