Papa anaandika katika jarida la "Il Regno:"sauti yenye mamlaka ya Mtaguso na baada ya Mtaguso
Vatican News
"Sauti ya mamlaka ya Mtaguso na baada ya Mtaguso nchini Italia." Kwa maneno haya Papa Francisko alifafanua jarida la mafunzo ya kidini na kiutamaduni la ‘Il Regno’, katika barua iliyotumwa tarehe 1 Januari 2025 wakati wa fursa ya maadhimisho ya miaka 70 ya kuanzishwa kwake. Baba Mtakatifu alitambua dhima kuu ya jarida la‘Il Regno’ katika mjadala wa kikanisa na kiutamaduni wa Italia kwamba, "limesindikiza maisha ya Kanisa, likimwilisha matakwa yake ya wanamageuzi, kadiri ya roho ya kufanya upya Mtaguso" na "linafanya kazi muhimu wa habari, nyaraka na tafsiri za wakati wetu.”
Zuppi:Mchango katika mazungumzo na mageuzi
Katika siku hizo hizo, Askofu Mkuu wa Bologna na Rais wa Baraza la Maaskofu wa Italia(CEI), Kardinali Matteo Zuppi, pia alituma ujumbe sawa kwa wafanyakazi wa wahariri na mkurugenzi wake. Kwa Kardinali, gazeti hili limetoa na linaendelea kutoa mchango msingi katika maisha ya Kanisa la Italia kwamba“Limefuatilia kwa makini changamoto kuu za upyaisho, kuanzia katekesi, uenezaji wa majiundo ya kitaasisi, mageuzi ya miundo ya kitaasisi na kufanywa upya kwa huduma.” 'Il Regno' kulingana na Kardinali Zuppi, daima limetoa "mchango fulani katika uenezaji wa mazungumzo ya kiekumene na ya kidini. Katika suala la uchambuzi na uelewa wa miundo ya kijamii na kisiasa, limekuwa na sifa ya maono ya baada ya itikadi na limeandika na kutafsiri kwa kina mabadiliko makubwa ya kitaifa na kimataifa."
Mkurugenzi Brunelli:kitendo cha ukarimu kutoka kwa Papa na Zuppi
Kwa mujibu wa mkurugenzi Gianfranco Brunelli aliandika kuwa:“ Barua ambayo Papa Francisko alitutumia mnamo tarehe 1 Januari 2025, siku ya kwanza ya kumbukumbu hiyo, pamoja na ile ya Askofu Mkuu wa Bologna na Rais wa CEI, Kardinali Matteo Zuppi, inawakilisha kitendo cha ukarimu ambacho hutuheshimu na kutufariji, kufunga shida fulani za mbali na ambayo hutufurahisha na kututia moyo, na kufungua tena upeo wa kazi yetu. Pengine ile punje ya haradali iliyotupwa kwa miaka mingi sana imekuwa mmea mzuri” msukumo huo wa Kikristo; kwa kulinganisha na watu wa tamaduni na imani tofauti, ambao hata hivyo wanayo kanuni ya uhuru na utu wa binadamu mioyoni mwao, kwa sababu hawa ni kioo cha kibinadamu cha Mungu."