Giubilei 2025:zaidi ya watu wa Kujitolea 5000 wa"Huruma Italia wanafika Roma!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Katika fursa ya Jubilei ya watu wa kujitolea itakayofanyika tarehe 8 na 9 Machi 2025 mjini Vatican kama mwendelezo wa Mwaka Mtakatifu wa Jubilei 2025, hatuna budi kujikumbusha tafakari ya Papa Francisko kuhusu ulimwengu huu wa Kujitolea ambapo mara nyingi alitoa mwaliko wa mshikamano wakusaidia wengine, kutazama jirani na kwa kila mtu mwenye kuhitaji. Moja ya nia za Papa Francisko kwa mwezi Desemba 2022 aliyokabidhi kwa Kanisa lote la Ulimwengu kupitia Mtandao wake wa Maombi kimataifa, Papa alisema: "Tuombee ili mashirika ya kujitolea na kuhamasisha watu yapate watu wenye shauku ya kujitolea kwa manufaa ya wote na kutafuta njia mpya za ushirikiano katika ngazi ya kimataifa."
Ulimwengu unahitaji watu wa kujitolea
Papa Francisko alisema kwamba "Ulimwengu unahitaji watu wa kujitolea na mashirika ambayo yanataka kujitolea kwa manufaa ya wote na anaona kwamba neno kujitolea ni neno ambalo wengi leo wanataka kufuta. Na badala yake kuna haja ya silaha zinazotoa msaada. Kuwa mwanakujitolewa wa mshikamano ni chaguo linalotufanya kuwa huru; hutufanya tuwe wazi kwa mahitaji ya wengine, kudai haki, kutetea masikini, kwa utunzaji wa uumbaji." Kwa mazoezi, kunatia ndani kuwasikiliza wengine na kujitahidi kujitoa ili kuendeleza maendeleo ya kibinadamu. Papa Francisko alisema kuwa mwanakujitolea kunamaanisha kuwa mafundi wa huruma: kwa mikono yetu, kwa macho yetu, kwa masikio yetu makini, kwa ukaribu wetu.” Na kisha “kuwa mtu wa kujitolea kunamaanisha kufanya kazi na watu unaowahudumia. Si kwa ajili ya watu tu, bali na watu.”
Kujitolea ni urithi wa kuimarishwa
Ni katika muktadha huu ambapo watu wa kujitoleza zaidi ya 5,000 wa chama cha Huruma cha Italia watashiriki na wenzao kutoka Ulimwenguni kote katika Jubilei ya Kujitolea, iliyoratibiwa mjini Roma kuanzia Jumamosi tarehe 8 hadi Dominika tarehe 8 na 9 Machi 2025. Katika ratiba yao Jumamosi alasiri, kikundi cha watu waliojitolea kutoka “Misericordie,” Huruma wakiongozwa na Msimamizi msaidizi wa Kitaifa, Askofu Franco Agostinelli kitakwenda kusali mbele ya Hospitali ya Gemelli Rozari kwa kufanya papa ahisi ukaribu wa Harakati hiyo ambaye amelazwa katika hospitali Roma tangu Februari 14. Pia Jumamosi hiyo tarehe 8 Machi katika Kanisa la Mtakatifu Salvatore huko Lauro, watu wa kujitolea watashiriki katika misa inayoongozwa na Askofu Agostinelli, ikifuatiwa na maandamano hadi kwenye Mlango Mtakatifu wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro. Wakati huo huo, kuanzia asubuhi saa 3:30 hadi 11:00, Katika Ukumbi wa Kanisa la Roho Mtakatifu (Santo Spirito) utakuwa mwenyeji wa warsha inayoongozwa na mada: "Kujitolea ni urithi wa kuimarishwa", wakati huo huo kuanzia saa 5:00 hadi 12:00 jioni katika Uwanja wa Kanisa la Mtakatifu Salvatore huko Lauro,Kikundi cha wanakujitolea wa Huruma kitakuwepo na eneo kubw, kujitolea kwa uhifadhi wa bure wa utume wa Afya.
Jibilei ya Ulimwengu wa kujitolea 8-9 Mchi 2025
Shukrani kwa ushirikiano wa Taasisi ya Afya IDI ya Bikira Maria, Kikundi cha Jengo la Benedetta, Uzoefu wa Sauti ya Kituo cha Muziki, Jumuiya ya Kiitaliano ya Saikolojia ya Dharura, A.S.Pro.C. na Wanasaikolojia wa Watu, madaktari wa kujitolea na wafanyakazi wa afya waliohitimu watatoa ushauri na uchunguzi katika nyanja mbalimbali, ikiwa ni pamoja na magonjwa ya moyo, ngozi, mifupa, watoto, kisukari,wataalamu wa matatizo ya upasuaji wa kichwa na shingo (otorhinolaryngology)na ( audiology) wataalamu wa masikio . Huduma za uchunguzi kama vile uchunguzi wa ultrasound na Xray, kipimo cha shinikizo la damu, uchanganuzi wa gesi ya damu, oximetry ya mapigo ya moyo na usaidizi wa kisaikolojia pia zitapatikana, pamoja na dawati la mwelekeo wa afya na kijamii, kwa uangalifu maalum kwa watu walio katika hali ya pembeni. Pia siku ya Jumamosi tarehe 8 Machi, kutakuwa na tukio la nafasi ya kuelezea shughuli ya Harakati hii ya Huruma (Misericordie), maana yake ni nini. Kitovu cha siku hizi mbili kitakamilisha Dominika tarehe 9 Machi 2025 wakati Harakati hiyo na wengine kutoka Ulimwengu wa Kujtolea watakaposhiriki Ibada ya Misa ya Jubilei katika Uwanja wa Mtakatifu Petro.