MAP

2025.01.17 Papa na Jumuiya ya Waseminari wa Cordoba nchini Hispania. 2025.01.17 Papa na Jumuiya ya Waseminari wa Cordoba nchini Hispania.  (Vatican Media)

Papa Francisko kwa Waseminari wa Córdoba:Nafasi za kwanza ni njia kipofu,tumfuate Yesu

Mwelekeo,hatari katika safari na maeneo ya vitulizo ni alama tatu alizofafanua Papa kwa Waseminari wa Córdoba.Mwelekeo:si katika nafasi za kwanza ambazo ni njia za kipofu,ikiwa hatuma bahati ya kuondokana nazo,tutalazimika kurudi nyuma kwa ugumu na kwa aibu;Hatari safarini:inawezekana kuvumilia katika safari ya Bwana,kwa kuamini kuwa Yesu atakuwa msaada;Maeneo ya vitulizo:tunahitaji kusindikizwa na kuhisi uwepo wa Yesu tumaini letu.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Ijumaa tarehe 17 Januari 2025 amekutana mjini Vatican na Jumuiya ya Waseminari wa Córdoba nchini Hipania. Katika hotuba yake alionesha furaha yake kuwakaribisha katika nyumba hiyo ambapo wamefika kama mahujaji wa matumaini katika Mwaka wa Jubilei. Papa amesema kuwa katika safari ya maisha, tumaini tunaweza kulifananisha  kama alama ambazo zinatulekeza mwendo.

Papa akiwa na waseminari wa Cordoba
Papa akiwa na waseminari wa Cordoba   (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Mwelekeo

Baba Mtakatifu kwa kufafanua hilo alisema alama ya kwanza ni mwelekeo: kuelekea mbingu na  kukutana hatimaye na Yesu. Si katika nafasi za kwanza, si katika maeneo ya starehe zaidi, kwa sababu zile ni njia  kipofu, ambazo , ikiwa hatuma bahati ya kuondokana nazo, tutalazimika kuondokana nazo kwa kurudi nyuma kwa ugumu na kwa aibu.

Hatari katika safari

Alama ya pili ni hatari katika safari. Papa Francisko ameeleza kuwa wao wanatoka katika eneo zuri sana ambapo linachukua jina la Mtakatifu Pelagius, na linatawaliwa na eneo la kizamani la uwanja wa mashahidi(hapa Papa alikuwa akimaanisha Mtakatifu Pelagius wa Cordoba ambaye alizaliwa  huko Crecente, karibia mwaka 912 – Cordoba, na kifo chake tarehe 26 Juni 926. Alikuwa shahidi wa Kihispania, mwathirika kwa mkono wa utawala wa kihislamu wa Abd al-Raḥmān III, aliyekuwa amiri wa Cordoba, na  ambaye tangu karne ya 10 amekuwa akiheshimiwa kama mtakatifu hasa na Wahispania. Kuna hati tatu za wasifu wa  Pelagius ambazo ni za nusu ya kwanza ya karne ya 10 na zimeandikwa miongo michache baada ya matukio yaliyosimuliwa).

Kwa njia hiyo Papa Francisko ameeleza kuwa “Kama alivyofanya wakati huo Mtakatifu huyo mtoto, katikati ya maumivu ya vita, ya ukatili zaidi usio stahili wa kuwa mwanadamu, akiwa amevalia kofia ya tumaini, inawezakana kutoa ushuhuda, inawezekana kuvumilia katika safari ya Bwana, kwa kuamini kuwa Yesu atawasimamia daima na atawapatia zaidi ya hayo, nguvu ya kuwa wapandaji wa matumaini.

Papa na waseminari wa Cordoba
Papa na waseminari wa Cordoba   (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Maeneo ya vitulizo

Alama ya tatu ni maeneo ya vitulizo. Papa alisisitiza kuwa katika safari ambayo sasa imewaleta jijini Roma, kwa kupitia Mlango Mtakatifu na kutembelea makaburi ya Mitume, “tunahitaji kusindikizwa, kuhisi uwepo wa Yule ambaye ni tumaini pekee, yaani Yesu. Yeye anajiwakilisha kwetu kama Mwalimu, kama Bwana, anatoa chakula kwetu katika Neno lake na katika Ekaristi,  anazungumza nasi tunapojikita ndani ya safari  na kutupokea wakati tunashindwa katika ugumu,  lazima kusimama ili kupumzika. Bila tumaini hilo, ingekuwa ukichaa kuanza safari, lakini, tukimtumaini Yeye, hatuna shaka kwamba tutafika kwenye bandari inayotakiwa."

Papa na waseminari wa Cordoba
Papa na waseminari wa Cordoba   (Vatican Media)

Baba Mtakatifu ameendelea kukazia kuwa, tusifikiri kamwe kuwa kupanda matumaini, iwe ni kusema maneno ya fadhili au uchague tabia njema ya kufanya wema la. Safari hii, ni safari ya Yesu, ambaye anatupeleka katika Yerusalemu ya mbingu, kwa kupitia ile ya duniani, tukikumbatiwa na msalaba na kuungwa mkono na maelfu ya Wakirene. Kwa kuhitimisha, Papa Francisko amebainisha Njia ambayo hatuwezi kusonga mbele peke yetu, lakini katika jamuiya, tukiongoza, tukitetea, tukiwasaidia na kuwabariki wale ambao Bwana ametuachia kama kazi. Yesu awasimamie katika haya yote na Bikira wa Fuensanta awalinde.

Papa amekutana na waseminari wa Cordoba
17 Januari 2025, 11:57