MAP

Papa alipotembelea  Cuba 2015. Papa alipotembelea Cuba 2015. 

Papa:Taasisi na jamii kwa ujumla lazima ifanye mipango na njia zinazorejesha imani ndani yao

Katika ujumbe kwa washiriki wa Mkutano wa VI wa Kimataifa unaoongozwa na mada:”Kwa Mizani Duniani,"huko Havana(Cuba),kuanzia tarehe 28 hadi 31 Januari 2025,Papa anabainisha kuwa tumaini linatuwezesha kuwa tayari kushiriki mateso,shida,kukata tamaa na hofu zinazoambatana na maisha ya kila mtu na kila jamii.Taasisi na jamii lazima zijitume kusaidia na kuhakikisha zinapinga maovu.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko ametuma  ujumbe wake kwa washiriki wa Mkutano wa VI wa Kimataifa unaoongozwa na mada ya  “Kwa Mizani Duniani," uliofunguliwa  tarehe 28 Januari mjini Havana nchini Cuba na hutamalizika  tarehe 31 Januari 2025. Papa Francisko katika ujumbe wake kwa lugha ya kihispanyola aanaandika kuwa: “Ni lazima tufanye kazi kwa kudhamiria ili kwamba tumaini, ambalo tunapewa kwa imani na upendo wa Yesu Kristo na kwa hiyo msingi wa upendo, lintafsiriwe kuwa amani kwa ulimwengu na ni muhimu kuacha mantiki ya vurugu na kushiriki katika mazungumzo na diplomasia, kujenga ujasiri na kwa ubunifu nafasi za mazungumzo yanayolenga amani ya kudumu.

Hofu ya siku sijazo

Katika ujumbe huo Papa anaonya kwamba hakuna juhudi zozote zitakazofanikiwa ikiwa haitafanikiwa katika kuhakikisha kwamba kila mtu, anazuiliwa kufungua maisha yake kwa shauku, kutokana na kasi ya maisha, hofu ya siku zijazo; ukosefu wa usalama wa kazi na ulinzi wa kutosha wa kijamii, wa mifano ya kijamii ambao ajenda yao inatawaliwa na kutafuta faida badala ya utunzaji wa mahusiano, ili waweze  kutazama siku zijazo kwa matumaini. Kwa upande wa Baba Mtakatifu mipango yote inayotafuta kufungua njia kwa kaka na dada wengi wanaoishi katika hali ngumu, bila kujali sababu, inapaswa kuhmasishwa.

Taasisi zishirikiane

Taasisi na jamii kwa ujumla, kwa ushirikiano wa mawakala wote wa kijamii, lazima wafanye mipango na njia zinazorejesha imani yao ndani yao na katika jamii, kwamba maskini na wagonjwa, vijana na jamii,  wazee, wahamiaji na watu waliohamishwa, ikiwa ni pamoja na wale walionyimwa uhuru wao” lazima kuwekwa katika. Hakuna anayepaswa kutengwa na kila mtu anapaswa kuona utu wake wa kibinadamu ukiheshimiwa, auliza, akipendekeza pia kwamba wajitoleaji na wataalamu wanaohusika katika nyanja hizi daima wawe na njia za kutosha za kuendeleza kutia moyo kwa manufaa ya wanadamu wote.

Tumaini lisilokatisha tamaa

Katika ujumbe huo, Baba Mtakatifu alikumbuka, Hati ya  , ya kutangaza kwa  Jubilei kwamba katika hati hiyo  iliyojikita juu ya  mwaka wa  Jubilei  ni mwaka wa neema na fursa ya kurejesha amani na maelewano kutumaini, kama wito kwa watu wote wenye mapenzi mema udugu wa kijamii, kwa njia ya msamaha na upatanisho. Na kwa sababu hiyo, katika Hati  mfululizo wa ishara na kuhimiza tumaini vilipendekezwa kupitishwa katika kiwango cha kijamii na kiutamaduni, kugundua tena adili hili la thamani leo hii kwa kutoa umakini kwa wema mkuu uliopo duniani ili tusiangukie katika jaribu la kujiona kuwa tumezidiwa na uovu na vurugu. Kwa hakika Papa anabainisha kuwa  matumaini yanathibitisha kuwa thamani inayofaa sana kwa  ajili ya Mkutano unaondelea  katika mji mkuu wa Cuba, ambao unalenga kuwa wazi, na kwa wingi wa  taaluma mbalimbali, ili kuchunguza sababu zinazochochea moyo wa mwanadamukutumaini.  

Kuishi kidugu kama familia moja ya Mungu

Kwa njia hiyo tunatumaini, kama tunavyosoma katika Waraka wa Kitume wa , linaturuhusu kuwa tayari kushiriki mateso, shida, kukatishwa tamaa na hofu ambayo huambatana na maisha ya kila mtu na ya kila jamii. Ni lazima tutambue ndani ya kila mwanamume na kila mwanamke sura ya Mungu,  ya kuwa kaka na dada na kuwa sehemu ya familia ya binadamu na familia ya watoto wa Mungu. Na hii hata nje ya ulimwengu wa imani,  kwa sababu wote wameitwa kuishi katika ukarimu wa kidugu na kila kitu tunachofanya kwa wengine kinatuhusu sisi kama watu binafsi na kama jamii. Papa Fransisko alihimiza. Kwa kuongezea anasisitiza kuwa: “Na tujifunze somo hili kutokana na upendo, kwa kujenga tumaini katika usawaziko huo unaotaka kumhakikishia kila mtu kile anachohitaji.” Kwa sababu hiyo ni lazima tujifunze kushiriki na maskini na kujifungua kwa ukarimu wa kuwakaribisha wengine, ili kujua jinsi ya kuchangia kile tulicho na kuwa nacho kwa manufaa ya wote.”

Ujumbe wa Papa kwa Cuba
29 Januari 2025, 10:56