Colombia:Seneta Uribe afariki baada ya kushambuliwa kwa risasi mwezi Juni
Vatican News
Seneta Uribe Turbay, mwenye umri wa miaka 39, alikuwa mwathirika wa shambulio la tarehe 7 Juni 2025 huko Bogotá wakati wa mkutano wa uchaguzi, 2026 na ambaye alikuwa akiuguza majeraha ya risasi kichwani na mguuni. Baada ya shambulio hilo, alifanyiwa upasuaji wa dharura na kubaki hospitalini katika uangalizi maalum hadi kifo chake. Kijana mmoja alikamatwa katika eneo la shambulio hilo, na tangu wakati huo viongozi wamewashikilia wengine kadhaa. Tukio hilo limeibua wasiwasi mpya kuhusu ghasia za kisiasa nchini Colombia.
Wanasiasa wa Colombia watoa rambirambi zao
Marais wa zamani Alvaro Uribe na Iván Duque waliandika baadhi ya jumbe za kwanza zilizochapishwa kwa kumbukumbu ya Miguel Uribe Turbay. "Ugaidi umetunyang'anya ahadi ya Colombia na kiongozi wa uadilifu na uwazi," aliandika Duque (rais tangu 2018 hadi 2022), akiongeza kuwa sifa bora zaidi ambayo Wakolombia wanaweza kutoa "ni kuheshimu urithi wake, kwa umoja wa kusudi na uzalendo kamili." "Uovu huharibu kila kitu; wameua matumaini. Mapambano ya Miguel yawe mwanga unaoangazia njia sahihi ya Colombia," aliandika Alvaro Uribe (2002-2012).
Uchungu wa muda mrefu
Miguel Uribe Turbay alizaliwa huko Bogota mwaka 1986, na alifariki katika Hospitali ya Mtakatifu Fe huko Bogotá, ambako alikuwa akitibiwa. Aliyetekeleza shambulizi hilo, ni mvulana wa chini ya miaka 15, na ambaye alinaswa kufuatia makabiliano ya moto na mlinzi wa seneti huyo. Katia Hospitali ya Uribe Turbay alifanyiwa upasuaji wa mishipa ya fahamu na mishipa na upasuaji kwenye paja lake la kushoto, lakini ripoti za kimatibabu mara kwa mara zilielezea hali yake kuwa "mbaya." Katika taarifa iliyotolewa tarehe 9 Agosti 2025, na madaktari ilibainisha kuwa Uribe alikuwa amevuja damu katika mfumo mkuu wa neva, na kuhitaji upasuaji zaidi wa dharura.
Uchunguzi bado unaendelea
Kulingana na wachunguzi, takriban watu kumi kwa ujumla walihusika katika shambulio hilo, lakini watu saba wamekamatwa hadi sasa, ambapo watatu kati yao wakiwa watoto wadogo. Kuhusu wachochezi, njia kadhaa za uchunguzi zimependekezwa, lakini hakuna hata moja ambayo imesababisha mashtaka rasmi. Miguel Uribe Turbay alikuwa mtoto wa Diana Turbay, mwandishi wa habari mashuhuri, aliyetekwa nyara mwaka 1991 na wahuzaji wa dawa za kulevya Pablo Emilio Escobar Gaviria na kuuawa wakati wa shughuli za ukombozi.