Papa huko Mtakatifu Maria Mkuu kukabidhi ziara ya Hungaria
Na Angella Rwezaula,- Vatican.
Kama ilivyo kawaida yake, ni kwa mara ya 106 ambayo Baba Mtakatifu Francisko, asubuhi umatano tarehe 26 Aprili 2023 amekwenda katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria Mkuu Roma ili kusali mbele ya picha ya Bikira Maria Afya ya Waroma na kumkabidhi ziara yake ya kitume ya kwenda nchini Hungaria kuanzia tarehe 28 hadi 30 Aprili 2023. Hayo yamethibitishwa kwa waandishi wa habari na msemaji wa vyombo vya habari Vatican.
Pamoja na ulinzi wa Mama Yetu, ikumbukwe kwamba Papa aliwaomba waamini wote kumsindikiza katika safari ya karibu huko Hubagaria ma baada ya sala ya Malkia wa Mbingu Alifanya hivyo Dominika tarehe 23 Aprili iliyopita akikumbusha ulimwengu kwamba kwa siku tatu atasafiri hadi mji mkuu Budapest “kukamilisha safari aliyofanya mwaka wa 2021 kwa Kongamano la Kimataifa la Ekaristi. Safari, ya baba Mtakatifu daima alisema, ambayo inafanyika katika Ulaya"ambapo pepo za barafu za vita zinaendelea kuvuma, wakati harakati za watu wengi zinaweka masuala ya dharura ya kibinadamu kwenye ajenda. Papa pia alisisitiza kwao anaowatembela kwa upendo ndugu zake na kwa Hungaria Kaka na dada wakiwa na shughuli nyingi za kutayarisha kuwasili kwake: “Ninawashukuru sana kwa hili. Ninaomba kila mtu anisindikize kwa maombi”.