杏MAP导航

Tafuta

Spika wa zamani wa Bunge la Tanzania aliaga dunia. Spika wa zamani wa Bunge la Tanzania aliaga dunia. 

Tanzania:Spika wa zamani nchini Tanzania azikwa kwake Kongwa,Dodoma

Spika wa zamani wa Bunge la Tanzania,Bwana Ndugai,alizikwa kwake Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma,Agosti 11.Viongozi mbalimali wa chama na serikali,wananchi wa Kongwa na waombolezaji wengine walihudhuria maziko hayo.Marehemu Ndugai alifariki dunia tarehe 6 Agosti 2025,wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali moja jijini Dodoma baada ya kuugua ghafla kwa mujibu wa taarifa za ndani ya Nchi.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Askofu Mkuu wa Kanisa la Kianglikani nchini Tanzania, Daktari Mahimbo Mndolwa aliongoza Misa ya Mazishi kwenye Kanisa la Mtakatifu Michael wilayani Kongwa, tarehe 11 Agosti 2025 kwa ajili ya aliyekuwa Spika wa zamani wa Bunge la Tanzania, Bwana Job Yustino Ndugai na baadaye mwili wake ulihitadhiwa katika nyumba yake ya milele huko Shambani kwake katika kijiji cha Mandumbwa wilayani Kongwa mkoani Dodoma, na ndiyo ilikuwa mwisho wa safari ya maisha yake hapa Duniani.  Akizungumza katika ibaada ya mazishi ya marehemu Ndugai, Askofu Mndolwa alisema kuwa: “kuna baadhi ya watu waliopewa kipawa cha uongozi katika nafasi mbalimbali lakini wamekuwa wakitumia nafasi zao vibaya kwa kuwaumiza wengine na aliwataka watu wafuate mema aliyoyatenda spika wa zamani wa Bunge la Tanzania marehemu Job Yustino Ndugai.”

Askofu huyo pamoja na mengine mengi aliyosema alitafakari: “Unakifanyia nini kipawa alichokupa mungu. Wapo waliopewa kipawa cha fedha nyingi, badala ya kujenga Ufalme wa Mungu na nchi, wanakitumia kuumiza wengine. Wapo wengine waliopewa vipawa vya uongozi badala ya kuvitumia vizuri kuzalisha wengine, wanawafisha wengine. Tunapoelekea kuuzika mwili wa mtumishi huyu, Mungu akusaidie kupeleleza Mungu amekupa nini. Kama umepewa madaraka yatumie vizuri na usiyatumie vibaya.”

Waziri Mkuu Majaliwa:kuenzi yote yaliyoasisiwa na marehemu Ndugai

Na kwa upande wake Waziri Mkuu wa Tanzania,  Bwana Kassim Majaliwa pamoja na mengi aliyosema alitaja kuwa, marehemu Ndugai alikuwa mwana mageuzi na mmoja wa wanasiasa mashuhuri aliyebeba taswira ya wana Kongwa, Mkoa wa Dodoma na Kitaifa na Kimataifa na kwamba Serikali itayaenzi yale yote yaliyoasisiwa na marehemu Ndugai. “Ndugu waombolezaji ni kwamba tunakumbuka jana mheshimiwa Rais wakati wa kuaga mwili wa mpendwa wetu pale Dodoma, pamoja na kutambua kazi kubwa na alama alizoacha marehemu ndani ya Kongwa kitaifa na kimataifa, aliagiza kukamilishwa masuala yote yaliyoanzishwa na marehemu, ikiwemo agizo kwa mamlaka husika kuendeleza kuitangaza Kongwa kama kielelezo cha makumbusho ya kupigania uhuru wa nchi za kusini mwa Afrika. Napenda kuwahakikishia wananchi wa Kongwa kuwa tutalisimamia agizo hili," alieleza.

Hafla ya Kitaifa ya kuaga mwili wa Spika Mstaafu Ndugai: Dk. Ackson

Wakati wa uhai wake alikuwa Mbunge wa Jimbo  la Kongwa na kuhudumu kama Spika wa Bunge la Tanzania tangu mwaka 2015 hadi alipojiuzulu nafasi hiyo mnamo mwaka 2022.  Kwa sasa Spika wa Bunge la Tanzania, ni Dk. Tulia Ackson, ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Wabunge duniani (IPU) na ambaye alitoa taarifa za kifo cha Bwana Ndugai. Akitoa neno  Spika Dk Tulia Ackson alisema: “Nikatika kipindi chake ambapo ugonjwa wa UVIKO-19 ulianza na nchi nyingi zilingia kwenye hali ya kufungiwa yaani, hata hivyo yeye alikuja na ubunifu wa kuendesha shughuli za bunge kwa njia ya mtandao. Ubunifu huo umetufanya mpaka leo, bunge limeendelea kuwa la mtandao hatutumii tena karatasi kama ilivyokuwa huko nyuma.” Kiongozi huyo kadhalika aliongeza kusema Ndugai, alileta wazo na pia alisimamia kwa ukamilifu kabisa la ujenzi wa shule ya sekondari ya wasichana iliyopewa heshima ya jina la bunge, iliyopo katika eneo la Kikombo, jijini Dodoma.

Ackson aliendelea lisema: “Naamini wote mmesikia habari njema za shule hii, kwamba watoto wetu wa kike wanafanya vizuri na kwa sababu hiyo kuendeleza yale aliyoyaanzisha na sasa umeanza utaratibu tunajenga shule nyingine ya bunge. Lakini hii sasa itakuwa ya wavulana na bahati nzuri inajengwa katika kipindi ambacho yeye amemaliza ya watoto wa kike, alikuwa ni mwanaume mimi Spika mwanamke naanza kujenga shule ya watoto wa kiume. Kwa kuazia zaidi alisema “katika kipindi cha uongozi wa Ndugai, akiwa Spika wa Bunge pamoja na sheria mbalimbali alizisimamia kutungwa ambazo asingeweza kuzitaja zote, mojajawapo ni uanzishwaji wa makao makuu ya nchi, kuwa Dodoma ya mwaka 2018. Sheria hii ndiyo iliyofanya mambo yote tunayayaona hapa Dodoma yaendelea kufanyika, kwa ukamilifu kabisa na kwa sehemu amesema mkuu wetu wa mkoa wa Dodoma," alisema.

Rais wa Tanzania: "Ndugai alikuwa kiongozi mkomavu kisiasa na kiungozi"

Kwa upande wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, aliongoza hafla ya kitaifa ya kuaga mwili wa Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri hiyo, Job Yustino Ndugai, katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma tarehe 10 Agosti  2025. Bwana Ndugai ambaye siku chache zilizopita aliongoza katika kura za maoni za kutetea kiti cha Ubunge wa Jimbo la Kongwa mkoani Dodoma kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), alifariki baada ya kuugua kwa muda mfupi  kwa shinikizo la chini la damu lililosababishwa na maambukizi makali kwenye mfumo wa hewa kwa mujibu wa maelezo.

Kwa njia hiyo akihutubia umati mkubwa wa waombolezaji katika tukio hilo, Rais Samia alisema, Ndugai alikuwa kiongozi mkomavu kisiasa na kiuongozi, ambaye aliweka thamani kubwa katika demokrasia ya Bunge. “Ndugai alikuwa mkomavu kisiasa na kiuongozi, na aliyeamini katika demokrasia ya Bunge. Alipokuwa Spika, Bunge lilishuhudia mafanikio mbalimbali yaliyoelezwa hapa na Katibu wa Bunge,” amesema Rais Samia. Wakati huo huo, kiongozi huyo wa nchi aliagiza mamlaka husika serikalini kujenga makumbusho yatakayoeleza mchango wa wilaya ya Kongwa katika ukombozi wa nchi za Kusini mwa Afrika ili kuenzi ndoto ya Ndugai. Hafla hiyo ya kuaga mwili wa Ndugai ilihudhuriwa na viongozi wa kitaifa, wabunge, ndugu, jamaa na wananchi waliojitokeza kumuenzi marehemu huyo. Baadaye mwili wa Spika Mstaafu ulisafirishwa kwenda Kongwa mahali alipozikwa tarehe 11 Agosti 2025.

Maziko ya Spika wa zamani Ndugai nchini Tanzania

 

11 Agosti 2025, 17:31