Papa azungumza na waandishi wa habari:itakuwa vizuri kuelewa ukimya wa Mongolia
Vatican News
Papa Francisko, Alhamisi jioni tarehe 31 Agosti 2023, baada ya kusalimiana na waandishi wa habari takriban sabini wanaoandamana naye kwenye ndege inayoelekea Mongolia, kwa kuchochewa na maoni kutoka kwa mmoja wao, alilezea moja ya sifa za watu wa Kimongolia anakokaribia kuwatembelea. Dokezo limetokana na kuwa na msongamano mdogo wa watu katika eneo kubwa la taifa.
Kwa mujibu wake amesema: “Kwenda Mongolia ni kwenda kwa watu walio wachache katika nchi kubwa. Mongolia inaonekana kutokuwa na mwisho na wenyeji ni wachache, watu sio wengi lakini wa utamaduni mkubwa. Ninadhani itatufaa kuelewa ukimya huo wa mrefu sana na wa ukuu wake. Itatusaidia kuelewa maana yake, lakini siyo kiakili, bali kuielewa kwa hisia”. Papa alikazia. Na kwa kuongezea alisema: “Mongolia inaweza kueleweka kwa hisia”. Ninajiruhusu kusema kwamba labda itakuwa vizuri kusikiliza muziki wa Borodin, ambao uliweza kuelezea mapana na marefu ya Mongolia yanamaanisha nini.”
Wakati wa mzunguko wa salamu kwa waandishi wa habari wanaokwenda na Papa, alioneshwa chupa ya maji. Ni ya askari wa Kiukraine ambaye aliokolewa kutokana na mlipuko. Alipeleka kitu hicho kanisani huko Lviv ili kumshukuru Mungu kwa kuokoka. Alikuwa ni mwandishi wa habari Eva Fernandez, kutoka Radio Cope, ambaye alisimulia historia hiyo. Iliingia katika milki ya muda ili aweze kumwonesha Papa. Kitu hicho chenye alama za vita zilizochongwa ndani yake, kwa vyovyote vile kitarudishwa kanisani kwa baraka ambayo Papa Fransisko alitoa.
Zaidi ya hayo, wakati wa salamu hizo, Papa Francesco pia alijibu swali lililoulizwa na mwandishi wa habari wa Ansa, Fausto Gasparroni, kuhusiana na ajali iliyotokea muda mfupi baada ya saa sita usiku wa kuamkia tarehe 31 Agosti 2023 huko Brandizzo, eneo la Torino, ambapo wafanyakazi watano walikufa kwa kuzidiwa na treni. Papa alisema ajali hizi daima ni ukosefu wa huduma. Wafanyakazi ni watakatifu, alisema.