Smirne,Kanisa linalotaka kukua katika mazungumzo!
Vatican News
Katika hafla ya safari iliyoandaliwa na Shirika la kuandaa hija mbali mbali katika maeneo matakatifu liitwalo “Opera romana pellegrinaggi”, kwa ushirikiano wa Ofisi ya Utamaduni na Habari ya Ubalozi wa Uturuki, katika kumbukumbu ya miaka 1700 ya Mtaguso wa Kikristo wa Nikea kwenye pwani ya magharibi ya Nikea, iliandaa Hija iitawayo "Mitaguso ya Nikea ammbapo Vatican News ilipata fursa ya kukutana na Padre Alessandro Amprino, Kansela wa Jimbo Kuu la Smirne nchini Uturuki, kando ya fursa hiyo ambaye aliwapeleka sehemu kadhaa za pwani ya Nikea. Katika maelezo yake kuhusu furusa hii alisema: “Sisi ni Kanisa ambalo hapa lina fursa ya kukua katika mazungumzo na wale ambao sio Wakristo, na vile vile kwa kawaida na jumuiya nyingine ndogo za Kikristo, kama vile Waorthodox au Waanglikani, ambao tayari kuna uhusiano bora. Kinachoshangaza ni kwamba tunaweza kuifanya kwa nguvu na upatikanaji kwa usahihi zaidi kwa sababu sote tunakabiliwa na changamoto ya kuwa wachache: ni rahisi kwetu kupatana.” Hata pamoja na taasisi za ulimwengu wa Kiislamu “kuna uhusiano chanya wa ushirikiano. Hatimaye, kama katika mambo yote, ni suala la ubinadamu na akili.”
Katika Parokia zetu tunaweza kufanya kila kitu
Padre huyo, mwenye asili ya Torino, Italia, aliviambia vyombo vya habari vya Vatican kwamba, "hata kukiwa na mapungufu, ndani ya jumuiya na parokia zetu tunaweza kufanya karibu kila kitu, tuna uwezo wa kutenda katika maisha ya kila siku na shughuli za kawaida zinazoonesha maisha yetu ya Kikristo. Bila shaka kuna changamoto, kwa sababu kwa wazi sehemu nzima ya nje ni ngumu zaidi, lakini tuko hapa kuishi maisha yaliyoongozwa na Injili, kuonesha maadili ya kibinadamu. Heshima na udadisi hujenga uhusiano na wengine.”
Kipimo cha kihistoria cha Kanisa
Kinachokugusa unaposafiri kutoka kusini hadi kaskazini kando ya pwani ya Uturuki ya leo ambayo inatazama moja kwa moja Bahari ya Aegean ni "mwelekeo wa kihistoria wa Kanisa, ambalo kutoka hapa limekuwa la ulimwengu wote, na hii ndiyo iliyonivutia mara ya kwanza nilipokuja Smirna, mwaka wa 2017, nikiitwa na rafiki ambaye alikuwa ameniomba nimsaidie wakati wa Noeli. Mimi husema kila mara, nikizungumzia historia yangu ya kibinafsi, kwamba nilialikwa kwa mara ya kwanza; Kisha nilihisi kuitwa, na kwa sababu hiyo hatimaye nilikaribishwa." Kwa kweli, kutoka Antiokia ya Orontes hadi Efeso, hadi Nikea, kila kitu kinazungumza juu ya vipimo vya asili vya Ukristo, ambao mambo yake muhimu katika nchi hizi yamefafanuliwa au kufafanuliwa kwa namna fulani (uwiano kati ya Baba na Mwana; na umama wa Maria Mama wa Mungu, Imani ya Nikea ya Constantinopoli) kuwa nguzo ambazo imani katika Kristo inakaa leo hii. Urithi wa kidini, wa kitaalimungu, wa kihistoria, wa kisanii, wa kipekee katika thamani yake.
Thamani ya Mtaguso wa Nikea leo hii
Miaka 1700 ya Mtaguso huo uliofanyika Nikea kwa amri ya Mfalme Constantine (325 BK) inatoa leo hii mfululizo wa vipengele vya kutafakari. Padre Amprino alisema "Kwanza kabisa uimara na uzuri wa imani yetu, ambayo ina mizizi ya kina katika Kristo na katika kutafakari kwa Kanisa. Kwa maadhimisho haya tunaweza kugundua upya mizizi yetu kukua leo. Ni ugunduzi upya ambao kila mtu anaweza kufanya, hasa wale wanaoishi nje ya dunia hii. Kwa sisi tulio hapa, inamaanisha kuweka hai mwali wa asili na kuwa mlango wazi kwa kila mtu. Pili, ushuhuda kwa Wakristo wote kwamba ni hasa katika mizizi hii kwamba tunaweza kuwa na umoja: shina ni sawa, na hivyo ni damu ya maisha, na kisha kuna matawi, "tofauti lakini kuunganishwa na kituo kimoja. "Kutoka hapa, hatua nyingine, thamani ambayo mazungumzo ya kiekumene inayo, ambayo Uturuki inaweza kuwa maabara." Bila kusahau kiasi cha maamuzi muhimu yaliyofuata, yaliyochukuliwa kwenye Mtaguso wa Efeso mwaka 431 BK, ambao ulianzisha kuhusu,Maria Mama wa Mungu".
Umuhimu wa Jubilei inayojitolea kwa matumaini
Maadhimisho ya Mtaguso wa kwanza wa Nikea yanaangukia kwa usahihi katika Mwaka Mtakatifu wa Jubilei kuu ya 2025 uliowekwa wakfu kwa ajili ya matumaini, kiasi kwamba hata Papa Francisko, katika Hati ya kutangaza Jubilei kuu, alitaka kutaja, akielezea matumaini ya kuweza kuwa hapa katika mwezi wa Mei kwa sherehe zake. Kwa maelezo ya Padre Amprino, ambaye pia ni mtu wa mawasiliano ya Baraza la Maaskofu ya Uturuki kwa Jubilei alisema: "Kwa maana hii zaidi ya yote tunasaidia waamini kuelewa Mwaka Mtakatifu ni nini, kwa nini unaadhimishwa. Hii inaweza kuonekana kama habari dhahiri, lakini sivyo. Katika kipindi hiki pia tumefanya kazi ya kutambua makanisa ya Jubilei, ambapo mtu anaweza kupata msamaha wa jumla kama huko Roma au katika Nchi Takatifu." Makanisa hayo ni: huko Istanbul, Kanisa kuu na Kanisa la Kuzaliwa kwa Mama yetu huko Büyükdere (ambapo shambulio lilitokea mnamo 2024); Parokia ya Bursa; katika Smirna Kanisa kuu na Kanisa la Mtakatifu Polycarp; Madhabahi ya Meryem Ana (Nyumba ya Maria huko Efeso); Kanisa la Konya, katika sehemu ya kati-kusini ya nchi, jiji ambalo pia lilitembelewa na Mtakatifu Paulo, kulingana na Matendo ya Mitume, na ambayo kutoka 1097 hadi 1243 ilikuwa mji mkuu wa Sultanate ya Rûm (au Sultanate ya Ikoniamu), iliyoundwa na Seljuk ambao walikuwa wamechukua Anatolia; hatimaye, Kanisa la Watakatifu Petro na Paulo huko Antiokia. Kwa kifupi, "tunajaribu kuweka misingi ili Jubilei iweze kufikiwa na wote na ujumbe wake umfikie kila mtu: tunataka kila mtu, kwa njia yake ndogo, atilie shaka wajibu wake wa kuhakikisha kwamba tukio kama hilo linazaa matunda."