杏MAP导航

Tafuta

Taarifa inaonesha kwamba, kuna Watanzania 168 waliopo nchini Iran, wakiwemo wanafunzi 134 katika mji wa Qom na wengine 34 jijini Tehran. Taarifa inaonesha kwamba, kuna Watanzania 168 waliopo nchini Iran, wakiwemo wanafunzi 134 katika mji wa Qom na wengine 34 jijini Tehran.   (AFP or licensors)

Vita kati ya Israeli na Iran: Watanzania Kurejeshwa Nchini Tanzania

Taarifa zilizopo hadi sasa zinaonesha kuwa kuna Watanzania 168 waliopo nchini Iran, wakiwemo wanafunzi 134 katika mji wa Qom na wengine 34 jijini Tehran. Kwa upande wa Israeli, inakadiriwa kuwa kuna zaidi ya Watanzania 200 wakiwemo watumishi wa Ubalozi wa Tanzania, wanafunzi, na wafanyakazi katika taasisi mbalimbali. Kati yao, Watanzania 50 tayari wamejiandikisha kwa ajili ya kupatiwa msaada wa kurejea nyumbani Tanzania.

Sarah Pelaji, - Vatican

Serikali ya Tanzania kupitia Balozi zake zilizopo katika nchi za Misri, Umoja wa Falme za Kiarabu (ambao unaiwakilisha Tanzania nchini Iran), Kuwait na Israeli imechukua hatua za haraka kuhakikisha raia wake wanarejeshwa Tanzania wakiwa salama. Hii ni kutokana na mapigano yanayoendelea kati ya nchi hizo mbili za Israeli na Iran. Taarifa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imeeleza kuwa, tayari Serikali ya Tanzania inafanya juhudi za kuwaorodhesha Watanzania waliopo katika nchi hizo ili, kuchukua hatua za haraka za kuwarejesha raia wake Tanzania wakiwa salama.

Serikali ya Tanzania kuwarejesha raia wake kutokana na vita
Serikali ya Tanzania kuwarejesha raia wake kutokana na vita   (AFP or licensors)

Hata hivyo Serikali ya Tanzania imewaondolea wananchi wake wasiwasi kuwa Watanzania waliopo nchini Israeli na Iran wapo salama, kufuatia mataifa hayo kushambuliana kwa makombora kwa muda wa wiki moja sasa. Taarifa zilizopo hadi sasa zinaonesha kuwa kuna Watanzania 168 waliopo nchini Iran, wakiwemo wanafunzi 134 katika mji wa Qom na wengine 34 jijini Tehran. Kwa upande wa Israeli, inakadiriwa kuwa kuna zaidi ya Watanzania 200 wakiwemo watumishi wa Ubalozi wa Tanzania, wanafunzi, na wafanyakazi katika taasisi mbalimbali. Kati yao, Watanzania 50 tayari wamejiandikisha kwa ajili ya kupatiwa msaada wa kurejea nyumbani. Pamoja na changamoto za kiusalama zilizopo, Serikali inathibitisha kuwa jengo la Ubalozi wa Tanzania nchini Israeli halijaathirika na mashambulizi ya hivi karibuni ya Iran. Wakati mashambulizi hayo yalipotokea, hapakuwa na mtu yeyote ndani ya jengo hilo, na maafisa wa ubalozi pamoja na familia zao wote wapo salama, ilisema taarifa hiyo.

20 Juni 2025, 14:02