MAP

Tuombee watu waengi wa Mungu wanaoteseka kwa kunyimwa haki zao za msingi za kujieleza katika Nchi nyingi. Tuombee watu waengi wa Mungu wanaoteseka kwa kunyimwa haki zao za msingi za kujieleza katika Nchi nyingi.  (Pixabay)

Nicaragua,mapadre wengine wawili walifukuzwa na kuletwa Roma

Balmaceda na Martínez,wote kutoka Jimbo la Estelí na lile la Matagalpa,walikuwa wamekamatwa katika siku za hivi karibuni.Kulingana na vyombo vya habari huru, watu 245 wa kidini wamefukuzwa na mamlaka ya Managua tangu 2018.

Vatican News

Leonel Balmaceda na Denis Martínez, mapadre wawili waliokamatwa Nicaragua tarehe 10 na 11 Agosti 2024, walifukuzwa na serikali na kupelekwa Roma. Paroko wa kwanza wa Kanisa la Jesús de Caridad huko La Trinidad, anatoka jimbo la Estelí, wa pili, mkufunzi katika seminari ya kati ya (Nuestra Señora de Fátima) Mama Yetu wa Fatima huko Managua, Mapadre wa  jimbo la Matagalpa, inayosimamiwa na Askofu Rolando Álvarez, walikaribishwa mjini Roma mnamo Januari iliyopita.

Padre mwingine ameondoka Nicaragua

Watetezi wa haki za binadamu na vyombo vya habari huru vilishutumu kufukuzwa kwao, kama vile tovuti za La Prensa na Noticias 100%, ambazo pia ziliripoti kwamba Danny García, paroko wa Kanisa la Mtakatifu Yohane Mbatizaji  huko Matagalpa, “aliachiliwa” baada ya habari za kukamatwa kwake na polisi wa Nicaragua tarehe 15 Agosti 2024, na tayari ameondoka kutoka Nicaragua.

Tangu 2018 watu wa dini 245 wamefukuzwa akiwemo Balozi wa Vatican

Kulingana na ripoti ya mtafiti wa Nicaragua aliye uhamishoni, na kuripotiwa na Tovuti ya Noticias 100%, tangu mlipuko wa mgogoro nchini humo mwaka wa 2018, wangeweza kulazimishwa uhamishoni au Watu wa Dini 245 walifukuzwa, akiwemo Balozi wa Vatican, Askofu Mkuu Waldemar Sommertag, na kisha maaskofu watatu, mapadre 136 kutoka majimbo mbalimbali ya Nicaragua, mashemasi watatu, waseminari kumi na moja na watawa 91 au watawa wa kiume. Pia kulingana na tovuti inayotaja hati hiyo, watu 19 wa kidini, akiwemo Askofu Álvarez, Askofu aliyehamishwa huko Silvio Báez, na mapadre wengine 14, walitangazwa kuwa “wasaliti wa nchi” na kupokonywa utaifa wao.

19 Agosti 2024, 18:03