杏MAP导航

Tafuta

Mwaka 2024 ulikuwa mbaya zaidi katika rekodi ya wafanyakazi wa misaada,na watu 383 waliuawa,ikiwa ni pamoja na takriban 172 kufikia wakati huu mwaka 2024. Mwaka 2024 ulikuwa mbaya zaidi katika rekodi ya wafanyakazi wa misaada,na watu 383 waliuawa,ikiwa ni pamoja na takriban 172 kufikia wakati huu mwaka 2024. 

Mwaka 2025 ni mbaya zaidi kuliko awali kwa kuuawa kwa wahudumu wa kibinadamu

Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita,mashambulizi mengi yametokea katika eneo la Palestina linalokaliwa kwa mabavu,Sudan Kusini na Sudan,na kufanya maeneo haya kuwa hatari zaidi kwa wafanyakazi wa kutoa misaada ya kibinadamu.Haya yametolewa na Shirika la Save the Children katika Muktadha wa Siku ya Kimataifa ya Msaada wa kinadamu,tarehe 19 Agosti 2025.Tangu 200 hadi sasa mfanyakaza mmoja anauawa,anajeruhiwa,kutekwa nyara wa kukamatwa.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Tangu 2000, kwa wastani, mfanyakazi wa kutoa misaada ameuawa, kujeruhiwa, kutekwa nyara, au kukamatwa kila siku, na 2025 uko mbioni kuwa mwaka mbaya zaidi kuwahi kutokea kwa wafanyakazi wa misaada, Shirika la Kimataifa la Saidia watoto ( Save the Children) lilisema katika fursa ya Siku ya Kibinadamu Ulimwenguni, ifanyika kila ifikapo tarehe 19 ya kila mwaka. Kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni kutoka Hifadhidata ya Usalama ya Wafanyakazi wa Misaada (AWSD), zaidi ya mashambulizi 8,500 makubwa dhidi ya wafanyakazi wa misaada yamerekodiwa tangu mwaka 2000. Takwimu zinaonyesha kuwa kuwa mfanyakazi wa misaada kunazidi kuwa hatari, huku hatari zikiongezeka mwaka baada ya mwaka, licha ya sheria za kimataifa kupiga marufuku mashambulizi dhidi yao.

Hongezeko la vifo

Mwaka 2024 ulikuwa mbaya zaidi katika rekodi ya wafanyakazi wa misaada, na watu 383 waliuawa, ikiwa ni pamoja na takriban 172 kufikia wakati huu mwaka jana. Hii ilisababisha Australia, pamoja na nchi nyingine kadhaa, kuandaa Azimio la Ulinzi wa Wafanyakazi wa Misaada, ikisisitiza dhamira ya jumuiya ya kimataifa ya kubadili mwelekeo huo. Hata hivyo, mwaka 2025 unaelekea kuwa mwaka mbaya zaidi katika rekodi, huku wafanyakazi wa misaada 265 waliuawa hadi sasa mwaka huu, ongezeko la 54% ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana, kulingana na hesabu ya muda ya AWSD. Ongezeko la vifo katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita kimsingi ni kutokana na vita vya Gaza, ambapo vikosi vya Israel vimewaua wafanyakazi wa misaada 173 hadi sasa mwaka huu, na kuzidi idadi ya waliouawa duniani kote mwaka 2022.

Hali ngumu huko Sudan Kusini na Sudan

Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, mashambulizi mengi yametokea katika eneo la Palestina linalokaliwa kwa mabavu, Sudan Kusini na Sudan, na kufanya maeneo haya kuwa hatari zaidi kwa wafanyakazi wa misaada. Kila siku, wafanyakazi wa kibinadamu huhatarisha maisha yao ili kuokoa wengine. Na kila siku, kwa zaidi ya miaka 25, kwa wastani, angalau mfanyakazi mmoja wa kibinadamu huuawa, kujeruhiwa, kutekwa nyara, au kuzuiliwa wakati wa kufanya kazi zao. Hii inawakilisha zaidi ya mashambulizi 8,500 makubwa. Ahadi ya ulinzi kwa wafanyikazi wa kibinadamu chini ya sheria ya kimataifa ya kibinadamu imevunjwa. Kazi yetu inafadhiliwa kidogo, inadhoofishwa, na inashambuliwa. Hatuwezi kukubali ulimwengu ambamo wale wanaookoa uhai wanalengwa kufanya hivyo.

Mwaka mmoja uliopita, ulimwengu ulisimama pamoja nasi, ukitoa wito wa kukomeshwa kwa mauaji ya wafanyakazi wa kibinadamu. Viongozi wa dunia walisikiliza na kutia sahihi Azimio hilo, kisha wakatazama pembeni huku idadi ya vifo ikiendelea kuongezeka. Sheria ziko wazi. Mashambulizi dhidi ya wafanyAkazi wa kibinadamu ni uhalifu wa kivita, na uhalifu wa kivita haupaswi kuadhibiwa. "Hakuna maana katika matamko zaidi kama hayatatekelezwa au kutiwa saini na nchi zote. Tunahitaji hatua madhubuti na uwajibikaji kuchunguza, kushtaki na kumaliza mzunguko wa kutokujali," alisema Inger Ashing, Mkurugenzi Mtendaji wa Save the Children Kimataifa.

Wito kwa serikali zote kuwa na uwajibikaji 

Kwa njia hiyo   Shirika la Save the Children linatoa wito kwa serikali zote kudai uwajibikaji kwa kila ukiukaji wa sheria ya kimataifa ya kibinadamu dhidi ya wafanyakazi wa kibinadamu na kuhakikisha waliohusika wanachukuliwa hatua. Shirika la Save the Children pia linatoa wito kwa serikali zote kuidhinisha Azimio la Ulinzi wa Wafanyakazi wa kutoa Misaada ya Kibinadamu, lililohamaishwa na Australia wakati wa Juma la Ngazi ya Juu ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwa mwezi Septemba ujao , ili kuonesha dhamira ya kimataifa ya kulinda wafanyakazi wa kutoa misaada ya kibinadamu na kuzingatia sheria za vita.

Shirika la Saidia Watoto
19 Agosti 2025, 16:09