China-Vatican,Askofu wa kwanza wa Lüliang aliyewekwa wakfu chini ya makubaliano ya Vatican na China
Vatican News
Kwa nia ya kukuza uchungaji wa kundi la Bwana na kuhudhuria kwa ufanisi zaidi kwa manufaa yake ya kiroho," tarehe 28 Oktoba 2024, Papa Francisko aliamua kufuta Jimbo la Fenyang huko China Bara, ambalo liliundwa tarehe 11 Aprili 1946 na Papa Pio XII, na wakati huo huo kusimika Jimbo jipya la Lüliang,huku akiigawa kutoka Jimbo kuu la Taiyuan, jimbo la Shanxi, lenye kiti cha uaskofu katika Kanisa kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu, lililoko Fenyang, mji wa Lüliang.
Jimbo jipya
Hayo yalitangazwa katika taarifa ya Vatican kwa vyombo vya habari, ikieleza kwamba mipaka ya kikanisa ya Jimbo jipya itajumuisha maeneo yafuatayo: wilaya ya Lishi, kata za Wenshui, Jiaocheng, Xingxian, Linxian, Liulin, Shilou, Lanxian, Fangshan, Zhongyang, Jiaokouna miji katza za Xiaoyi na Fenyang. Badala yake, Kata za Kelan na Jingle zimejumuishwa katika Jimbo Kuu la Taiyuan; huku Kata za Pingyao na Jiexiu zikiunganishwa kuwa Jimbo la Yuci. Kwa njia hii, eneo la Jimbo la Lüliang linaendana na lile la Mji Mkuu wa Lüliang, lenye jumla ya eneo la km2 21,000 na jumla ya wakazi 3,346,500, ambao takriban elfu 20 ni Wakatoliki, wanaohudumiwa na Mapadre 51 na watawa 26.
Askofu wa kwanza kuwekwa wakfu
Ujumbe wa Vatican ulitangaza kwamba, Jumatatu tarehe 20 Januari 2025, pia aliwekwa wakfu wa kiaskofu Monsinyo Anthony Ji Weizhong, ambaye Papa alimteua kuwa Askofu wa Lüliang (Mkoa wa Shanxi) tarehe 28 Oktoba 2024, "baada ya kuidhinisha ugombea wake ndani ya mfumo wa Makubaliano ya Muda kati ya Vatican na Jamhuri ya Watu wa China".
JI Weizhong asili yake ni Wenshui (Shanxi), ambapo alizaliwa tarehe 3 Agosti 1973. Alisoma taalimungu katika Seminari ya Kitaifa ya Beijing na akapewa daraja la Upadre tarehe 4 Oktoba 2001 kwa Jimbo la Fenyang. Kisha akafanya masomo ya lugha katika Chuo Kikuu cha Xi'an na kupata Leseni ya Taalimungu katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (Ujerumani). Alijikita na hughuli za kichungaji huko Fenyang kama padre msaidizi wa parokia, mkuu wa Kituo cha Kichungaji cha Jimbo na mkuu.