MAP

2022.12.01 Nembo ya Ziara ya Papa nchini Sudan Kusini 3-5 Februari 2023. 2022.12.01 Nembo ya Ziara ya Papa nchini Sudan Kusini 3-5 Februari 2023. 

Sudan Kusini,ziara ya Papa ya kiekumene ili kufungua njia za amani

Padre Christopher Hartley,mmisionari Mhispania,ambaye yuko Nandi,katika Jimbo la Tombura-Yambio anaelezea historia ya dini ya Kikristo,kimila,elimu na miito katika fursa ya Ziara ya Papa nchini humo kuanzia tarehe 3-5 Februari 2023.Kauli mbiu:'Wote wawe na Umoja'(Yh 17).

Na Angella Rwezaula; - Vatican.

Sudan Kusini nchi ambayo inajiandaa kupokea ziara ya kiekumene ya Papa Francisko pamoja na Askofu Mkuu wa Canterbury Justin Welby, Mkuu wa  Usharika Kiangilikani  na mchungaji Iain Greenshields, Msimamizi wa Mkutano Mkuu wa Kanisa la Scotland kwa jumuiya mbalimbali za imani inawakilisha kwa hakika kipengele cha kuunganisha cha muundo na maisha ya kijamii, katika muktadha ulioharibiwa na kusambaratishwa na miongo kadhaa ya vita vya wenyewe kwa wenyewe. Mara nyingi uwepo huu umekuwa na jukumu katika kuunganisha umbali na tofauti za kikabila ambazo huchochea migogoro. Kwa sababu hiyo, kwa miaka mingi, viongozi wa jumuiya mbalimbali za kidini wamehusika katika majaribio ya kuanzisha majadiliano ya amani. 

Ishara ya kuunga mkono shuku ya amani na wema ulio ndani ya watu 

Kwa njia hiyo hilo ndilo eneo ambalo ziara ya  kiekumene iliyofikiriwa na Baba Mtakatifu Francisko, Askofu Mkuu Justin Welby na mchungaji Greenshields inakita mzizi na  kupandikizwa, kama ishara na fursa ya kuunga mkono shauku ya amani na wema unaokaa katika mioyo ya watu wengi ambao wamekuwa wakilipa gharama zaidi ya mizozo isiyo na maana kwenye ngozi zao wenyewe kwa miongo kadhaa. Inafurahisha kutilia maanani safari ya kihistoria ambayo sasa inaona Makanisa na jumuiya mbalimbali za kikanisa zikiweka kumbukumbu za mashindano ya maungamo ya kale na kufanya kazi bega kwa bega pia katika kujaribu kuzima migogoro na kuunga mkono ujenzi wa kuishi pamoja kwa amani kwa wananchi wenye mwelekeo wa manufaa ya wote.

Tangazo la Kikristo Sudan 

Hayo yamefafanuliwa na Padre Christopher Hartley, mmisionari Mhispania kutoka Jimbo la Toledo, ambaye sasa yuko Nandi, katika Jimbo la  Tombura-Yambio katika fursa hii ya Ziara ya Kitume  ya Papa Francisko katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC ) pamoja na Sudan Kusini ikiongozwa kwa ujumla na kauli mbiu:“ Mhujaji wa Kiekumene wa Amani nchini Sudan Kusini”, kuanzia tarehe 31 Januari hadi tarehe 5 Februaria ambapo atakuwa Sudan Kusini kuanzia tarehe 3-5 Februari. Kwa mujibu wa Padre Hartley akifafanua juu ya Uinjilishaji alibainisha kwamba tangazo la Kikristo tayari lilikuwa limewasili katika eneo la sasa la Sudan Kusini katika karne ya sita. Mipango ya kweli ya uinjilishaji katika Sudan nzima katika zama za kisasa ilianzia  tangu karne ya 19, katika kipindi cha Milki ya Uingereza, pamoja na wamisionari wa Comboni waliofika kutoka Verona  Italia na wamisionari wa Jumuiya ya Mill Hill. Katika maeneo mengi ambayo sasa yamejumuishwa katika Sudan Kusini, shughuli za kimisionari na uwepo zilichukua umuhimu na mwendelezo kuanzia miaka ya 70 ya karne ya ishirini. Hata kama bado kuna sehemu ya ulinganifu na vipengele kutoka katika katika  dini za jadi, imani kwa  sehemu kubwa ya Wakristo inastaajabisha na inasonga mbele.

Takribani watu milioni 6.2  kati ya Milioni 16,Sudan Kusini ni Wakatoliki

Takriban Watu wa Sudan Kusini milioni 6.2 (sawa na 37.2% ya watu wa kitaifa, wanaojumuisha zaidi ya watu milioni 16) ni Wakatoliki. Mtakatifu  Josephine Bakhita, mtawa wa kwanza wa Kiafrika wa Wakomboni aliyezaliwa karibu 1845 katika Milima ya Nuba, katika eneo ambalo sasa ni Sudan Kusini, na Mtakatifu Daniel Comboni ni wafia imani wakuu wanaoheshimiwa na Wasudan Kusini, hapo pia  katika Jimbo la  Tombura Yambio. Kazi ya wamisionari wa Comboni huko Sudani Kusini haikupotoka, licha ya kufukuzwa kwao mnamo tarehe 6 Machi 1964 na vita  mnamo mwaka 1983, alisisitiza  Padre Christopher.  Kwa maana hiyo mani ya Kikatoliki ilifika kwa mara ya kwanza pamoja na wamisionari wa Comboni huko Mupoi, karibu na Tombura, mnamo mwaka wa 1912.

Parokia, seminari na miito

Parokia ya Nandi ni ya tatu katika jimbo hilo na ilianzishwa mnamo mwaka 1947, tena na wamisionari wa Comboni. Lakini Ukristo ulifika katika maeneo mengi ya nchi miongo michache iliyopita. Kuna mahali ambapo bado wamisionari wanamtangaza Yesu Kristo kwa mara ya kwanza. Hakuna uhaba wa miito ya kipadre na kidini, kuna watahiniwa wengi katika seminari za nchi, hata kama wakati fulani malezi ni muhimu sana na makali. Kuna seminari kuu moja tu katika Jimbo kuu la Juba, na sehemu kubwa ya majimbo yana  taasisi ndogo za malezi. Kutokana na hilo wengi wa wanafunzi wa Sudan Kusini wanakwenda  kusoma taalimungu kati ya Juba, Nairobi na Kinshasa. Elimu yenyewe ndiyo kitovu cha wasiwasi na mipango ya Kanisa Katoliki  mahali hapo. Wengi wa watoto wadogo nchini Sudan Kusini wanakua na wamesoma katika taasisi za elimuKikatoliki.

Shule za kikatoliki na umma

Padre Christopher aidha alieleza kuwa huko Tombura, kwa mfano, kuna shule nyingi za Kikatoliki kuliko za umma. Wamisionari wa kwanza wa Comboni waliwasili Sudan mnamo mwaka wa 1842. Walijenga shule na hospitali ili kuwahudumia wakazi wa eneo hilo, wakiwa bado wamefungamana na imani na desturi za kidini. Shukrani kwa wamisionari, wengi wa wenyeji waliacha dini yao ya jadi na kuwa Wakatoliki. Mnamo mwaka wa 2005, Mkataba wa Amani wa Kikamilifu (CPA) kati ya mikoa ya kusini na serikali ya Khartoum ulifungua njia ya uhuru wa Sudan Kusini, ambao ulitiwa saini baadaye mwaka 2011. Tangu nchi hiyo imejitenga na Sudan, Wakatoliki wengi walikuwa wamejilimbikizia huko Juba na maeneo ya jirani ambao walichagua kubaki Sudan Kusini.

Waanglikani na waliopyaishwa

Makanisa mengine yasiyo ya Kikatoliki na jumuiya za kikanisa ziliwasili katika maeneo ya Sudan kuanzia mwaka wa 1899. Waanglikani, kupitia Shirika la Wamisionari wa Kanisa, tayari katika miaka ya kwanza ya uwepo wao katika eneo hilo, kutokana na mahubiri yao na kujitolea kwao kimisionari, walibatiza makumi ya maelfu ya wakazi. Hivyo sasa, Kanisa la Maaskofu la Sudan, ambalo ni sehemu ya Usharika wa Kianglikani, kwa idadi ni Kanisa la pili kwa ukubwa katika Sudan na Sudan Kusini, baada ya Kanisa Katoliki. Kanisa la Umoja wa Kipresbiteriani, ambalo ni sehemu ya Usharika wa Ulimwengu wa Makanisa ya Yaliyopyaishwa, lilianza kazi yake nchini Sudan mnamo mwaka wa 1900. Baadaye  katika karne ya 20, wamisionari wa jumuiya nyingine nyingi za kikanisa wenye chapa ya Marekebisho na Kiinjili, kama vile Kanisa la Sudan ya Kristo, walifikia nchi hiyo  wakikazia shughuli zao kusini. Miongoni mwa jumuiya nyingine za kidini zilizopo Sudan Kusini,  pia Waislamu ni wachache. Wengi wao waliishi nchini humo kabla ya kupata uhuru kutoka Sudan mnamo mwaka 2011. Na wakati huo huo dini ya   kimila huko nchini Sudan Kusini  yenye msingi wa imani ya miungu ambayo inatofautiana kulingana na makabila na jamii mbalimbali, inaendelea kufuatwa na sehemu kubwa ya wakazi hao.

Njaa, uhaba wa chakula na ukosefu wa utulivu wa kisiasa

Hata kama kuna takwimu ambayo inaonekana kuashiria mchakato wa kurejesha na kukomaa kwa nchi hiyo changa  Padre Christopher alieleza kuwa hali halisi kwa  ujumla inabaki kuwa ya kutisha. Zaidi ya nusu ya watu wako katika hatari ya njaa na wanaishi katika uhaba wa chakula. Takriban watoto milioni mbili wanakabiliwa na utapiamlo kutokana na  kukosekana kwa utulivu wa kisiasa, kiuchumi na kijamii ambayo Sudan Kusini inakabili kunatokana zaidi na mzozo wa muda mrefu kati ya Rais Salva Kiir, wa kabila kubwa zaidi la Dinka, na naibu wake Riek Machar, wa kabila la Nuer.

Viongozi wawili wa Sudan Kusini mjini Vatican 2019

Ikumbukwe kwamba ilikuwa mnamo 2019 ambapo maadui hao wawili wa kibinadamu walikuja pamoja jijini Vatican  na ambao Papa Francisko alibusu hata miguu yao, huku akiwaomba amani. Ingawa nchini Sudan Kusini asilimia 4-5 tu ya wakazi wana umeme na upatikanaji wa maji karibu haupo, wakati nchi hiyo ina utajiri mkubwa wa maliasili, ikiwa ni pamoja na dhahabu, almasi, mafuta. Hizo ni rasilimali ambazo haziwezi kupatikana kwa raia kwa sababu ya hali ya ukosefu wa usalama na ukosefu wa utulivu wa kisiasa na kijamii. Hata kabla ya kuzaliwa kwa Sudan Kusini kama taifa huru, kurudi nyuma katika maisha ya Sudan nzima kulikuja na mzozo wa Darfur, eneo lililoko magharibi mwa nchi hiyo. Mzozo huo uliozuka rasmi mnamo mwaka 2003 na kutangazwa kuhitimishwa mwaka 2009, na kusababisha vifo vya watu 400,000 na takriban watu milioni mbili waliokimbia makazi yao. Licha ya makubaliano ya amani yaliyotiwa saini nchini Ethiopia mwaka wa 2018 lakini  hayajawahi kuheshimiwa, hadi sasa mivutano mikali ya kikabila inaendelea.

Mapigano ya waasi yameanza tena tangu Agosti 2022

Nchini Sudan Kusini, mapigano kati ya wanamgambowaasi yameanza tena tangu Agosti 2022. Uchaguzi umepangwa kufanyika mwishoni mwa 2024 nchini humo, ambao umeahirishwa mara kadhaa. Sudan Kusini iliyozaliwa mwaka wa 2011 kati ya vita viwili vikali vya wenyewe kwa wenyewe, ilipata uhuru wake baada ya takriban miaka 30 ya vita, mji mkuu wa  Juba ambako kwa sasa kuna angalau makabila 50. Wanawake wana wastani wa watoto 5/6 na umri wa kuishi haufikii miaka 60.

27 Januari 2023, 13:18