MAP

2025.02.05:Vijana wanaharakati dhidi ya Biashara haramu ya Binadamua huko Mtakatifu Maria Trastevere,Roma 2025.02.05:Vijana wanaharakati dhidi ya Biashara haramu ya Binadamua huko Mtakatifu Maria Trastevere,Roma  (© Marco Mastrandrea/ Talitha Kum)

Kuitwa kwa Matumaini na Uponyaji ni mkutano utakaofanyika Februari 6,Roma

Tarehe 6 Februari 2025 katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Msalaba Mtakatifu,Roma utafanyika mkutano wa “Wito wa Matumaini na uponyaji” ambao ni moja ya matukio ya maandalizi ya Siku ya XI ya Maombi na Tafakari dhidi ya Biashara haramu ya Binadamu,ifanyikayo kila ifikapo tarehe 8 Februari sanjari na siku kuu ya Mtakatifu Josphine Bakhita.Huu ni mpango wa Kimataifa wa Mama Wakuu wa Mashirika ya Kitawa(UISG) na Umoja wa Mama Wakuu(USG).

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Wito wa Matumaini na Uponyaji ni moja ya matukio kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya XI  ya Kimataifa ya Maombi na Tafakari Dhidi ya Biashara  Haramu ya Binadamu (8 Februari) tukio la maandalizi litakalofanyika katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Msalaba Mtakatifu(Santa Croce Roma), tarehe 6 Februari 2025.  Baba Mtakatifu Francisko alizindua Siku ya kwanza ya Kimataifa ya Maombi na Uhamasishaji Dhidi ya Biashara haramu ya Binadamu mnamo mwaka 2015, na maadhimisho ya mwaka huu yanaambatana na Jubilei ya Matumaini.

Kama matukio mengine kadhaa yanayotokea katika Juma hili, Wito wa Matumaini na Uponyaji unahamasishwa  na Umoja wa  Kimataifa wa Mama Wakuu wa Mashirika ya Kitawa  (UISG) na Umoja wa Mama  Wakuu (USG). Siku hii inaratibiwa  na Harakati ya Talitha Kum kwa ushirikiano na Washirika wa Mashirika. Mada kuu ya tukio la Wito wa Matumaini na Uponyaji  ambapo ni TUMAINI.

Kardinali Michael Czerny atatoa ujumbe wa kutia moyo wakati wa hafla hiyo. Wanafunzi vijana kutoka Kituo cha Kijamii na Kielimu cha Bakhita Foggia, Italia, watawasilisha onesho la moja kwa moja ambalo linaakisiwa wakati muhimu katika maisha ya Mtakatifu Josephine Bakhita-mwathirika wa biashara haramu ambaye alikuja kuwa Mtawa  na sasa ni mfano na  ishara ya ulimwengu katika  dhamira ya Kanisa Katoliki ya kutokomeza biashara haramu ya binadamu na utumwa mamboleo.

Washiriki pia watasikiliza kutoka kwa Pauline Akinyi Juma, mwathirika wa unyanyasaji wa kijinsia ambaye amekuwa mtetezi mkubwa wa waathirika wa nyanyaso za nyumbani na biashara haramu ya binadamu. Asili yake kutoka Kenya, uwezo wa ajabu wa Pauline wa kusimulia historia  hunatumika kuwa kama msukumo kwa wengine walionaswa katika misururu ya vurugu, na kuwatia moyo kuwa Mabalozi wa Matumaini, kama yeye.

Zaidi ya hayo, Balozi wa Vijana kutoka Kenya atashiriki ushuhuda wa kutia moyo dhidi ya Biashara mbaya ya binadamu. Mkurugenzi wa Sanaa aliyeshinda tuzo Lia Beltrami pia atashiriki historia zinazoangazia matumaini kwa walio hatarini kupitia kazi yake nyuma ya lenzi ya kamera. Aidha, tukio hilo litakuwa na wimbo uliorekodiwa awali na mwalimu wa zamani na mwanaharakati wa biashara haramu ya binadamu kutoka Thailand. Sasa ni Balozi wa Matumaini wa Harakati ya Talitha Kum, na kujitolea kwake kutokomeza biashara haramu ya binadamu hakuyumbishwi, licha ya ugonjwa hatari unaomkabili kwa sasa.

Hafla hiyo pia itawatambulisha baadhi ya Mabalozi wa Matumaini kutoka tasnia ya sanaa na filamu. Maonesho ya ‘Gen Verde’,kikundi cha Harakati ya Wafocolari,  Bi. Daniela Kruss, na Kwaya wa Malaika ya Degl Roma, ya  Kiafrika, itaimba  mara kwa mara katika kipindi chote cha programu hiyo.

Ratiba

Ratiba ya mkutano huo itaanzia saa 9.30 alasiri ambapo mratibu ni Sr Bernadette Reis fsp, Msimamizi Hotuba za Ufunguzi: Sr Abby Avelino M.M., Mratibu wa Kimataifa, Talitha Kum, Ujumbe kutoka UISG: Sr. Roxanne Schares, SSND, Katibu Mtendaji Mshiriki wa Mashirika ya Kitawa UISG na  Kardinali Michael Czerny, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la ajili ya kuhamasisha Maendeleo Fungamani  ya Kibinadamu watatoa mada.

Talitha KUM
05 Februari 2025, 17:01