ĐÓMAPµĽş˝

Kinachobaki na kuendelea kwa uharibifu kutokana na mapigano kati ya waasi wa M23 na wanajeshi wa Congo huko Goma. Kinachobaki na kuendelea kwa uharibifu kutokana na mapigano kati ya waasi wa M23 na wanajeshi wa Congo huko Goma.  (ANSA)

Ujumbe wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Afrika ya Kati:Mamlaka za DRC suluhisheni mzozo haraka!

Moyo unaotoka damu,kwa niaba ya Maaskofu wa nchi zetu tatu za Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Afrika ya Kati(ACEAC),tunashiriki machungu ya wale wote waliopoteza wanafamilia au wapendwa wao,katika safu ya askari na raia wasio na hatia,pamoja na watoto.Tunalaani ghasia mbaya ambazo zinaendelea kuleta maombolezo katika kanda yetu ndogo na ambazo,kwa mara nyingine tena,zimelitumbukiza jiji la Goma katika dhiki na kukata tamaa.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Afrika ya Kati (ACEAC) wametoa ujumbe u uliosainiwa na Rais wa Shirikisho hili, Askofu  José MOKO, tarehe 6 Februari 2025 huko Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Ujumbe huo kwa Wakristo na Watu wenye mapenzi mema  katika Ukanda Mdogo wa Maziwa Makuu Kuhusu Tukio la Mapigano ya Silaha katika Jiji la Goma katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Ujumbe huo unaongozwa na kifungu cha kibiblia kisemacho: "Kwa kuwa wanadamu wameshiriki damu na mwili; basi ilimpasa kuwa kama ndugu zake katika mambo yote" (Waebrania 2:14-18). Ujumbe huo unabainisha kuwa: Ndugu wapendwa, Siku chache kabla ya kuadhimisha sikukuu ya Kikatoliki ya Kutolewa kwa Bwana wetu Hekaluni, mnamo tarehe 2 Februari 2025, kanda ndogo ya Maziwa Makuu ilitikiswa tena na kuzuka tena kwa mapigano makali ya kutumia silaha katika mji wa Goma katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Hii ilisababisha hasara nyingi za maisha ya binadamu, kuongezeka kwa watu wengi kuhama makazi yao, kuzorota kwa mazingira magumu ya watu walio katika dhiki, mmomonyoko wa mitaji ya uaminifu kati ya watu na/au jamii, na tishio la maafa ya kibinadamu ambayo yanakumbuka kurasa za giza katika historia ya kanda. Moyo unaotoka damu, kwa niaba ya Maaskofu wa nchi zetu tatu za Shirikisho la Maaraza ya Maaskofu Afrika ya Kati(ACEAC), tunashiriki machungu ya wale wote waliopoteza wanafamilia au wapendwa wao, katika safu ya askari na raia wasio na hatia, pamoja na watoto wadogo. Tunalaani ghasia mbaya ambazo zinaendelea kuleta maombolezo katika kanda yetu ndogo na ambazo, kwa mara nyingine tena, zimelitumbukiza jiji la Goma katika dhiki na kukata tamaa.

Kurejea mpango wa kichungaji wa ACEAC wa amani kama ulivyobuniwa huko Roma mnamo Oktoba 2023, na kuanza kutumika Goma mnamo Januari-Februari 2024:  tunatoa wito kwa wawakilishi wa mamlaka ya kisiasa katika kanda ndogo na vile vile katika Afrika na Duniani, kulingana na majukumu yao, kushiriki katika utatuzi wa mgogoro ambao unatanguliza kukuza utu wa kila mtu, na heshima kwa haki za watu binafsi na watu;  tunawaalika mabinti na wana wote wa eneo dogo kuungana ili kuondokana na hali ya mgawanyiko na chuki ambayo inaweza tu kusambaratisha mfumo mzima wa kijamii na kuendeleza wimbi la vurugu; tunahimiza ufahamu na wajibu wa mshikamano kati ya binadamu kusaidia wale ambao wameteseka na kuzuia mahitaji mabaya yanayotokana na hali ya vita;

Maaskofu aidha wanabainisha kuwa "tunahitaji mshikamano wa mashirika yote na watu wenye mapenzi mema ili kuwasaidia watu wanaoteseka; tunatoa wito kwa haraka kwa wavuvi katika maji yenye shida, wale wanaovuta kamba kwenye vivuli, watengenezaji wa habari za uwongo na wale wanaoeneza habari potofu na bidhaa zenye sumu, wasitengeneze hali mpya zinazoweza kusababisha machafuko; tunapendekeza kwamba jumuiya za Kikristo ziwatunze waathiriwa, waliojeruhiwa na waliohamishwa, na kuomba kwamba mwali wa amani usizime, na tumaini hilo lisifie katika upeo wetu; tunaendelea kuvumilia kwa matumaini ya mchanganyiko wa juhudi za mamlaka wote kwa nia ya suluhisho la kikanda yenye uwezo wa kuchangia kwa njia ya kudumu katika ujenzi wa amani.

Tumefanywa kwa mwili na damu, na wote walioumbwa kwa sura na mfano wa Mungu, sisi ni wanadamu wenzenu ambao Mwana Mungu amejifanya kuwa ndugu, kama vile Mtakatifu Paulo atangazavyo katika barua yake kwa Waebrania: “Kwa kuwa wanadamu wameshiriki damu na mwili, Yesu naye alishiriki yayo hayo, ili kwa njia ya mauti akawaweka huru wale ambao kwa hofu ya mauti walipitia maisha yao yote katika utumwa. Na kwa sababu alipatwa na jaribu la Mateso yake hadi mwisho, anaweza kuwasaidia wale wanaopitia majaribu. (Waebrania 2:14…18). Bikira Maria aliyemsindikiza Mwanae Hekaluni ili kumkabidhi kwa Bwana, atulie leo hii, yeye anayetushauri juu ya njia hiyo, anayetusindikiza katika njia hiyo na kutia ndani yetu nguvu ya matumaini ya amani ya kudumu.”

Shirikisho la Maaskofu Afrika ya Kati kuhusu DRC
07 Februari 2025, 17:48