MAP

2025.01.3 Abate  Prosper Guéranger, mtumishi wa Mungu na abati wa kwanza wa Abasia ya Mtakatifu-Pierre huko Solesmes. 2025.01.3 Abate Prosper Guéranger, mtumishi wa Mungu na abati wa kwanza wa Abasia ya Mtakatifu-Pierre huko Solesmes. 

Papa Francisko:Abate Guéranger,kinara wa upyaisho wa imani na mwalimu wa sala

Papa ametuma barua katika Abasia ya Mtakatifu Pierre wa Solesmes katika kumbukizi ya miaka 150 ya kifo cha mwanzilishi na Abate wa kwanza,akikumbuka jukumu lake msingi katika ugunduzi upya wa liturujia kama lugha ya Kanisa na katika urejesho wa Kanisa.Shirika la Wabenediktini nchini Ufaransa:Ushuhuda hai wa maisha ya kimonaki.

Na Angella Rwezaula – Vatican.


Baba Mtakatifu Francisko ametuma ujumbe kwa Shirika la Wabenediktini wa Ufaransa huko Solesmes, wakati wanaadhimisha kumbukumbu ya miaka 150 ya kifo cha mwanzilishi wao, Abati Prosper-Louis-Pascal Guéranger (1805-1875), ambaye alirejesha utawa wa Wabenediktini nchini Ufaransa katika karne ya 19 na kuanzisha uamsho wa kiliturujia ya kisasa. Mpinzani mkubwa wa Harakati la Wagallikani, lililotafuta uhuru zaidi kwa Kanisa la Ufaransa kutoka kwa Upapa, Abate Guéranger anachukuliwa kuwa mtangulizi wa kile kilichojulikana kama Harakati la kiliturujia ya kisasa katika karne ya 20.

Katika ujumbe wake kwa Mkuu wa Shirika wa Solesmes, Abate Geoffroy Kemlin OSB, Papa Francisko anatoa maneno ya sifa kwa watawa wa Kibenediktini wanaoendelea kufuata nyayo za Abate Guéranger na kazi ya kuhifadhi na kueneza maarifa ya urithi wake, akiakisizi kwa kina hali ya kiroho ambayo iliashiria maisha yake hadi mwisho. Baba Mtakatifu Francisko pamoja na watangulizi wake, anakumbuka mchango wake, hasa katika maeneo matano muhimu: urejesho wa maisha ya utawa wa Wabenediktini nchini Ufaransa, kazi yake ya kitaaluma katika Liturujia, kujitolea kwake kwa Moyo Mtakatifu wa Yesu na Bikira Maria, msaada wake katika kufafanua mafundisho ya imani ya Bikira Maria Mkingiwa dhambi ya Asili na Papa na hatimaye utetezi wake wa uhuru wa Kanisa.

Ujumbe unalenga hasa vipengele viwili vya karama yake ambavyo vina umuhimu hasa kwa Kanisa la leo hii: uaminifu kwa Kiti Kitakatifu mji wa Vatican, hasa katika masuala ya kiliturujia, na ubaba wa kiroho. Kwanza, kabisa Papa anatambua nafasi kubwa ya Abati Guéranger katika Harakati la Liturujia, ambalo hatimaye lilichangia katika Katiba ya Sacrosanctum Concilium ya Mtaguso wa Pili wa Vatican iliyopelekea mageuzi ya liturujia ya Kirumi, huku akmsifu jinsi ambavyo Abate Guéranger alivyotafuta kugundua upya liturujia kama lugha ya Kanisa na kielelezo cha imani yake.Ugunduzi huu mpya ulimpelekea kutetea kurejea kwa umoja wa Liturujia ya Kirumi huko Ufaransa na kuhamasisha maandishi yake ya kina, hasa Mwaka wa Liturujia, ambayo ililenga kufanya uzuri na utajiri wa liturujia kupatikana kwa wote.

Akinukuu imani ya Abate Guéranger alibainisha kwamba “sala ya Kanisa ndiyo inayopendeza zaidi sikio na moyo wa Mungu,” aidha Papa Francisko anaelezea matumaini yake kwamba mfano wa Abate Mbenediktini unaweza kuamsha upendo mpya kwa mapokeo ya kiliturujia ya Kanisa na umoja wa kina zaidi na Kanisa. “Mfano wa Abate Guéranger na utie moyo katika mioyo ya wabatizwa wote upendo kwa Kristo na Bibi-arusi Wake, pamoja na uaminifu wa kindugu na ushirikiano wa upole cum Petro et sub Petro (pamoja na Petro na chini ya Petro), ili Kanisa, waaminifu kwa Mapokeo yake hai, linaweza kuendelea kuinua 'sala moja na ile ile inayoweza kuonyesha umoja wake'."

Katika sehemu ya pili ambayo Papa Francisko anaakisi ni ubaba wa kiroho wa Abate Guéranger, hasa kujitolea kwake "kuongoza roho katika kumtafuta Mungu." Papa anabainisha kwamba imani yake ya upole na yenye shangwe katika maongozi ya kimungu haikuathiri tu watawa na watawa chini ya uongozi wake bali pia watu wa kawaida—wazazi, watoto, na waamini wa kawaida—waliotafuta ushauri wake. Iwe katika nyakati za amani au katika shida, aliimarisha imani ya wale waliokuwa karibu naye, alikuza maisha yao ya maombi, na kuongeza upendo wao kwa Kanisa. Hapa tena Baba Mtakatifu Francisko anaeleza matumaini yake kwamba, kielelezo chake cha mwongozo wa kiroho kitaendelea kuwatia moyo wengi katika safari yao ya imani. Mfano wake wa unyenyekevu kwa Roho Mtakatifu na utumishi utie moyo na kuwaongoza wengi waaminifu katika njia za Bwana, ‘wapole na wanyenyekevu wa moyo’ (Mt 11:29). Kwa kuhitimisha ujumbe wake, Papa anaomba kwamba Abate Guéranger “aendelee kuzaa matunda ya utakatifu kati ya waamini wote na kubaki kuwa shahidi hai wa matunda ya maisha ya utawa katika moyo wa Kanisa.”

Papa na wabenediktini
30 Januari 2025, 17:39