ĐÓMAPµĽş˝

2025.03.18 Askofu Willy Ngumbi, wa Goma,Congo DR: 2025.03.18 Askofu Willy Ngumbi, wa Goma,Congo DR: 

Askofu wa Goma,DRC:Hatua za kijeshi sio suluhisho

Katika mahojiano na Vatican News,Askofu Willy Ngumbi Ngengele anaelezea matumaini yake kwa maazimio ya amani,kuchagua mazungumzo kutafuta njia ya amani na umoja wa nchi.

Na Christian Losambe,SJ na Kielce Gussie

Mvutano na mzozo unaendelea kushuhudiwa katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kati ya vikosi vya serikali na waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda. Licha ya majaribio kadhaa yaliyoshindikana ya kuleta amani kupitia mazungumzo, Askofu Willy Ngumbi Ngengele wa Goma aliviambia vyombo vya habari Vatican kwamba "hali inaonekana haijabadilika sana" tangu kuongezeka kwa migogoro mwishoni mwa Januari. Hata hivyo, katikati ya ghasia, alisifu ujasiri na uamuzi ambao idadi ya watu wanakabiliwa nayo janga hili, ambalo limedumu kwa zaidi ya miongo mitatu.

Watu wanaishi kwa hofu

Imepita takriban miezi miwili tangu Goma ilipochukuliwa na waasi wa M23 na Askofu Ngengele alieleza kuwa hali haijabadilika sana. "Tofauti pekee ni kwamba vita haviko tena Goma, lakini vimehamia maeneo mengine ya Jimbo," alielezea. Watu "wanazidi kuishi kwa hofu" kwani utekaji nyara na mauaji ni sehemu ya kawaida. Kila siku maisha yamebadilika sana na imekuwa vigumu kulala usiku huku majambazi wenye silaha wakiingia majumbani kwa ajili ya kupora pesa na kupora mali nyingine," Askofu Ngengele alisimulia.

Kuongezeka kwa umaskini katika msimu wa Kwaresima

Hata hivyo, licha ya mzozo huo, Lanisa la Askofu Ngengele lilijaa siku ya Jumatano ya Majivu kuashiria mwanzo wa Kipindi cha Kwaresima tarehe 5 Machi 2025. Askofu wa Goma alieleza mshangao wake kwamba “katika parokia zote za jiji hilo, hali ilikuwa sawa licha ya hali ya usalama. Zaidi ya suala la usalama, hali ya kiuchumi pia ni mbaya, kwani benki zimefungwa tangu waasi waliposhambulia mji wa Goma mwishoni mwa Januari. "Watu, hasa wafanyabiashara, wananyimwa uwezo wa kujikimu. Zaidi ya hayo, wafanyakazi wa serikali hawapokei mishahara yao na wazazi wanatatizika kulipia ada ya masomo ya watoto wao, Askofu Ngengele alisema.

Kuishi kipindi cha Kwaresima licha ya migogoro

Kiwango cha umaskini kinapoongezeka katika eneo hilo, Askofu alisema kwamba Wakristo wanaweza kutumia msimu huu wa Kwaresima “kutumaini mustakabali ulio bora zaidi, wakati ujao wa amani.” Alisema hata pamoja na idadi ya changamoto, "wanaendelea kuonesha mshikamano wao kwa wao, hasa kwa maskini zaidi, watu waliohamishwa na vita, ambao wengi wao ni familia za kijeshi.” Ili kuishi katika kipindi cha Kwaresima, Wakristo wa mahali hapo wamepanga hija - nje ya Goma- na mazoezi ya kiroho katika ngazi ya parokia. Kituo cha Kichungaji cha Jimbo kiliunda vikundi na wahuishaji wa kichungaji kwenda parokiani na mapadre na kuandaa kampeni za uinjilishaji. Hudhurio ni kubwa, ingawa mikutano hiyo “hushughulikia mada ambazo si rahisi sikuzote, kama vile kupenda adui, msamaha, au kushiriki kumunio. Kampeni hizi zimefanikiwa sana.” Askofu Ngengele alikazia kwamba Wakristo mahalia “wanaendelea kuhubiri upendo wa kidugu na umoja wa Kikristo, uwazi kwa wengine, hata wale ambao si Wakatoliki.”

Hatua za kijeshi sio suluhisho

Mazungumzo ya amani kati ya vikosi vya serikali na waasi wa M23 huko Luanga, Angola yalipangwa kufanyika Jumanne tarehe 18 Machi 2025. Siku moja kabla, kundi la M23 lilitangaza kujiondoa, likitaja vikwazo vya kimataifa dhidi ya wanachama wao kuwa kikwazo cha mazungumzo. Angola iliwekwa kuwa mpatanishi kati ya makundi hayo mawili. Askofu Ngengele alielezea kusikitishwa kwake na maendeleo haya. Kwake yeye, mazungumzo ni sehemu muhimu ya kupata amani. Lakini anatumaini kuwa walio madarakani wanaweza kutetea mazungumzo. "Hatuamini sana katika suluhisho la kijeshi kwa mzozo huu, kwani vita huharibu maelfu ya maisha na itaongeza pengo la umaskini katika eneo hilo."

20 Machi 2025, 15:23