MAP

Sr  Maria Rosa Venturelli, mmisionari wa Comboni, Mratibu wa mtandao wa USMI wa kupambana na Biashara haramu wy binadamu Sr Maria Rosa Venturelli, mmisionari wa Comboni, Mratibu wa mtandao wa USMI wa kupambana na Biashara haramu wy binadamu 

Sr. Venturelli,Biashara haramu ya binadamu:hatua kali za kijamii,kiuchumi na kikanisa

Ushuhuda wa Sr.Maria Rosa Venturelli mratibu wa mtandao wa Umoja wa Mama Wakuu Italia(Usmi)mjini Roma,aliakisi juu ya kudhoofisha kutojali kunakotufanya walioathirika wasionekane wa Biashara haramu ya Binadamu.“Ni kama utaratibu potovu ambao unawakamata na kuwaponda watu,lakini chembe chembe nyingi za mchanga,yaani mshikamano wa watu inawezekana kusababisha gia zake kukwama.”

Na  Stefano Leszczynski  na  Angella Rwezaula – Vatican.

Katika fursa ya Siku ya XI ya Kimataifa ya Sala na Tafakari dhidi ya Biashara haramu ya binadamu iliyofanyika tarehe 8 Februari, sanjari na Kumbukizi ya Mtakatifu Josephije Bakhita ni wito wa kimataifa wa kuchukua hatua na hasa(kwa watawa wote ) kwa namna ya pkee katika Jimbo kuu la Roma, ambao walieleza umuhimu wa Juma la sala na tafakari iliyotengwa kwa kutangulia mpango wa  kilele cha Siku hiyo ulioanzishwa na Baba Mtakatifu  Francisko mnamo mwaka 2015. Kulingana na Umoja wa Mataifa, takriban watu milioni 50 wanasafirishwa  ulimwenguni kote katika biashara haramu ya Binadamu. Wanaoteseka zaidi ni wanawake, watoto, wahamiaji na wakimbizi.

Mmoja kati ya waathiriwa watatu ni mtoto, wakati asilimia 79 ya watu wa unyanyasaji wa kijinsia ulimwenguni ni wanawake na wasichana. Vita, migogoro, ghasia, umaskini, majanga ya kimazingira duniani kote huwalazimisha watu kuacha makazi yao, jambo linalowafanya wawe hatarini zaidi kwa biashara haramu ya binadamu na unyonyaji kwa sababu mara nyingi wanakimbilia kwa wasafirishaji au soko nyeusi kuhama kutoka nchi moja hadi nyingine. Imeongezwa kwa hii ni aina nyingine ya usafirishaji haramu wa binadamu ambayo ni unyonyaji mtandaoni.

Kwa mujibu wa  Sr  Maria Rosa Venturelli, ambaye, pamoja na watawa  wengine 22 na walei, wanaratibu mtandao wa  (Umoja wa Mama wakuu wa Mashirika Italia (USMI),makao makuu yakiwa  Roma,  alisema kuwa:"Kuondoa hali ya kutojali ambayo hufanya aina mbalimbali za Biashara haramu zionekane ni jambo la kwanza. Ni muhimu kuchukua hatua katika viwango vyote: kijamii, kiuchumi, hata kikanisa, ninaweza kusema. Hali ya Biashara haramu wa binadamu inatisha na mara nyingi tunajaribiwa kutazama pembeni, na sio kujihusisha,” alibainisha mmisionari wa Comboni.

Mtawa huyo alidha alieleza kuwa “Hali ya utumwa ambayo ni sifa ya aina zote za biahsara haramu wa binadamu imetawaliwa na utambuzi wa uovu, ni ukweli mgumu sana kuukabili na hatari kwa usalama wa waathiriwa na wale wanaojaribu kupinga ni kweli.” "Nakumbuka msichana mdogo wa Nigeria tulimkuta amekufa kando ya barabara, ameuawa kwa sababu hakuwa na manufaa tena, ametupwa kama kitu kisichofaa. Ilichukua miezi miwili kumtambua na kumzika. Jina lake lilikuwa Issi." Wanyonyaji wanajua mkakati mmoja tu, ule wa ugaidi: "Hivi ndivyo wanavyobatilisha nia ya kumpinga mtu ambaye hana uwezo tena wa kusema itosha kwa maisha mitaani, kwa sababu kwa hofu ni vigumu kufanya uchaguzi mzuri. Sheria haisaidii kila wakati kushughulikia hali hizi, pia kwa sababu kila wakati inahitaji malalamiko kutoka kwa mhathiriwa na sio watu wote wanaohusika na biashara hiyo wana ujasiri wa kufanya hivyo. Kuna hofu kubwa ya ghasia ambazo zinahatarisha kuteseka ikiwa watakamatwa tena na wanyonyaji wao baada ya kukimbia."

Lakini pia kuna historia nyingi za ukombozi na matumaini ambazo zinaonesha jinsi kujiweka huru kutoka kwa wanyonyaji kunawezekana, wakati mwingine tu kwa kufahamu kwamba kuna njia nyingine ya kuishi: "Kulikuwa na msichana wa Salvador ambaye kwa kushangaza alipata njia ya kutoroka kutoka kwa watesi wake wa utumwa wake shukrani kwa ukweli kwamba alikamatwa na kuzuiliwa kwa miezi miwili katika CIE ya Ponte Galeria, alikumbuka Sr Maria Rosa anakumbuka. Tangu alipokuwa mtoto, aliishi katika mazingira ya udhalilishaji, yaliyooneshwa na jeuri ya mara kwa mara, na aliishia kuamini kwamba hakuna maisha mengine kwa ajili yake. Mara nyingi ni njia ya ufufuko ambao wasichana au wanawake ambao wamenusurika katika usafirishaji haramu wanaweza kupata uzoefu. Katika safari yao ya kuzaliwa upya, wao huthibitika kuwa wa kipekee, wenye nia na dhamira kuu, na wanaweza kufanya mambo makubwa.  Jambo la muhimu ni kutohukumu kamwe, lakini kuunga mkono, kumwaga tone la ubinadamu kila siku kwa dada na kaka walio hatarini zaidi."

10 Februari 2025, 14:44