Papa awashukuru sana watu wa kujitolea na makundi ya huduma za upendo
Na Angella Rwezaula; - Vatican
Papa Francisko akihutubia kundi la wawakilishi wa baadhi ya mashirika ya kutoa misaada akiwa katika Ukumbi wa Ubalozi wa Vatican huko Kinshasa siku ya Jumatano, alaisiti tarehe Mosi Februari 2023 aliwasifu kwa kazi yao ambayo, alisema, ni kama msitu unaokua kimya kimya na kuzaa matunda, huku kukiwa na kelele za ghasia na ukosefu wa haki unaoendelea. Habari zaidi zinaweza kusomeka katika picha:
Waliohudhuria mkutano huo kwa hiyo ni waendeshaji na wanufaika wa mashirika sita ya kutoa misaada na taasisi ambazo walielezea juu ya uzoefu wao na kuwasilisha shughuli zao katika nyanja za afya, elimu, na maendeleo ya watu kwa maskini na waliotengwa.
Hawa ni pamoja na watu walioathiriwa na aina mbalimbali za ulemavu, na ugonjwa wa Hansen na magonjwa mengine kama ukimwi, vipofu, viwete na viziwi. Miongoni mwao, kuna hata kituo cha DREAM (Msaada wa Magonjwa kwa Njia Bora na za Juu) cha Jumuiya ya Mtakatifu Egidio.
Kikundi kingine ni Fasta Association, shirika la kibinadamu lenye makao yake makuu nchini Argentina, ambalo lengo lake ni kuhamasisha kijamii na kujumuisha watu waliotengwa kupitia malezi na jumuiya, shirika la ushiriki, na Telema Ongenge ambacho ni chama cha ndani kinachosaidia watu wenye ulemavu katika kuboresha hali zao za maisha.
Katika makundi hayo pia kulikuwa na watawa wa Kirappist wa Mama Yetu wa Mvanda, huko Kikwit.