杏MAP导航

Tafuta

2023.08.02 Rais wa Baraza la Maaskofu Ureno akisalimiana na Papa kabla ya Masifu ya jioni kwenye Monasteri ya Jero'nimos 2023.08.02 Rais wa Baraza la Maaskofu Ureno akisalimiana na Papa kabla ya Masifu ya jioni kwenye Monasteri ya Jero'nimos  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

WYD,rais wa maaskofu Ureno,Carvalho:Kanisa ni makao ya waliotengwa!

Mwanzoni mwa maadhimisho ya Masifu ya jioni huko Lisbon pamoja na wawakilishi:Maaskofu,mapadre,watawa na wahudumu wa kichungaji,Rais wa Baraza la Maaskofu Ureno,Askofu José Ornelas Carvalho amemkaribisha Papa na kwamba wanahisi changamoto ya mwaliko wa kujifungua wenyewe kwa furaha ya Injili katika jamii yenye haki na udugu.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Katika mkusanyiko wa Maaskofu, mapadre, mashemasi, wanaume na wanawake waliowekwa wakfu, waseminari na wachungaji walichukua nafasi zao wakiwa wamekaa katika Monasteri ya Jerónimos ili kusali Masifu ya jioni na Baba Mtakatifu, tarehe 2 Agosti 2023. Kabla ya sala hiyo, Askofu José Ornelas Carvalho, rais wa Baraza la Maaskofu wa Ureno na askofu wa Jimbo la Leiria-Fatima alitoa salamu za kumkaribisha Baba Mtakatifu Francisko kwa niaba ya Kanisa zima la Ureno na washiriki wa maadhimisho ya Masifu ya jioni, ambayo yalihitimisha siku hii ya kwanza ya Papa Francisko katika nchi ya Ureno. Ni katika fursa ya ziara yake ya kitume ya 42 Kimataifa ili kushiriki Siku ya Vijana duniani 2023 huko Lisbon iliyofunguliwa kwa Ibada ya Misa Takatifu na kuongozwa na Patriaki wa Lisbon. Kwa hiyo Askofu Carvalho alimshukuru Papa Fransisko kwa uwepo wake katika Siku ya Vijana ulimwenguni(WYD). Huu ni mkutano wa vijana unaodhihirishwa na kukutana kwao na Kristo, ili uweze kuwaongoza kuelewa na kuota ndoto ya Mungu mwenyewe kwa kutafuta njia za ushiriki wa furaha, ukarimu na ubunifu katika Kanisa na katika ubinadamu wote, alisema.


Kwa hiyo rais wa maaskofu wa Ureno aliendelea kusema kuwa hii pia ni fursa ya kuonesha ushirika na ufuasi wa jumuiya nzima ya kikanisa mahalia kwenye mafundisho yanayofanywa na Papa. “Tunajisikia kuguswa na kuwa shaka hasa kuhusu mwaliko wako wa kujifungua wenyewe kwa  ajili ya furaha ya Injili  katika hali ya umoja wako wote, ambayo huzalisha Kanisa na jamii yenye haki na kidugu, ambapo 'wote ni kaka na dada'. Pia tunachochewa kwa ombi lako la kuhimiza 'Kanisa linalopaswa kutoka nje na ambalo linatoa uangalifu maalum kwa wale wote waliotengwa na ulimwengu, katika shida ya wakimbizi na ishara za kiinjili za uwepo na kuwa na wasiwasi na utunzaji, kuanzia na huduma ya Sayari  ambayo Mungu ametupatia kama nyumba ya pamoja  ya wanadamu", alisema Rais wa Baraza la Maaskofu Ureno.


Askofu pia alirejea katika mchakato wa safari ya sinodi ambayo ina maombi haya yote na ambayo kama Kanisa la Ureno limeifanya pia kwa kujitoa lenyewe katika njia ya mageuzi ya kichungaji, kwa ushirika wa kidugu, katika kushiriki kikamilifu na utume wa kimisionari kwa jumuiya zao. Hatimaye Askofu Carvalho alimhakikishia Baba Mtakatifu sala zake endelevu za kumwomba Bwana afya, nuru na furaha kwa ajili yake kwamba: “Sote tunaomba baraka za Mungu juu yake, ili aweze kuendelea kutubariki kwa Jina lake na kuwa baraka kwa ulimwengu wetu”.

Dakika moja ya siku ya Papa Francisko nchini Ureno kwa siku ya tarehe 2 Agosti 2023

 

02 Agosti 2023, 23:28