杏MAP导航

Tafuta

Tuliombee taifa la Nicaragua Tuliombee taifa la Nicaragua  (AFP or licensors)

Nicaragua,Zaidi ya watawa 30 Waklara waondolewa kutoka katika monasteri tatu

Ukandamizaji wa upinzani unaendelea katika nchi hiyo ya Amerika Kusini.Hatima ya watawa waliochukuliwa kutoka katika monasteri za Managua,Matagalpa na Chinandega bado haijulikani.Mnamo Mei 2023,mamlaka Managua ilivunja Umoja wa Wafransiskani Waklara.Na katika miaka ya hivi karibuni Mashirika kadhaa ya kitawa yamefukuzwa kwa sehemu au kabisa.

Vatican News

Zaidi ya watawa 30 wa Shirika la Mtakatifu Clara wa Assisi, wajulikanao  kama Waklara Maskini, waliondolewa kutoka katika monasteri tatu za Nikaragua huko Managua, Matagalpa na Chinandega wakati wa usiku kati ya tarehe 28 na 29 Januari 2025.

Watawa waliofukuzwa nchini
Hata hivyo mnamo Mei 2023, Mamlaka ya Managua nchini Nicaragua iliendelea kufuta Muungano wa Masista wa Wafransiskani  wa Ndani (Waclara)  na taasisi na mashirika mengine tisa. Mashirika kadhaa ya kidini ya watawa yalifukuzwa kwa kiasi au mengine kabisa kutoka nchini Nicaragua katika miaka ya hivi karibuni, hasa baada ya uchaguzi wenye utata wa mwezi Novemba 2021, ambapo Daniel Ortega alichaguliwa tena kwa muhula wa tano, ikiwa ni wa nne mfululizo.

Ukandamizaji dhidi ya  Mashirika yasiyo ya kiselikali (NGOs)
Hatua kama hizo pia zilipitishwa. Serikali ya Nikaragua imefuta hadhi ya kisheria ya mashirika mengine 10 ambayo yalifanya kazi kama mashirika yasiyo na faida, na kufanya jumla ya mashirika yasiyo ya kiserikali yaliyopigwa marufuku tangu Desemba 2018 katika nchi hiyo ya Amerika ya Kati kufikia zaidi ya 5,600.

31 Januari 2025, 10:42