ĐÓMAPµĽş˝

2025.02.17 Mazishi ya Padre Donald Martin Ye Naing Win aliyeuawa kikatili huko Myanmar. 2025.02.17 Mazishi ya Padre Donald Martin Ye Naing Win aliyeuawa kikatili huko Myanmar. 

Kardinali Bo aombea Padre aliyeuawa kikatili nchini Myanmar na zikomeshwe ghasia

Kardinali Charles Maung Bo wa Yangon alimwombea Padre Donald Martin Ye Naing Win wa Jimbo kuu la Mandalay,aliyeuawa kikatili nchini Myanmar na wanamgambo,huku kiongozi wa Maaskofu wa taifa hilo akitoa wito wa kukomeshwa kwa ghasia na kila kitu kifanyike ili kuhakikisha matukio ya aina hiyo hayatokei katika siku zijazo.

Na Deborah Castellano Lubov – Vatican.

Kardinali Charles Maung Bo, Rais wa Baraza la Maaskofu wa Myanmar katika ujumbe wa rambirambi aliotuma kufuatia na kifo cha Padre Donald Martin Ye Naing Win, ambaye aliuawa na kundi lenye silaha huku mzozo ukiendelea kati ya jeshi la Myanmar na vikosi vya upinzani alisema. “Damu na sadaka za watu wengi wasio na hatia, pamoja na Padre Donald Martin Ye Naing Win, zitumike kama sadaka ya kukomesha vurugu zinazotokea nchini kote.” Mapema mwezi huu, jeshi la kijeshi la Myanmar lilishambulia kwa bomu Kanisa Katoliki la Moyo Mtakatifu wa Yesu huko Mindat, eneo lililo katika Jimbo la Chin kaskazini-magharibi mwa Birmania. Lilikuwa ni Kanisa lililochaguliwa kuwa Kanisa kuu la Jimbo Jipya lililoanzishwa la Mindat, ambalo Papa Francisko aliliunda tarehe 25 Januari 2025. Kanisa kuu jipya lilishambuliwa tarehe 6 Februari 2025, ambapo halikuweza kutumika baada ya mashambulizi ya angani kuharibu paa na madirisha ya vioo. Hakukuwa na majeruhi katika mlipuko huo kwa sababu mapadre na waamini walikuwa tayari wameondoka eneo hilo kutokana na hali mbaya ya usalama na mapigano yanayoendelea huko.

Wito wa dhati kukomesha vurugu

Katika salamu zake za rambirambi kufuatia na kifo cha Padre Donald, Kardinali Bo alisema, "Tulipokea habari kwamba Padre Donald Martin Ye Naing Win, padre wa Jimbo Kuu Katoliki la Mandalay, aliuawa kikatili na kundi la watu wenye silaha jioni ya Ijumaa, tarehe 14 Februari 2025. Tumeshtushwa na kusikitishwa sana na habari hizo.” Kanisa Katoliki nchini kote Myanmar, pamoja na Askofu Mkuu wa Mandalay Marco Tin Win, mapadre, watawa, waamini wa Jimbo kuu la Mandalay na wazazi na ndugu wa marehemu padre wa Birmania, mkuu wa Kanisa nchini Myanmar wamebainisha wanavyo omboleza kifo chake. “Mungu Baba, Bwana wa maisha yote, afariji mioyo yenu inayoomboleza na yetu,” Kardinali Bo aliomba. "Kwa kujifunza kutokana na matukio haya ya kuhuzunisha ambayo tumekumbana nayo, roho ya kidugu iamshwe, na tunaomba kwa bidii kukomeshwa kwa jeuri na kuzuia matukio kama hayo katika siku zijazo. Ukatili uliofanyiwa Padre Donald Martin Ye Naing Win, Kadinali Bo alisisitiza, si jambo linaloweza kusahaulika kwa urahisi. Kwa hiyo, tunawaomba waliohusika kuchukua hatua stahiki na kuhakikisha haki inatendeka, ili matukio ya aina hiyo yasijirudie siku zijazo. Roho ya Padre Donald Martin Ye Naing Ishinde kwa rehema za Mungu, ipumzike kwa amani ya milele!”

Lawama kali kwa kila shambulio

Mbali na salamu za rambirambi za Kardinali Bo, pia Balozi wa Vatican nchini Myanmar  alionesha huzuni kutokana na mauaji ya Padre huyo, kwa mujibu wa Habari za Kanisa barani Asia (LiCAS.news). Askofu Mkuu Andrea Ferrante, Balozi wa Vatican, aidha "alilaani  vikali kila shambulio dhidi ya maisha na hadhi ya mwanadamu na aina zote za jeuri kama njia ya kusuluhisha mizozo." Mwanadiplomasia huyo aliwataka mapadre, watawa na wamisionari katika Jimbo kuu, licha ya hatari zilizopo, kusimama kidete katika utume wao ambao ni mzizi katika upendo wake. Askofu Mkuu huyo alihimiza: "Kila mmoja awe ishara ya uwepo wa huruma wa Baba ambaye anawakaribisha watoto wake na kuponya majeraha yao."

 

18 Februari 2025, 13:41