Nigeria:Padre aliyetekwa nyara mjini Abuja tarehe 6 Februari awatoroka watekaji nyara wake
Vatican News.
Wakati wa kutekwa nyara kutoka kwa makazi yake huko Zuma, Baraza la Eneo la Bwari, Abuja, nchini Nigeria, Padre Cornelius Manzak Damulak wa jimbo katoliki la Shendam, alikuwa mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Veritas, Abuja. Kwa mujibu wa Shirika la habari za Kimisionari la Fides lilithibitisha maendeleo hayo kutokana na taarifa iliyotolewa na Jimbo la Shendam. Vile vile, msemaji wa Kamanda wa Polisi ya Jimbo la Niger, Wasiu Abiodun, alifahamisha vyombo vya habari kwamba Padre Damulak alipatikana karibu na barabara kuu ya Pogo-Paiko huko Minna na timu ya doria ya polisi.
"Mnamo tarehe 14 Februari 2025, muda wa saa sita mchana, mshukiwa wa utekaji nyara alipatikana akizurura karibu na barabara kuu ya Pogo-Paiko na timu ya doria ya Kitengo cha Chanchaga, na aliokolewa mara moja," ilisema taarifa hiyo. Taarifa hiyo inaongeza, "Wakati wa kuhojiwa, mwathiriwa alitambuliwa kama Cornelius Damulak, mwenye umri wa miaka 36, na mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Veritas, Abuja," Polisi wa Nigeria walisema.
Alihamishwa kutoka msitu mmoja hadi mwingine
Alitekwa nyara tarehe 6 Februari 2025, karibu saa 5.00 asubuhi, Padre Damulak alihamishwa kutoka msitu mmoja hadi mwingine na watekaji wake. Mahali ambapo Polisi walipomuokoa, ilikuwa ni dhahiri kwamba alikuwa amesafiri kwa muda mrefu. Baadaye alipelekwa kwenye kituo cha matibabu kwa uchunguzi.
Akitangaza utekaji nyara mapema mwezi huu, Chansela wa Jimbo la Shendam, Padre Joshua Daffa, alisema Dayosisi hiyo inaomba maombi. Alisema wakati huo: “Tunamkabidhi ndugu yetu, Padre Cornelius Manzak Damulak, kwa maombezi ya Mama Bikira Maria, Mama yetu, na watakatifu wote, ili kumtia nguvu na kumrudisha kwetu salama.