Rais anayemaliza muda wake Marekani aliwasiliana na Papa Francisko kwa upya kwa simu!
Na Salvatore Cernuzio na Angella Rwezaula – Vatican.
Rais anayemaliza muda wake nchini Marekani Bwana Joe Biden alimtunukia Papa Francisko Nishani ya Urais wa Uhuru wa Dini, ambayo ni heshima ya juu zaidi ya kiraia katika taifa hilo. Kiongozi wa Kidemokrasia mwenyewe aliwasiliana moja kwa moja na Papa Francisko kwa njia ya simu tarehe 11 Januari 2025. Kama inavyojulikana, viongozi hao wawili walipaswa kukutana ana kwa ana, siku ya Ijumaa tarehe 10, Januari 2025 kama ilivyokuwa imepangwa mjini Vatican kwa mkutano wa faragha, ikiwa ni sehemu ya safari ya Biden nchini Italia, safari yake ya mwisho ya kimataifa kabla ya mwisho wa mamlaka yake. Walakini, dharura ya moto huko Los Angeles ilisababisha safari hiyo kusitishwa.
Mazungumzo mapya ya simu
Kwa njia hiyo tangazo hilo kwa njia ya simu ya Jumamosi 11 Januari linafuatia lile la tarehe 20 Disemba iliyopita ambapo miongoni mwa masuala mbalimbali yaliyoshughulikiwa, ni pamoja na haki za binadamu ambazo zilikuwa kiini cha wasiwasi wa Papa kwa wafungwa wanaohukumiwa kifo katika magereza ya shirikisho. Mkutano huo ulifuatiwa na uamuzi wa Biden wa kubadilisha hukumu ya kifo kwa wafungwa 37, wanaume na wanawake, hadi kifungo cha maisha jela. Tayari katika hafla ya mawasiliano hayo ya kwanza, barua kutoka Ikulu iliripoti kwamba Biden "alimshukuru Papa kwa kujitolea kwake kuendelea kupunguza mateso ya ulimwengu, pamoja na kazi yake ya kukuza haki za binadamu na kulinda uhuru wa kidini." Kimsingi, sababu zilezile ambazo sasa zimemfanya kiongozi huyo wa Marekani kumchagua Papa kuwa mpokeaji wa Nishani hiyo, ambayo tayari imetunukiwa takriban Juma moja iliyopita kwa watu 19 kutoka ulimwengu wa siasa na sanaa ambao “wametoa mchango kwa kuwa mfano katika ustawi, kwa maadili au usalama wa Marekani, kwa amani ya ulimwengu, au kwa shughuli nyingine muhimu za kijamii, za umma au za kibinafsi." Baadhi ya waangalizi walikuwa wamebainisha kuwa idadi ya waliopokea haikuwa 20 ya kawaida; Biden ni dhahiri alikuwa akiokoa mshangao wa ziara yake huko Roma.
Motisha
Msukumo huo, ulioripotiwa katika taarifa kutoka Washington, unasema: “Akiwa kijana, Jorge Bergoglio alifanya kazi ya sayansi kabla ya imani kumpeleka kwenye maisha pamoja na Wajesuit. Kwa miongo kadhaa, ametumikia wasio na sauti na walio hatarini nchini kote Argentina. Kama Papa, utume wake wa huduma kwa maskini haujawahi kukoma. Mchungaji mwenye upendo, anajibu kwa furaha maswali ya watoto kuhusu Mungu Mwalimu mwenye kutia moyo, anatuamuru kupambania amani na kulinda sayari. Kiongozi mkaribishaji, hufikia madhehebu mbalimbali. Papa wa kwanza kutoka Ulimwengu wa Kusini, Papa hana tofauti na mtu yeyote ambaye amewahi kufika. Zaidi ya yote, yeye ni Papa wa watu: mwanga wa imani, matumaini na upendo unaong’aa kwa uangavu ulimwenguni kote.”
Chapisho la Biden
Rais Biden aliwasilisha heshima hiyo kwa balozi wa kitume nchini Marekani, Askofu Mkuu Christoph Pierre, kama inavyoonekana kwenye picha iliyowekwa kwenye akaunti yake ya X @Potus. Picha hiyo inaambatana na chapisho kutoka kwa rais linalosomeka hivi: “Papa Francisko, unyenyekevu na neema yake havielezeki na upendo wake kwa wote havilinganishwi. Akiwa Papa wa watu, yeye ni mwanga wa imani, matumaini na upendo unaong’aa duniani kote. Leo nilipata heshima ya kumtunuku Baba Mtakatifu Francisko Nishani ya Urais ya Uhuru wa Dini.”
Aliyetanguli kupata heshima hiyo ni Papa Yohane Paulo II
Hata hivyo hii si mara ya kwanza kwa Papa kupokea heshima ya urais wa Marekani kwani tayari mnamo tarehe 4 Juni 2004, Rais wa wakati huo Bwana George W. Bush alikuwa amemkabidhi Papa Yohane Paulo II nishani ya Uhuru wakati wa ziara yake mjini Vatican.