ĐÓMAPµĽş˝

2025.01.27 Papa na Maaskofu, Marais wa Tume za Mawasiliano na Wakurugenzi wa Kitaifa wa Ofisi za Mawasiliano duniani. 2025.01.27 Papa na Maaskofu, Marais wa Tume za Mawasiliano na Wakurugenzi wa Kitaifa wa Ofisi za Mawasiliano duniani.  (Vatican Media)

Papa akutana na wahusika wa Mawasiliano ya mabaraza ya Maaskofu:kuwasiliana ni upendo Kanisa lazima litoke nje!

Papa akikutana na maaskofu,Marais wa Tume za Mawasiliano za Maaskofu na Wakurugenzi wa Ofisi za Mawasiliano za Mabaraza ya Maaskofu Junuari 27,alisisitiza maneno mawili:“kwa pamoja”na“mtandao.”Matumaini hayakatishi tamaa;Je tunajua jinsi ya kuwasilisha hili?Je!tunajua jinsi ya kuwasilisha kwamba maisha ya wengine yanaweza kuwa mazuri zaidi,hata kupitia sisi?Kila Mkristo anaitwa kuona na kusimulia historia za mema ambayo uandishi wa habari potofu hujaribu kufuta na kutoa nafasi ya uovu tu.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko Jumatatu tarehe 27 Januari 2025, alikutana katika Ukumbi wa Clementina mjini Vatican na Maaskofu, Marais wa Tume za Mawasiliano za Mabaraza ya Maaskofu na wakurugenzi wa Ofisi za Mawasiliano za Mabaraza ya Maaskofu. Katika hotuba yake aliwakaribisha wote ambao katika Makanisa mahalia wanafanya huduma ya kuwajibika katika nyanja ya mawasiliano. Inapendeza kuwaona hapo, maaskofu, mapadre, watawa wa kike na kiume na walei, walioitwa kuwasilisha maisha ya Kanisa na mtazamo wa Kikristo wa ulimwengu. Kuwasiliana na maono haya ya Kikristo ni kuzuri, alisema Papa Francisko. Papa aidha aliongeza kuwa “Tunakutana leo, baada ya kuadhimisha Jubilei ya Ulimwengu wa Mawasiliano, kufanya mapitio na pia uchunguzi wa dhamiri pamoja. Hebu tutulie ili kutafakari zaidi juu ya njia halisi tunayowasiliana nayo, inayohuishwa na imani ambayo, kama ilivyoandikwa katika Waraka kwa Waebrania (rej 11:1), ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo na bayana ya mambo yasiyoonekana. Na kwa hiyo “hebu tujiulize basi: je, tunapandaje matumaini katikati ya hali ya kukata tamaa sana ambayo inatuathiri na kutupa changamoto? Je, tunatibu vipi virusi vya mgawanyiko, ambavyo pia vinatishia jumuiya  zetu? Je, mawasiliano yetu yanaambatana na sala? Au tunaishia kuwasiliana na Kanisa kwa kupitisha sheria za uuzaji wa kampuni tu? Tunapaswa kujiuliza maswali haya yote.” Papa alisema.

Papa akutana na maaskfou marais wa tume za mawasiliani na wakurugenzi ofisi za mawasiliano
Papa akutana na maaskfou marais wa tume za mawasiliani na wakurugenzi ofisi za mawasiliano   (Vatican Media)

Papa aliendelea:  â€śJe, tunaweza kushuhudia kwamba historia ya mwanadamu haijaishia katika mwisho mbaya? Na je, tunaelekezaje mtazamo tofauti kuelekea wakati ujao ambao haujaandikwa tayari?  â€śNinapenda usemi huu kuandika siku zijazo”, alisema papa . Ni juu yetu kuandika siku zijazo. Je, tunaweza kuwasiliana kwamba tumaini hili si udanganyifu? Matumaini kamwe hayakatishi tamaa; lakini tunajua jinsi ya kuwasilisha hili? Je! tunajua jinsi ya kuwasilisha kwamba maisha ya wengine yanaweza kuwa mazuri zaidi, hata kupitia sisi? Je, ninaweza, kwa upande wangu, kuleta uzuri katika maisha ya wengine? Na tunajua jinsi ya kuwasiliana na kushawishi kwamba inawezekana kusamehe? Hii ni ngumu sana!” Papa amekiri. Mawasiliano ya Kikristo yanaonesha kwamba Ufalme wa Mungu umekaribia: hapa, sasa, na ni kama muujiza unaoweza kushuhudiwa na kila mtu, na kwa wote. Muujiza ambao lazima usemwe kwa kutoa funguo za kutazama zaidi ya mzaa, zaidi ya uovu, zaidi ya ubaguzi, zaidi ya mazoea, zaidi ya sisi wenyewe. Ufalme wa Mungu ni zaidi yetu. Ufalme wa Mungu pia unakuja kupitia kutokamilika kwetu, na hii ni nzuri. Ufalme wa Mungu unakuja katika uangalifu tunaotoa kwa wengine, katika utunzaji wa uangalifu tunaoweka katika kusoma ukweli.UInakuja katika uwezo wa kuona na kupanda tumaini la mema. Na hivyo kuushinda ushabiki wa kukata tamaa.

Mkutano wa Papa
Mkutano wa Papa   (Vatican Media)

Papa Francisko kadhali alifafanua kuwa hii  ambayo kwao ni huduma ya kitaasisi, pia ni wito wa kila Mkristo, wa kila mtu aliyebatizwa. Kila Mkristo anaitwa kuona na kusimulia historia za mema ambayo uandishi wa habari mbaya hujaribu kufuta, na kutoa nafasi ya uovu tu. Uovu upo, haupaswi kufichwa, lakini lazima ukoroge, uzae maswali na majibu. Kwa sababu hiyo  kazi yao ni kubwa na inawahitaji wajitoe mwenyewe, kufanya kazi ya pamoja  ili ya kuwashirikisha kila mtu, kuwathamini wazee na vijana, wanawake na wanaume; kwa kila lugha, kwa maneno, sanaa, muziki, uchoraji, na picha. Sisi sote tumeitwa ili kuthibitisha jinsi gani na nini tunawasiliana naye. Tunahitaji kuwasiliana. Papa amesisitiza kuwa hiyo pia changamoto ni kubwa. Kwa hiyo alihimiza kuimarisha harambee kati yao, katika ngazi ya bara na ya ulimwengu mzima. Kujenga mtindo tofauti wa mawasiliano, tofauti katika roho, katika ubunifu, katika nguvu ya kishairi inayotoka katika Injili na isiyokwisha. Kuwasiliana daima ni asili. Tunapowasiliana, sisi ni waundaji wa lugha, wa madaraja. Sisi ndio waumbaji. Mawasiliano ambayo hupitisha maelewano na ni mbadala thabiti wa minara mipya ya Babeli. Papa ameomba kufikiria kuhusu hili kwa muda. Minara mipya ya Babeli kwamba: kila mtu anaongea na haelewani na  mwenzake. Kufikiria juu ya ishara hii.

Kwa hiyo Papa Francisko aliwaachia mambo mawili wahusika hawa wa mawasiliano ya mabaraza ya Maaskofu ya “Pamoja “na “Mtandao.” Akianza kudadavua, Papa alisema Neno ni “kwa Pamoja tunaweza kuwasilisha uzuri ambao tumekutana nao: si kwa sababu sisi ni wenye ujuzi, si kwa sababu tuna rasilimali nyingi, lakini kwa sababu tunapendana. Kutokana na hilo  nguvu ya kuwapenda hata adui zetu inakuja, kuwashirikisha hata wale ambao wamefanya makosa, kuunganisha yaliyogawanyika na kutokata tamaa. Na vile vile kupanda tumaini.” Kwa kuongezea Papa aliomba wasisahau hilo la “kupanda tumaini na siyo kunyume chake  hata kidogo bali kupanda matumaini.” Kama sisi, kuwasiliana sio mbinu. Sio juu ya kurudia maneno mafupi au kauli mbiu, wala sio kuandika tu taarifa kwa vyombo vya habari. Kuwasiliana ni tendo la upendo. Ni  tendo la bure tu  la mapendo ya  kufuma mitandao ya wema. Lakini mitandao inahitaji kutunzwa, kutengenezwa, kila siku. Kwa subira na imani.”

Mkutano wa Papa
Mkutano wa Papa   (Vatican Media)

Neno la Pili ambalo Papa amependa kuwaachia ni Nyavu ambapo amewaalika kulitafakari. Kwa sababu, kiukweli, tumepoteza kumbukumbu yake, kana kwamba ni neno linalohusishwa na ustaarabu wa kidigitali. Na badala yake ni neno la kale. “Linatukumbusha, mbele ya zile za kijamii, nyavu za wavuvi na juu ya mwaliko wa Yesu kwa Petro awe mvuvi wa watu. Nyavu kwa hivyo: inamaanisha ustadi wa mitandao, maarifa, michango, kuweza kufahamisha vya kutosha na hivyo kuokolewa kutoka katika bahari ya kukata tamaa na upotovu. Huu tayari ni ujumbe, na tayari ni ushuhuda wa kwanza wenyewe. Kwa njia hiyo ameomba wafikirie, basi, ni kiasi gani wanaweza kufanya pamoja, kutokana na zana mpya za enzi ya kidijitali, shukrani pia kwa akili mnemba, ikiwa badala ya kugeuza teknolojia kuwa sanamu, tujitolee zaidi kuwa nyavu.” 

Papa amekiri jambo moja kwao kuwa “Ninajali zaidi akili ya asili kuliko akili mnemba, akili ambayo lazima tuikuze. Tunapohisi kuwa tumeanguka kwenye shimo, tuache tutazame  zaidi ndani yetu sisi wenyewe. Hakuna kinachopotea; daima tunaweza kuanza tena, kwa kuaminiana sisi kwa sisi na sote kwa Mungu, na ndiyo siri ya nguvu zetu za mawasiliano.” Kwa hiyo mtandao au nyavu na kuwa mtandao! Badala ya kutegemea ving'ora tasa vya kujitangaza, kwenye sherehe za mipango yetu, hebu tufikirie jinsi ya kujenga pamoja historia za matumaini yetu. Papa Francisko alisisitiza kuwa  mtandao wetu ni wa kila mtu. Kwa wote! Mawasiliano ya Kikatoliki si kitu tofauti, si kwa Wakatoliki tu. Sio uzio wa kujifungia, katka madhehebu ya kusemezana, hapana! Mawasiliano ya Kikatoliki ni nafasi wazi ya ushuhuda unaojua jinsi ya kusikiliza na kupitisha ishara za Ufalme. Ni mahali pa kukaribisha kwa mahusiano ya kweli. Hebu tujiulize: ofisi zetu na mahusiano kati yetu yapo hivyo? Mtandao wetu ni sauti ya Kanisa ambalo kwa kutoka tu lenyewe nje  linaweza kujikuta lenyewe na sababu za tumaini lake. Kanisa lazima litoke nje lenyewe.

Papa na wawasilianaji
Papa na wawasilianaji   (Vatican Media)

Papa alisema navyopenda kufikiria kifungu hicho kutoka kwa Kitabu cha Ufunuo, wakati Bwana alisema: "Nasimama mlangoni na kubisha" (Uf 3:20). Alisema hivyo ili aingie. Lakini sasa, kwa mara nyingi tena Bwana anabisha kutoka ndani ili sisi, kama Wakristo tuweze kumruhusu atoke nje! Na mara nyingi tunamchukulia Bwana kwa ajili yetu wenyewe. Kinyume chake ni lazima tumruhusu Bwana atoke ne  na kubisha mlango ili tusimwache kuwa  "mtumwa" kidogo kwa ajili ya huduma zetu. Je, ofisi zetu, mahusiano yetu, mtandao wetu ni wa Kanisa linalotoka nje? Papa ameuliza. Alihitimisha  akiwashukuru  kwa kazi yao. Aliwatakia waendelee mbele kwa ujasiri, kwa furaha na kuinjilisha. Amewabariki wote kwa moyo na tafahadli aliwaomba wasisahau kumuombea.

Papa na wahusika wa Mawasiliano ya Mabaraza ya Maaskofu
27 Januari 2025, 10:49