Vatican,semina kuhusu “uumbaji,asili,mazingira kwa dunia ya amani”
Vatican News
Kardinali Pietro Parolin, Katibu Mkuu wa Vatican atafungua semina ya kimataifa kuhusu "Uumbaji, Asili, Mazingira kwa Ulimwengu wa Amani" tarehe 11 Septemba saa 9:00 Alasiri huko Casina Pio IV mjini Vatican. Semina hiyo itaendelea hadi Septemba 12. Tukio lililoandaliwa na Baraza la Mafunzo ya Juu la Chuo cha Kipapa cha Taalimungu (PATH), litakuwa na sehemu nne za mada kwa ushiriki wa watu mashuhuri wa kikanisa, biashara, kijamii na kiutamaduni kutoka ulimwenguni kote.
“Kanisa linajiuliza lenyewe na watu wenye mapenzi mema ni njia gani za kufuata ili kulinda na kuthibitisha tena wema na kuishi pamoja, katika roho ya amani, ustawi wa binadamu na viumbe vyote,” inasema programu hiyo ya siku mbili. Wakati wa kazi - ambayo itakuwa kama hatua ya kumbukumbu, Ujumbe wa Papa Leo XIV kwa Siku ya 10 ya Kuombea Utunzaji wa kazi ya Uumbaji 2025, Wimbo wa Sifa kwa Viumbe wa Mtakatifu Francis wa Assisi, baada ya miaka 800, Waraka wa 'Mkombozi wetu' wa Papa Yohane Paulo II, 'tafakari ya ikolojia ya mwanadamu' ya Papa Benedikto XVI. Waraka wa Laudato si' na waraka wa kitume wa Laudate Deum zote nyaraka za Baba Mtakatifu Francisko, kwa wazungumzaji watazingatia changamoto zinazowakabili wanadamu leo hii ??na haja ya kufanya kazi pamoja kwa ajili ya kuhuisha upya maendeleo ya binadamu.
Vipindi vya semina
Vipindi vya masomo vitahitimishwa kwa Adhimisho la Ekaristi litakaloongozwa na Rais wa Chuo cha Kipapa cha Taalimungu, Monsinyo Antonio Staglianò, kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Petro saa 11:30 jioni siku ya Ijumaa, tarehe 12 Septemba 2025, na Mkutano na Papa uliopangwa kufanyika Jumamosi, tarehe 13 Septemba 2025 saa 11:00 asubuhi mjini Vatican. Mpango wa kina wa tukio hilo unapatikana katika tovuti hii: . Semina ya kimataifa kuhusu"Uumbaji, Asili, Mazingira kwa Ulimwengu wa Amani" imewezekana kutokana na mchango wa makampuni kadhaa, ikiwa ni pamoja na Arpinge, Polideck, Guglietta Global, Njia Yake Kazini, na NTT DATA. Chuo cha Kipapa cha Taalimungu, kwa kuungwa mkono na wafanyabiashara wakuu, kinatangaza shughuli zake nchini Italia na duniani kote kadiri ya miongozo iliyomo katika sheria mpya zilizoidhinishwa mwaka 2023 kwa njia ya Motu Proprio ya Ad Theologiam Promovendam.