杏MAP导航

Tafuta

2025.01.20 Kuwekwa wakfu kwa askofu wa China Anthony Ji Weizhong. 2025.01.20 Kuwekwa wakfu kwa askofu wa China Anthony Ji Weizhong.  (? Fides)

China-Vatican,Askofu wa kwanza wa Lüliang aliyewekwa wakfu chini ya makubaliano ya Vatican na China

Papa alifuta Jimbo la Fenyang na kuanzisha Jimbo jipya la Lüliang huku akimteua Padre Anthony JI Weizhong kuwa mchungaji wake wa kwanza"baada ya kuidhinisha ugombea wake ndani ya mfumo wa Makubaliano ya Muda kati ya Vatican na Jamhuri ya Watu wa China."

Vatican News

Kwa nia ya kukuza uchungaji wa kundi la Bwana na kuhudhuria kwa ufanisi zaidi kwa manufaa yake ya kiroho," tarehe 28 Oktoba 2024, Papa Francisko aliamua kufuta Jimbo la Fenyang huko China Bara, ambalo liliundwa tarehe 11 Aprili 1946 na Papa Pio XII, na wakati huo huo kusimika Jimbo jipya la Lüliang,huku  akiigawa kutoka Jimbo kuu la Taiyuan, jimbo la Shanxi, lenye kiti cha uaskofu katika Kanisa kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu, lililoko Fenyang, mji wa Lüliang.

Jimbo jipya

Hayo yalitangazwa katika taarifa ya Vatican kwa vyombo vya habari, ikieleza kwamba mipaka ya kikanisa ya Jimbo jipya itajumuisha maeneo yafuatayo: wilaya ya Lishi, kata za Wenshui, Jiaocheng, Xingxian, Linxian, Liulin, Shilou, Lanxian, Fangshan, Zhongyang, Jiaokouna miji katza za Xiaoyi na Fenyang. Badala yake, Kata za  Kelan na Jingle zimejumuishwa katika Jimbo Kuu la Taiyuan; huku Kata za  Pingyao na Jiexiu zikiunganishwa kuwa Jimbo la  Yuci. Kwa njia hii, eneo la Jimbo la Lüliang linaendana na lile la Mji Mkuu wa Lüliang, lenye jumla ya eneo la km2 21,000 na jumla ya wakazi 3,346,500, ambao takriban elfu 20 ni Wakatoliki, wanaohudumiwa na Mapadre 51 na watawa 26.

Askofu wa kwanza kuwekwa wakfu

Ujumbe wa Vatican ulitangaza kwamba, Jumatatu tarehe 20 Januari 2025, pia aliwekwa  wakfu wa kiaskofu Monsinyo Anthony Ji Weizhong, ambaye Papa alimteua kuwa Askofu wa Lüliang (Mkoa wa Shanxi) tarehe 28 Oktoba 2024, "baada ya kuidhinisha ugombea wake ndani ya mfumo wa Makubaliano ya Muda kati ya Vatican  na Jamhuri ya Watu wa China".

JI Weizhong asili yake ni Wenshui (Shanxi), ambapo alizaliwa tarehe 3 Agosti 1973. Alisoma taalimungu katika Seminari ya Kitaifa ya Beijing na akapewa daraja la Upadre tarehe 4 Oktoba 2001 kwa Jimbo la Fenyang. Kisha akafanya masomo ya lugha katika Chuo Kikuu cha Xi'an na kupata Leseni ya Taalimungu  katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (Ujerumani). Alijikita na hughuli za kichungaji huko  Fenyang kama padre msaidizi wa parokia, mkuu wa Kituo cha Kichungaji cha Jimbo na mkuu.

22 Januari 2025, 11:06