Italia/Gaza:wamefikishwa Italia watoto14 wenye Saratani kutoka Gaza
Na Padre Ibrahim Faltas (OFM)
Si rahisi kukabiliana na uhamisho wa wagonjwa wanaohitaji huduma, inakuwa ngumu sana kuhamisha watoto wenye magonjwa ya saratani. Nilipata fursa ya kuwapo wakati wa kuwasili kwa ndege ya Jeshi la Wanahewa la Italia huko Ciampino na kuwakaribisha watoto na wasindikizaji wao pamoja na wahudumu wa Italia ambapo Mawaziri Antonio Tajani na Anna Maria Bernini, pamoja na Mkuu wa Chuo Kikuu cha La Sapienza, Roma Dr. Ramzi Khoury, rais wa Kamati Kuu ya Rais ya Masuala ya Kanisa huko Palestina. Hisia tofauti huingiliana: furaha na huzuni, shukrani na wasiwasi. Furaha hutokea katika mawazo ya kuweza kuwakaribisha, kuwatunza na kuwaokoa watoto, huzuni hutokea kwa sababu viumbe hawa, waliofanywa kuwa dhaifu na magonjwa mabaya, wameteseka kutokana na vita vinavyowazunguka ambavyo vimezuia utunzaji muhimu.
Shukrani kwa serikali na watu wa Italia
Shukrani ni kubwa kwa kujitolea kwa serikali na watu wa Italia: Nimeona na kugusa hisia na ukarimu wa kila mtu. Nina wasiwasi, sote tuna wasiwasi kuhusu siku zijazo za hivi karibuni. Uhamisho wa wagonjwa kutoka Gaza ulikuwa umezuiwa na miezi ya vita ambayo ilizuia kuingia kwa aina yoyote ya msaada na kuzuia kutoka kwa wale waliohitaji msaada. Sitaki kufikiria nini kinaweza kutokea ikiwa vita vingeanza tena njia yake ya kifo na uharibifu. Kilichoongezwa kwa hisia hizi ni uhakika kwamba kazi ya kibinafsi na ya kitaaluma ya waokoaji hutuzwa na tabasamu la shukrani la wale ambao wamekaribishwa. Kukaribisha watoto, haki zao, mahitaji yao ni hisia ya juu zaidi ya ustaarabu ambayo watu wanaweza kueleza. Msaada na matunzo ni maisha kwa watoto hawa ambao pia wana haki ya mpango wa maisha unaofikiriwa na kutamaniwa kwa ajili ya maisha yao ya baadaye.