ĐÓMAPµĽş˝

Papa Francisko:Mungu hapendi kuhukumu bali anasamehe daima

Na Angella Rwezaula, - Vatican

Katika uwanja mkubwa  zaidi wa michezo “Papp László Budapest ndani mji mkuu wa nchi, Baba Mtakatifu Jumamosi jioni tarehe 29 Aprili 2023 alikutana na   na vijana. Katika Uwanja huo una uwezo wa kuingia watu12,500 na hutumiwa kwa hafla nyingi kama vile michezo, masuala ya kiutamaduni, mikutano, maonesho, kwa hiyo katika fursa hii wameandaa kwa ajili ya mkutano wa imani, na Mrithi wa Petro. Hawa ni  vijana wa kike na kiume waliowasili kutoka sehemu mbalimbali za nchi, kwa kutumia usafiri wa umma, treni na mabasi ambayo yalikuwa ya bure katika tukio hilo. Katika uwanja huo, Baba Mtakatifu alikaribishwa na Askofu mwenye dhamana ya uchungaji wa vijana, ambapo aliweza kushuhudia ngoma ya asili, alisikiliza shuhuda za vijana watatu, nyimbo na baadaye alitoa hotuba iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu sana na ambayo imepata mwangwi wa shangwe, vifijo na makofu. Kama kawaida ya utamaduni wa Hungaria wakati wa kusalimiana alisema: “Tumsifu Yesu Kristo… vijana walishagilia wakati wa kujibu milele Amina!  Amewashukuru kwa ngoma, kwa wimbo, kwa ushuhuda wao wa ujasiri na kwa  kwa kila mtu kuwepo pale. Na Furaha kuwa na wao.

Mkutano wa Vijana nchini Hungaria
Mkutano wa Vijana nchini Hungaria

Askofu Mkuu Ferenc alieleza kwamba ujana ni wakati wa kujiuliza maswali mazuri na majibu mazuri. Ni kweli, na ni muhimu kwamba kuna mtu anayekasirisha na kusikiliza maswali yao na ambaye hakupi majibu rahisi na yaliyofungwa tayari, lakini hukusaidia kushindana bila woga na adha ya maisha katika kutafuta majibu mazuri. Kiukweli, ndivyo Yesu alivyofanya. Bertalan, alisema kwamba Yesu si mhusika katika kitabu cha hadithi au shujaa mkuu katika katuni, na ni kweli: Kristo ni Mungu katika mwili na damu, Mungu aliye hai anayekaribia; yeye ni Rafiki, bora wa marafiki, ni Ndugu, bora wa ndugu, na ni mzuri sana katika kuuliza maswali. Hakika, katika Injili, yeye ambaye ni Mwalimu, anauliza maswali kabla ya kutoa majibu. Papa amefikiri wakati alijikuta mbele ya yule mwanamke mzinzi kila mtu alikuwa akimnyooshea vidole. Yesu anaingilia kati, wale wanaomshtaki waliondoka na alibaki peke yake pamoja naye. Kisha alimuuliza kwa upole: “Mwanamke, wako wapi? Hakuna aliyekuhukumu?” (Yh 8:10 ). Alijibu: "Hakuna, Bwana!” Na kwa hivyo, wakati alikuwa anasema, alielewa kuwa Mungu hataki kuhukumu, lakini kusamehe. Mungu husamehe daima, yuko tayari kutuinua tena na kila anguko letu! (Papa ameomba kurudia neno hilo:“ “Kwa hivyo tukiwa naye hatupaswi kamwe kuogopa kutembea na kusonga mbele maishani. Pia tunamfikiria Maria Magdalene, ambaye asubuhi ya Pasaka alikuwa wa kwanza kumwona Yesu aliyefufuka. Alikuwa akitokwa na machozi karibu na kaburi tupu na Yesu alimwuliza: “Mwanamke, kwa nini unalia? Unatafuta nani?” ( Yh 20:15). Na hivyo, kwa kuguswa haraka, Maria Magdalena alifungua moyo wake, na akamwambia juu ya mahangaiko yake, alifunua shauku  zake na upendo wake.

Baba Mtakatifu amekazia vijana kuwaleza kutazama tukio la kwanza la Yesu na wale ambao wangekuwa wanafunzi wake. Wawili kati yao, wakiongozwa na Yohana Mbatizaji, walimfuata. Bwana aligeuka na kuuliza swali moja: “Unatafuta nini?" ( Yh 1:38 ). Papa Francisko amependa kuwauliza swali, lakini kila mmoja alijibu katika moyo wake, na hasa mara baada ya kuuliza wafanye kimya. Swali lilikuwa: Je mnatafuta nini? Mnatafuta nini katika maisha? Ni kitu gani unatafuta katika moyo wako? Ni kujiliuza ndani ya moyo… (Ukimya ulitawala). Papa ameongeza kusema kwamba: “Yeye hubiri, bali anatembea njiani pamoja nao: hataki wanafunzi wake wawe watoto wa shule wanaorudia somo, bali vijana walio huru na wanaosonga mbele, wasindikizaji  wanaosafiri na Mungu anayesikiliza mahitaji yao na kuwatii, mwenye kuwa makini na ndoto zao. Baada ya muda mrefu, wanafunzi wawili vijana waliteleza vibaya: walimwomba Yesu ombi lisilo sahihi, yaani, waweze kusimama mmoja upande wake wa kuume na wa kushoto atakapokuwa Mfalme.

Vijana wakicheza ngoma ya utamaduni
Vijana wakicheza ngoma ya utamaduni

Papa amesema lakini hii inashangaza kuona kwamba Yesu hakuwakemea kwa kuthubutu, hakuwaambia: “Mnathubutuje, acheni kuota mambo haya!” Hapana, Yesu havunji ndoto zao, bali aliwasahihisha jinsi ya kuzitimiza; alikubali tamaa zao za kufikia kilele, lakini alisisitiza juu ya jambo moja, ambalo lazima likumbukwe vizuri: Mtu hafanyi kuwa mkuu kwa kupita juu ya wengine, lakini kwa kujishusha kwa wengine; si kwa gharama ya wengine, bali kwa kuwatumikia wengine (Mk 10:35-45). Baba Mtakatifu alimuomba mfasiri arudie maneno aliyotamka kwamba: “Yesu anachosema, anatusahihishaje? Inatukumbusha kwamba “mtu hawi mkuu kwa kuwapita wengine, bali kwa kujishusha kuelekea kwa wengine”. Hatukui kwa gharama ya wengine, bali kwa kuwatumikia wengine.” [Mfasiri alirudia maneno hayo katika lugha ya kihungaria, na kisha, Papa kauliza: Je! Mmeelewa? .... vijana walipiga makofi…

Papa amewaita marafiki kwamba, Yesu anafurahi kuwa wanafanikisha mambo makuu. Kwa hiyo hakuna haja ya kuwa wavivu, hawahitaji kuwa kimya na aibu, wanahitaji kuwa hai, na  wahusika wakuu. Na hadharau matarajio yao , lakini, kinyume chake, inainua kiwango cha matamanio ya kila mtu. Yesu angekubaliana na methali yao, ambayo alitumaini aitamke vema isemayo: Aki mer az nyer,   yaani ni nani anayethubutu hushinda. Lakini je unashindaje maishani? Kwa kujibu Papa amesema “Kuna hatua mbili za kimsingi, kama katika mchezo: kwanza, lengo la juu; pili, kufanya zoezi.  Kuhusiana na lengo la juu. Je, una kipaji? Una hakika! Basi usikiweke kando kufikiri kwamba kiwango cha chini cha wazi kinatosha kuwa na furaha: shahada, kazi ya kupata pesa, kuwa na furaha ... Hapana, weka kile ulicho nacho mstari wa mbele. Je, una ubora mzuri? Wekeza katika hilo, bila woga! Je, unahisi moyoni mwako kwamba una uwezo ambao unaweza kuwa mzuri kwa wengi? Je, unahisi kwamba ni vizuri kumpenda Bwana, kuunda familia kubwa, kusaidia wale walio na uhitaji? Usifikirie kuwa ni matamanio yasiyo tekelezeka, bali wekeza katika malengo makuu ya maisha! Na kisha fanya mzaoezi. Kwa vipi? Katika mazungumzo na Yesu, ni nani kocha bora zaidi. Anakusikiliza, anakuhamasisha, anakuamini, anajua jinsi ya kuleta kilicho bora ndani yako. “Na kila mara anatualika tuungane: tusiwe peke yetu bali na wengine, katika jumuiya, kwa pamoja, tukiishi uzoefu wa kawaida. “Ninawazia, kwa mfano, Siku za Vijana Ulimwenguni, na ninachukua fursa hii kuwaalika kwenye Siku hiyo ijayo, ambayo itakuwa Lisbon nchini Ureno, mwanzoni mwa Agosti.

Ngoma ya utamaduni kwa vijana mbele ya Papa
Ngoma ya utamaduni kwa vijana mbele ya Papa

Baba Mtakatifu akiendelea amesema leo hii hata hivyo, kuna jaribio kubwa la kufurahia simu ya mkononi na marafiki wachache. Lakini, hata kama hivyo ndivyo wengi hufanya, hata kama ndivyo wanavyohisi kufanya, wajue kuwa sio nzuri kwao. Papa ameongeza kusema “ Huwezi kujifungia katika kundi la marafiki ndogo, na kuzungumza tu na simu ya mkononi: hii ni kitu” na ameomba aruhusu kusema neno. Kisha kuna kipengele muhimu cha mafunzo na Krisztina, aliyetoa ushuhuda alikumbusha hilo kwa kusema kwamba kati ya mbio elfu, kelele nyingi na kasi, kuna jambo moja muhimu ambalo vijana, na watu wazima pia, wanakosa leo hii: Suala la nafasi kwani “ Hatujiachii muda wa kunyamaza kimya katika kelele, kwa sababu tunaogopa upweke na kisha kila siku tunaishia kuchoka”.

Papa amependa kuwaleza kwamba katika hili, wasiogope kwenda kinyume na wimbi, kutafuta muda wa kusimama kwa ukimya kila siku na kusali. “ Kusali hakuchoshi. Ni sisi tunaofanya kuwa kugumu. Kusali ni kukutana, na  Bwana hiyo ni nzuri”. Leo kila kitu kinawambia kuwa lazima uwe na haraka, uwe mzuri, mkamilifu, kama mashine! Lakini basi tunagundua kwamba mara nyingi tunaishiwa na gesi na hatujui la kufanya. Ni vizuri kujua jinsi ya kuacha kujaza, kuchaji betri. Lakini lazima kuwa mwangalifu: wasijishughulishe na huzuni yao au uchungu juu ya huzuni wao, wasifikirie juu ya nani aliwafanyia hivi au vile, wakifanya nadharia juu ya jinsi ya wengine wanavyofanya; hii sio nzuri! Papa amewaonya.

Baba Mtakatifu amesisitiza kwamba ukimya ni msingi wa kusitawisha uhusiano wenye manufaa, kwa sababu unatuwezesha kumkabidhi Yesu kile tunachoishi, kumletea nyuso na majina, kumtupia wasiwasi wetu, kuwapitia marafiki zetu na kuwaombea. Ukimya unatupatia fursa ya kusoma ukurasa wa Injili unaozungumza na maisha yetu, kumwabudu Mungu hivyo kupata amani mioyoni mwetu. Ukimya hukuruhusu kuchukua kitabu ambacho sio lazima ukisome, lakini kinachokusaidia kusoma roho ya mwanadamu, kutazama maumbile ili sio tu kuwasiliana na vitu vilivyotengenezwa na wanadamu na kugundua uzuri unaozunguka.  Sisi lakini ukimya si wa kushikamana na simu za mkononi na mitandao ya kijamii; hapana kwa hiyo Papa ameomba kwamba maisha ni ya kweli, sio ya yasiyo ya kweli, na hayafanyiki kwenye skrini, lakini ulimwenguni!

Ukimya ni mlango wa maombi na maombi ni mlango wa upendo. Papa, alimshukuru Dora kwa ushuhuda wake kwa sababu alizungumza juu ya imani kama hadithi ya upendo, ambapo kila siku anakabiliana na magumu ya ujana, lakini anajua kuwa kuna Mtu pamoja naye, wa kwake, na mtu fulani, Yesu, haogopi kushindana  na  kila kikwazo anachokutana nacho. Maombi husaidia kufanya hivyo, kwa sababu ni mazungumzo na Yesu, kama vile Misa ni kukutana naye, na Kukiri ni kumbatio ambalo mtu hupokea kutoka kwake. Mwanamuziki  mkuu  wa nchi yao Ferenc Liszt amekuja akilini mwake. Wakati wa kusafisha piano yake baadhi ya shanga za rozari zilipatikana ambazo labda, zikivunjika, zilianguka ndani ya chombo chake. Ni dalili inayotufanya tufikirie jinsi, kabla ya utunzi au uigizaji, labda hata baada ya muda wa kufurahisha kwenye piano, ilikuwa kawaida kwake kusali: alizungumza na Bwana na Maria juu ya kile alichopenda na kuweka sanaa yake na vipaji vyake katika maombi. “Mnapoomba, Msiogope kumletea Yesu kila kitu kinachopita katika ulimwengu wenu wa ndani: mapenzi, hofu, matatizo, matarajio, kumbukumbu, matumaini”.

Uwaja ulijaa umati wa vijana kutoka sehemu mbali mbali za dunia
Uwaja ulijaa umati wa vijana kutoka sehemu mbali mbali za dunia

Sala ni mazungumzo, ni maisha. Shuhuda mwingine ambaye Papa ametaja ni Bertalan, ambaye anasema hukuona aibu kumwambia kila mtu kuhusu mahangaiko ambayo nyakati fulani yamemfanya kuwa na ulemavu na mapambano ya kuikaribia imani. Ni jinsi gani ilivyo nzuri unapokuwa na ujasiri wa kuwa wa kweli, ambao hauoneshi kwamba hauogopi kamwe, lakini kufungua na kushiriki udhaifu wako na Bwana na wengine, bila kujificha, bila kuvaa barakoa. Kama Injili inavyosimulia katika kila ukurasa, Bwana hafanyi mambo makuu na watu wa ajabu, bali na watu halisi. Badala yake, wale wanaotegemea uwezo wao na kuishi kwa kuonekana wazuri, wanamweka Mungu mbali na moyo. Yesu kwa maswali yake, kwa upendo wake, kwa Roho wake, anatuchimba ndani yetu ili kutufanya tuwe watu halisi. Na leo hii kuna uhitaji mkubwa wa watu halisi! Katika jambo hilo, Papa amethibitisha walivyo vutiwa na maneno aliyosema, Tódor, kuanzia na jina lake, ambalo analichukua kwa heshima ya Mwenyeheri Theodore, muungaji mkuu wa imani ambaye anatoa mwaliko kutoishi nusu nusu.

Kwa maelezo yake alitaka “kupiga kengele”, akisema kwamba bidii ya  utume inasisitizwa na kuishi kwao kwa usalama na faraja, wakati sio kilomita nyingi kutoka hapo, vita na mateso ni utaratibu wa kila siku. Kutokana na hilo, Papa ametoa mwaliko wa kuchukua maisha mikononi ili kusaidia ulimwengu uweze kuishi kwa amani. “Tujiruhusu kusumbuliwa na hilo, kila mmoja wetu ajiulize: ninafanya nini kwa ajili ya wengine, kwa ajili ya Kanisa, kwa ajili ya jamii? Je, ninaishi nikifikiria mema yangu mwenyewe au ninajiweka kwenye mstari mbele kwa ajili ya mtu fulani, bila kuhesabu maslahi yangu? Tujiulize juu ya utovu wetu, juu ya uwezo wetu wa kupenda kulingana na Yesu, yaani kutumikia”.

Tazama inavyopendeza
Tazama inavyopendeza

Baba Mtakatifu Francisko alipenda kuelezea jambo moja la mwisho kwa  kushirikisha, ukurasa wa Injili unaofupisha kile walichosema. “Mwaka mmoja na nusu uliopita nilikuwa hapa kwa Kongamano la Ekaristi; katika Injili ya Yohana, sura ya 6, kuna ukurasa mzuri wa Ekaristi ambao una kijana katikati yake. Unasimulia juu ya mvulana aliyekuwa katika umati wa watu akimsikiliza Yesu. Pengine alijua kwamba mkutano ungechukua muda mrefu na alikuwa ameona kwa mbali akaondoka  na chakula cha mchana.(Papa ameuliza ikiwa na wao wameleta chakula hapo kwa kuwachkesha). Lakini Yesu alihurumia umati na alitaka kuwalisha; kisha, kwa mtindo wake, aliwauliza wanafunzi maswali ili kufungua nguvu zao. Aliuliza mmoja wao jinsi gani ya kufanya hivyo na jibu la mhasibu linafika: “Mikate ya dinari mia mbili haitoshi hata kila mtu kupokea kipande” (Yn 6: 7). Kwa maneno mengine: haiwezekani kihesabu. Wakati huohuo, mwingine alimwona mvulana huyo na kufanya uchunguzi, lakini kwa mara nyingine tena mwenye kukatisha tamaa alisema: “Huyu hapa mvulana ambaye ana mikate mitano ya shayiri na samaki wawili; lakini hii ni nini kwa watu wengi?” (Yh 6, 9). Badala yake, zinatosha na zaidi kwa Yesu kufanya muujiza maarufu wa kuzidisha mikate na samaki, Papa amesisitiza.

Wanakwaya walioongoza nyimba wakati wa mkutano wa vijana huko Budapest Hungaria
Wanakwaya walioongoza nyimba wakati wa mkutano wa vijana huko Budapest Hungaria

Lakini hata hivyo, Injili haisemi kwa undani, ambayo inaacha mawazo yetu: je  ni jinsi gani wanafunzi waliweza kumshawishi kijana huyo kutoa kila kitu alichokuwa nacho? Labda walimwomba aandae chakula chake cha mchana na akatazama huku na huko, akiwaona maelfu ya watu. Na pengine, kama wao, atakuwa alijibu kwa kusema: “Haitoshi, kwa nini mnaniuliza na hamshughulikii ninyi ambao ni wanafunzi wa Yesu?2. Kisha, pengine, watakuwa walimwambia kwamba ni Yesu mwenyewe aliyeomba. Na alifanya jambo la ajabu: aliamini, na akatoa kila kitu, hakujibakiza chochote. Alikuwa amekuja kupokea kutoka kwa Yesu na anajikuta akimpatia Yesu. Lakini ndivyo muujiza hutokea. Inatokana na kushiriki: kuzidisha kunafanywa na Yesu kunaanza na kushiriki kwa kijana huyo pamoja naye na kwa wengine.

Kijana  mdogo huyo aliye mikononi mwa Yesu anakuwa mengi. Hapo ndipo imani inapopelekea: kwenye uhuru wa kutoa, kwa ari ya kutoa, kushinda woga, kujihusisha! Papa ameongeza kuwaleza kwamba, kila mmoja wao ni wa thamani kwa Yesu, na pia kwakwe yeye! “Kumbuka kwamba hakuna mtu anayeweza kuchukua nafasi yako katika historia ya Kanisa na ya ulimwengu: hakuna anayeweza kufanya kile ambacho wewe pekee unaweza kufanya. Hebu basi tujisaidie kuamini kwamba tunapendwa na wa thamani, kwamba tumeumbwa kwa ajili ya mambo makuu. Tuombe kwa ajili ya hili na tujitie moyo katika hili! Na kumbukeni pia kunitendea wema kwa maombi yenu. Köszönöm! Yaani Asante! Amehitimisha Papa.

Hotuba kwa vijana nchini Hungaria
29 Aprili 2023, 18:17