杏MAP导航

Tafuta

Siku ya Wanawake duniani tarehe 8 Machi Siku ya Wanawake duniani tarehe 8 Machi  (ANSA)

Siku ya Wanawake:Kwa Wanawake na Wasichana wote:Haki,Usawa na Uwezeshaji

Katika kuelekea kilele cha siku hiyo,Mkurugenzi Mtendaji masuala ya wanawake UN Women,Bi Bahous alisema:Haki za wanawake na wasichana zinashambuliwa,fursa za wanawake kupaza sauti zinazidi kupungua na endapo tutaendelea na kasi hii msichana aliyezaliwa leo atakuwa na umri wa miaka 39 kabla wanawake hawajawa na viti vingi bungeni kama wanaume,atakuwa na umri wa miaka 68 kabla ndoa za utotoni hazijakomeshwa,na atakuwa na umri wa miaka 137 kabla umasikini uliokithiri kuisha.

Na Angella Rwezaula- Vatican.

Tarehe 8 Machi 2025 inaadhimishwa Siku ya Kimataifa ya Wanawake, kwa kuongozwa na kauli mbiu: Kwa Wanawake na Wasichana wote:Haki,Usawa na Uwezeshaji.”Jambo msingi katika maono haya ni kuwezesha kizazi kijacho cha vijana,hasa wanawake wa rika zote kuanzia na  balubalu kuwa kama vichocheo vya mabadiliko ya kudumu. Siku ya Wanawake duniani ilianzishwa rasimi na Umoja wa Mataifa kunako mwaka 1977, ili kuadhimishwa kila ifikapo tarehe 8  Machi ya kila mwaka, siku ambayo inaakisi umuhimu wa kupambania haki za wanawake na ukombozi wa wanawake. Kaulimbiu ya mwaka huu kwa njia hiyo  inataka hatua zichukuliwe ambazo zinaweza kufungua haki sawa, uwezo na fursa kwa wote na mustakabali wa wanawake ambapo hakuna anayeachwa nyuma. Jambo la msingi katika maono haya ni kuwezesha kizazi kijacho—vijana, hasa wanawake wachanga na wasichana balubalu kuwa kama vichocheo vya mabadiliko ya kudumu.

Miaka 30 ya azimio la Wanawake huko Beijing

 Kando na hayo mwaka huu 2025, Jumuiya ya Kimataifa itaadhimisha kumbukumbu ya miaka thelathini ya Mkutano wa Nne wa Dunia wa Wanawake na kupitishwa kwa Azimio la Beijing na Jukwaa la Utekelezaji (1995).   Waraka huu ndio mwongozo unaoendelea zaidi na ulioidhinishwa kwa upana zaidi wa haki za wanawake na wasichana duniani kote ambao ulibadilisha ajenda ya haki za wanawake katika suala la ulinzi wa kisheria, upatikanaji wa huduma, ushirikishwaji wa vijana, na mabadiliko ya kanuni za kijamii, fikra potofu na mawazo yaliyokwama hapo awali. Kwa kushirikisha vyombo vya habari, viongozi wa mashirika, serikali, viongozi wa jumuiya, jumuiya za kiraia na vijana, na wengine wenye ushawishi kuchukua hatua katika jumuiya zote. Lazima kuomba viongozi kuchukua hatua na kuwekeza katika kukuza haki za wanawake na usawa wa kijinsia. Lazima kushirikisha historia na jumbe za Siku ya Kimataifa ya Wanawake kwenye mifumo ya kidijitali, kwa kutumia alama ya reli: #ForAllWomenAndGirls ili kuibua mazungumzo na kuhamasisha hatua. Ni katika muktadha wa miaka 30 ya Azimio hilo ambapo  Kikao cha 69  cha Tume ya Hali ya Wanawake kitafanyika katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York kuanzia tarehe 10 hadi 21 Machi 2025. Wawakilishi wa Nchi Wanachama, Mashirika ya Umoja wa Mataifa na mashirika yasiyo ya kiserikali yaliyoidhinishwa na ECOSOC kutoka kanda zote za dunia wamealikwa kuhudhuria kikao hicho.

Siku ya Wanawake duniani
Siku ya Wanawake duniani

Miaka 30 baada ya Azimio la Beijing kuhusu haki za wanawake,safari bado ni ndefu

Katika kuelekea Siku  ya wanawake duniani naye  Mkurugenzi Mtendaji wa  shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya wanawake , Sima Bahous, alisisitiza kwamba ahadi zilizowekwa kwenye Azimio la Beijing miaka 30 iliyopita kuhusu haki za wanawake hazipaswi tu kukumbukwa bali zinahitaji kutekelezwa kikamilifu. Akizungumza Juma hili mjini Geneva Uswisi katika majadiliano ya Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa ya kuadhimisha miaka 30 ya Azimio la Beijing (#Beijing30), Bi Bahous alibainisha umuhimu wa kuharakisha maendeleo ya usawa wa kijinsia huku akiwataka viongozi wa dunia kuchukua hatua thabiti ili kuhakikisha haki za wanawake zinapewa kipaumbele wakati wa changamoto zinazoendelea duniani.

Siku ya anawake duniani
Siku ya anawake duniani   (AFP or licensors)

Bi Bahous alikazia kusema kuwa: “Miaka 30 iliyopita dunia iliweka ahadi ya kusongesha fursa na utu wa wanawake na wasichana wote. Ahadi hiyo haikuwa maneno matupu kwenye karatasi, ilikuwa ramani ya njia na wito wa mshikamano. Na kwa miongo mitatu imechochea hatua, wasichana wengi sasa wako shule, wanawake wengi wako bungeni, kuna sheria nyingi zaidi zinawalinda wanawake dhidi ya ukatili, na mataifa mengi zaidi yanatambua usawa wa kijinsia ni lazima.”&苍产蝉辫;Hata hivyo pamoja na  mafanikio hayo yote Bi, Bahous alisema kuwa safari bado ni ndefu kufikia malengo: “Hebu tuwe wakweli hatujafika tunapopaswa kuwa. Haki za wanawake na wasichana zinashambuliwa, fursa za wanawake kupaza sauti zinazidi kupungua na endapo tutaendelea na kasi hii msichana aliyezaliwa leo atakuwa na umri wa miaka 39 kabla wanawake hawajawa na viti vingi bungeni kama wanaume, atakuwa na umri wa miaka 68 kabla ndoa za utotoni hazijakomeshwa, na atakuwa na umri wa miaka 137 kabla umasikini uliokithiri kwa wanawake na wasichana haujatokomezwa. Hatuwezi kulikubali hili.” Kwa njia hiyo Mkuu huyo wa UN Women aliyahimiza mataifa yote kuchukua hatua sasa ili kuhakikisha ndoto za azimio la Beijing hazisalii kuwa ndoto bali maisha halisi.

07 Machi 2025, 17:07