Papa kwa Trump:Marekani lazima iwe nchi ya fursa na inayokaribisha wote!
Vatican News
Kwa msukumo wa maadili ya Taifa, ardhi ya fursa na ukaribisho kwa wote, ni matumaini kuwa chini ya uongozi wake watu wa Marekani watafanikiwa na daima watajitahidi kujenga jamii yenye haki zaidi, ambapo hakuna nafasi ya chuki, ubaguzi au kutengwa. Haya ndiyo matashi mema ambayo Papa Francisko ametuma katika ujumbe kwa Donald Trump, siku ya kuapishwa kwake kama rais wa arobaini na saba wa Marekani, tarehe 20 Januari 2025.
Juhudi za amani
Katika ujumbe huo, Papa Francisko anatuma salamu zake na kumhakikishia maombi yake ili aweze kumjalia rais mpya "hekima, nguvu na ulinzi katika kutekeleza majukumu yake ya juu." Tukitazama basi “changamoto nyingi” ambazo familia ya binadamu inakabili leo, kwanza kabisa janga la vita, Papa anaomba “Mungu aongoze juhudi zake katika kukuza amani na upatanisho kati ya watu”.
Sherehe hiyo
Kwa hivyo Donald Trump atarejea Ikulu ya White House kwa muhula wa pili (ya kwanza ilikuwa 2016) baada ya uchaguzi mnamo Novemba 2024. Sherehe ya makabidhiano na Joe Biden itafanyika karibujioni saa 12 za Italia), ndani ya mzunguko wa Ikulu mbele ya viongozi wa dunia na watu washuhuri wa kteknolojia. Kabla ya Trump, Makamu wa Rais JD Vance ataapishwa.