Cuba yatangaza kuachiliwa kwa wafungwa 553!
Vatican News
Kuachiliwa kwa taratibu lakini ulio mpana, katika muktadha wa upatanishi kati ya Kanisa Katoliki ambalo limekuwa likiendelea kwa miaka. Hayo yalitangazwa tarehe 14 Januari 2025 na Wizara ya Mambo ya Nje ya Cuba, ambapo katika taarifa yake iliweka hadharani uamuzi wa kuwaachilia huru wafungwa 553, waliopatikana na hatia ya uhalifu mbalimbali. Haikuwa wazi ikiwa wale walioachiliwa na Serikali ya Havana watajumuisha wafungwa wa kisiasa, ambao wengi wao wanatumikia vifungo kwa kushiriki katika maandamano ya kuipinga serikali mnamo Julai 2021. Tangazo hilo lilikuja saa chache baada ya utawala wa Marekani, wa Joe Biden kutangaza kuwa utaiondoa Cuba kutoka katika orodha ya nchi zinazofadhili ugaidi, ambayo pia inajumuisha nchi kama vile Korea Kaskazini, Iran na Syria.
Kudumisha mawasiliano na Papa Francisko
Hata hivyo Serikali ya Cuba iliripoti kwamba "imedumisha mawasiliano na Papa Francisko na wawakilishi wake na kama ilivyokuwa zamani kwamba ilijulisha msimamo wake juu ya michakato ya ukaguzi na kuachiliwa kwa watu walionyimwa uhuru na kukumbusha kuwa "zaidi ya watu 10,000 waliadhibiwa na kunyimwa uhuru” waliachiliwa kutoka katika gerezani kati ya 2023 na 2024 kwa aina mbalimbali za manufaa zinazotolewa na sheria." Aidha "Katika mkesha wa Mwaka Mtakatifu wa sasa 2025, Papa alitarajia aina za msamaha na ondoleo la adhabu katika Waraka wa Kutangaza Jubilei ambao unaongozwa na kauli mbiu: "Mahujaji wa Matumaini" na ndiyo "Roho hii ya Jubilei, ilikumbukwa katika tamko la Havana.
Hatua katika historia
Mnamo 1998, Mtakatifu Yohane Paulo wa Pili alipotembelea kisiwa hicho, Fidel Castro aliwaachilia wafungwa wapatao 200. Maelfu ya wafungwa pia waliachiliwa huru usiku wa kuamkia ziara ya Papa Benedikto XVI nchini Cuba mnamo mwaka 2012, na wengine 3,500 kabla ya kuwasili kwa Papa Francisko mnamo 2015. Katikati ya mwezi Desemba 2014, ilianzishwa tena uhusiano wa kidiplomasia kati ya Washington na Havana. Rais wa Marekani Barack Obama na mwenzake wa Cuba Raúl Castro walimshukuru Papa Francisko kwa mchango wake katika kufikia makubaliano hayo.