Papa na Wajumbe wa Mtandao wa Maombi Ulimwenguni:Moyo wa Kristo:huruma,ukaribu na upole!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko Alhamisi tarehe 23 Januari 2025, alikutana na Wajumbe wa Mfuko wa Mtandao wa Maombi ya Papa Ulimwenguni kote. Akianza hotuba yake alimsalimia Mkurugenzi mpya, Padre Cristóbal Fones, ambaye alimtakia kazi njema; na wakati huo huo alitoa shukrani zake kwa Padre Fornos aliyemaliza muda wake na kwamba alikuwa mzuri…! Mahiri sana kwa huduma yake aliyoifanya na kwamba alikuwa "mbunifu." Alitoa salamu kwa wanachama wa Ofisi ya Kimataifa, Waratibu wa Bara, Wajumbe wa Bodi, Washirika wa Kudumu na, hasa, wale wanaounga mkono Mfuko ili kuhakikisha utulivu na kasi ya shughuli zake. Ametoa asante kwao. Papa alifurahi kwamba walikaribisha kwa furaha Waraka wake wa Dilexit nos, juu ya upendo wa kibinadamu na wa Kimungu wa Moyo wa Kristo. Ndani yake watapata lishe kubwa inayomwilisha hali ya kiroho ya kazi yao, ya utume wao.
Papa amependa kwamba wanaita hali hii ya kiroho kuwa ni "njia ya Moyo." Na alipenda kutambua usemi huu kwa maana mbili: ni safari ya Yesu, ya Moyo wake mtakatifu, kwa njia ya fumbo la umwilisho, mateso, kifo na ufufuko; na pia ni njia ya moyo wetu, iliyojeruhiwa na dhambi, ambayo inaruhusu yenyewe kushindwa na kubadilishwa kwa upendo. Katika safari hii ya moyo, Mama yetu, Maria, anatuongoza, kama siku zote, ambaye hututangulia katika hija ya imani na matumaini na anatufundisha kuweka katika mioyo yetu maneno na ishara za Yesu neno hili la kulinda.
Papa amesema kwamba hii ni kazi ya Roho Mtakatifu: hakuna safari ya moyo na Kristo bila maji ya uzima ya Roho Mtakatifu. Papa aliongeza kusema kuwa ni matumaini yake kuwa “Mtandao wa Maombi ya Ulimwenguni Pote utatoa mchango muhimu sana kwa Jubilei, kusaidia watu na jumuiya kuishi roho yake, kama safari ambayo sala na huruma, sala na ukaribu kwa angalau, vinaunganishwa bila kutenganishwa, maombi na matendo ya huruma. Asante, asante sana! Amewatakiwa wasonge mbele kwa furaha, daima kwa furaha, wakishirikiana na wengine. Aliwabariki kutoka moyoni mwake na kuhitimisha.