MAP

Bikira Maria ni Mama wa Mungu Bikira Maria ni Mama wa Mungu  

Papa:Maria anatufundisha kusikiliza kilio cha waliosahauliwa!

Katika ujumbe wa Papa Francisko kwa washiriki wa Kongamano la 25 la Elimu ya Maria kimataifa,iliyanza 8-11 Septembakwa njia ya mtandao,anasema Mama wa Yesu anafanya kuzaliwa ulimwengu wa udugu mahali ambamo kuna nafasi ya kila aliyetupwa.Na Roho anaendelea kutueleza kuwa nyakati ambazo tunaishi ni nyakati za Maria.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Papa Francisko ametuma ujumbe wake kwa washiriki wa Kongamano la 25 la Elimu ya Maria kimataifa kuanzia tarehe 8 hadi 11 Septemba 2021, linalofanyika kwa njia ya mtandao. Katika ujumbe huo, Papa Francisko anawaeleza jinsi anavyoshiriki kwa moyo wote furaha yao ya kuadhimisha hata kama ni kwa njia tofauti ya kongamono hilo linaongozwa na mada ya “Maria kati ya Taalimungu na tamaduni za leo hii. Mitindo, mawasiliano na matarajio”. Furaha yetu isisahau kilio cha ukimya cha kaka na dada ambao wanaishi hali za matatizo makubwa yaliyosababishwa na janga. Furaha ya kweli ambayo inatoka kwa Bwana, daima inatoa nafasi kwa sauti zilizosahauliwa, kwa sababu pamoja nao inawezekana kujenga wakati ujao ulio bora. Maria katika uzuri wa kufuasa kiinjilina katika huduma ya wema wa pamoja wa ubinadamu na sayari, anaelimisha daima kusikiliza sauti hizi na Yeye mwenyewe anakuwa sauti ya wasio kuwa nazo, ili kuzaaa ulimwengu mpya mahali ambamo sisi sote ni ndugu, mahali ambamo kuna nafasi ya kila aliyetupwa katika jamii zetu.(Waraka Fratelli tutti, 278).

Kwa zaidi ya miaka 60 ya shughuli za Taasisi ya Kipapa ya Elimu ya Maria Kimatifa, Papa amesema kuwa inaratibu na kuunganisha tamaduni za Maria katika ulimwengu mzima  hasa kwa njia ya kuadhimisha Kongamano la Maria Kimataifa kama hilo. Na imeweza kutoa ufahamu na maoni katika enzi inayobadilika kwa haraka, kwa namna ya kuishi, ya mahusiano, kuwasiliana na kulifanyia kazi wazo, kujihihusisha kati ya kizazi cha kibinadamu na kuelewa na kuishi imani.Kongamano hizi ni shuhuda zilizo wazi kwa jinsi ambavyo elimu ya Maria inakuwa ya lazima katika mazungumzo kati ya tamaduni, uwazi wa kukuza udugu na amani. Papa Francisko amesema kuwa, tunaelewa kwa dhati kuwa taalimungu na utamaduni unaotokana na ukristo umekuwa wa hali ya juu katika utume wake hasa ulipotambua kuishi katika hatari na kwa uaminifu kwenye mipaka. (Veritatis gaudium, 5).

Na kuhusiana na mipaka, Mama wa Bwana anaonekana  uwepo wake maalum; Kwa sababu yeye ni mama wa wote, kutegemeana na kabila au taifa. Kwa namna halisi ya Maria amekuwa sehemu  ya kuanza kwa utamaduni na wenye uwezo wa kushinda vizingiti ambavyo vinaweza kuunda migawanyiko. Kwa njia hiyo katika safari ya utamaduni huo wa kidugu, Roho anatuita kupokea kwa upya ishara ya faraja na uhakika wa tumaini ambalo linatokana na lina jina, sura, moyo wa Maria, mwanamke, mwanafunzi, mama na rafiki. Safari hiyo ndefu ambayo Roho anaendelea kutueleza kuwa nyakati ambazo tunaishi ni nyakati za Maria. Taasisi ya Elimu ya Maria kimataifa, inahifadhi katika jitihada za upyaisho, inatafuta kusoma alama za nyakati kwa ajili ya faida ya Kanisa na kwa ajili ya mwanamke na mwanaume mwenye mapenzi mema. Fumbo ambalo linafumbatwa kwa Maria linajifunga ndani mwake fumbo lile lile la Neno la Mungu aliyejifanya mtu.

08 Septemba 2021, 16:26