ÐÓMAPµ¼º½

Papa awashukuru sana watu wa kujitolea na makundi ya huduma za upendo

Papa Francisko alihitimisha siku yake ya pili ya Ziara ya Kitume huko DRC kwa kukutana na wawakilishi kutoka katika makundi mbali mbali ya upendo pamoja na watu wao waowahudumia.Aliwashukuru sana kwa huduma yao msingi kwa walio katika mazingira magumu.Habari ni katika video fupi na picha.

Na Angella Rwezaula; - Vatican

Papa Francisko akihutubia kundi la wawakilishi wa baadhi ya mashirika ya kutoa misaada akiwa katika Ukumbi wa Ubalozi wa Vatican huko  Kinshasa siku ya Jumatano, alaisiti tarehe Mosi Februari 2023  aliwasifu  kwa kazi yao ambayo, alisema, ni kama msitu unaokua kimya kimya na kuzaa matunda, huku kukiwa na kelele za ghasia na ukosefu wa haki unaoendelea. Habari zaidi zinaweza kusomeka katika picha:

Papa alikutana na makundi ya kutoa misaada kwa wahitaji
Papa alikutana na makundi ya kutoa misaada kwa wahitaji
Mavazi ya utamaduni ambao walimwimbia Papa na kucheza wakati wa kukutana na makundi ya utoaji msaada
Mavazi ya utamaduni ambao walimwimbia Papa na kucheza wakati wa kukutana na makundi ya utoaji msaada

Waliohudhuria mkutano huo kwa hiyo ni waendeshaji na wanufaika wa mashirika sita ya kutoa misaada na taasisi ambazo walielezea  juu ya uzoefu wao na kuwasilisha shughuli zao katika nyanja za afya, elimu, na maendeleo ya watu kwa maskini na waliotengwa.

Papa amekutana wahitaji na wahudumu wa upendo
Papa amekutana wahitaji na wahudumu wa upendo
Mlemavu akimpelekea zawadi Papa
Mlemavu akimpelekea zawadi Papa

Hawa ni pamoja na watu walioathiriwa na aina mbalimbali za ulemavu, na ugonjwa wa Hansen na magonjwa mengine kama ukimwi, vipofu, viwete na viziwi. Miongoni mwao, kuna hata kituo cha DREAM (Msaada wa Magonjwa kwa Njia Bora na za Juu) cha Jumuiya ya Mtakatifu Egidio.

Papa alikutanana wahitaji na watoa huduma ya upendo
Papa alikutanana wahitaji na watoa huduma ya upendo
Baadhi ya watoto waliowakilisha wenzao ambao wanatunzwa na makundi ya upendo
Baadhi ya watoto waliowakilisha wenzao ambao wanatunzwa na makundi ya upendo

Kikundi kingine ni Fasta Association, shirika la kibinadamu lenye makao yake makuu nchini Argentina, ambalo lengo lake ni kuhamasisha  kijamii na kujumuisha watu waliotengwa kupitia malezi na jumuiya, shirika la ushiriki, na Telema Ongenge ambacho ni chama cha ndani kinachosaidia watu wenye ulemavu  katika kuboresha hali zao za maisha.

Mkutano wa Papa na wahitaji na wahudumu wao wa upendo
Mkutano wa Papa na wahitaji na wahudumu wao wa upendo

Katika makundi hayo pia kulikuwa na watawa wa Kirappist wa Mama Yetu wa Mvanda, huko Kikwit.

Hawa ni watawa wa kitrapisti
Hawa ni watawa wa kitrapisti
Furaha ya Papa kukutana na wahudumu wa upendo na wahitaji
Furaha ya Papa kukutana na wahudumu wa upendo na wahitaji
Wawakilishi wa Makundi ya Upendo
Wawakilishi wa Makundi ya Upendo
02 Februari 2023, 09:31