杏MAP导航

Tafuta

Watoto wadogo Watoto wadogo 

Who/Unicef:Juma la kunyonyesha Kimataifa:kuwekeza katika mifumo ya afya na kusaidia wanyonyeshaji!

Kunyonyesha ni uwekezaji katika siku zijazo,lakini ni asilimia 48 tu ya watoto wa kike na kiume walio chini ya miezi sita ndio wanaonyonyeshwa maziwa ya mama yao,chini ya kiwango cha asilimia 60 cha lengo lililowekwa na Shirika la Afya Ulimwenguni kwa mwaka wa 2030.Haya yamethibitishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya duniani(WHO)na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Watoto UNICEF katika fursa ya Juma la Kimataifa la kunyonyesha kuanzia tarehe 1-7 Agosti 2025.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika Juma la kimataifa la kunyonyesha kuanzia tarehe 1-7 Agosti 2025, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya duniani(WHO) Tedros Adhanom Ghebreyesus na Bi Catherine Russell, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Watoto UNICEF. Kunyonyesha ni mojawapo ya njia bora zaidi za kuhakikisha afya, maendeleo, na maisha ya watoto wachanga katika hatua za mwanzo za maisha. Inafanya kama chanjo ya kwanza, kutoa ulinzi dhidi ya magonjwa kama vile kuhara na mneumonia. Kunyonyesha ni uwekezaji katika siku zijazo, lakini ni asilimia 48 tu ya watoto wa kike na kiume walio chini ya miezi sita ndio wanaonyonyeshwa maziwa ya mama yao, chini ya kiwango cha asilimia 60 cha lengo lililowekwa na Shirika la Afya Ulimwenguni(WHO) kwa mwaka wa 2030. Hii ni kutokana na mwingiliano wa changamoto kwa akina mama wapya, wafanyakazi, na mifumo ya afya. Mamilioni ya familia ulimwenguni pote hazipokei usaidizi ufaao kwa wakati unaofaa, wakati ambapo wanauhitaji zaidi.

Nchi zinazotoa mafunzo ya kulisha watoto ni chache

Ni moja tu ya tano tu ya nchi zinazotoa mafunzo ya kulisha watoto wachanga kwa walezi wa mama wachanga. Hii ina maana kwamba akina mama wengi duniani kote huondoka hospitalini bila taarifa za kutosha kuhusu kunyonyesha na wakati wa kuanzisha ulishaji wa ziada. Katika nchi nyingi, mifumo ya afya mara nyingi haifadhiliwi sana, imegawanyika, au haina vifaa duni ili kutoa usaidizi thabiti, unaotegemea ushahidi na ubora wa kunyonyesha. Uwekezaji katika usaidizi wa kunyonyesha bado uko chini sana, licha ya kila dola iliyowekezwa kuleta faida ya kiuchumi ya Dola 35.

Katika hafla ya  Juma la Unyonyeshaji Duniani (WBC), inayoongozwa na kauli mbiu: "Kuweka Kipaumbele Unyonyeshaji wa Maziwa ya Mama: Kujenga Mitandao Endelevu ya Usaidizi," Shirika la Afya Dunia (WHO) na Shirika la Umoja wa Matiafa la Watoto(UNICEF) zinatoa wito kwa serikali, mamlaka za afya na washirika kuwekeza katika usaidizi bora wa kunyonyesha kwa: kuhakikisha uwekezaji wa kutosha katika matunzo ya usawa, bora ya uzazi na watoto wachanga, ikiwa ni pamoja na huduma za usaidizi wa kunyonyesha. Kuongeza mgao wa bajeti ya kitaifa kwa programu za unyonyeshaji. Kujumuisha ushauri nasaha wa unyonyeshaji na usaidizi katika huduma za msingi za afya ya mama na mtoto, ikijumuisha utunzaji katika ujauzito, ndani ya uzazi na baada ya kuzaa. Kuhakikisha kwamba wafanyakazi wote wa afya wamewezeshwa ujuzi na ujuzi unaohitajika ili kusaidia kunyonyesha, ikiwa ni pamoja na katika hali za dharura.

Nchini Italia siku ya kunyonyesha huadhimishwa kuanzia Oktoba 1- 7

Nchini Italia, ambapo Siku ya Kunyonyesha kwa Mtoto(SAM)huadhimishwa kuanzia Oktoba 1 hadi 7 na kuratibiwa na MAMI, UNICEF inaendelea na mpango wake wa "Pamoja kwa Kunyonyesha: Mbinu Bora, Kwa kuzingatia Ushahidi. Lengo letu katika UNICEF Italia ni kulinda, kukuza, na kusaidia unyonyeshaji huku tukitoa na kuhakikisha huduma na usaidizi wa kutosha kwa akina mama wasionyonya. Hadi sasa, nchini Italia, Mipango ya Kusaidia Mtoto ni pamoja na hospitali 36 na vituo 12 vya jamii vinavyotambuliwa kuwa vya Kufaa kwa Mtoto, programu nne za shahada ya Unyonyeshaji-Rafiki wa Kunyonyesha, na vifaa vingine vingi vinaendelea," alisema hayo Nicola Graziano, Rais wa UNICEF Italia. "Miongoni mwa shughuli zilizofanywa mwaka huu, ningependa kuangazia Mkataba wa Maelewano tuliotia saini na Idara ya Shirika la Mahakama, Utumishi, na Huduma ya Wizara ya Sheria ili kutekeleza shughuli za habari na mafunzo juu ya uzazi wa usikivu na siku elfu za kwanza za maisha ya mtoto, pamoja na utekelezaji wa "UNICEF Baby Shit Stops" katika ofisi za mahakama na kutoa msaada wa watoto katika nchi nzima.

Juma la Kunyonyesha duniani 1-7 Agosti 2025
05 Agosti 2025, 11:36