杏MAP导航

Tafuta

2020.10.28 armi nucleari, missili, guerra, armamenti, disarmo atomico

Vatican:Kuibuka tena kwa kutatizika kwa matamshi ya kinyuklia yenye fujo

Katika hotuba yake kwenye Umoja wa Mataifa,Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican,Askofu Mkuu Caccia,alisisitiza wasiwasi wa Vatican juu ya ongezeko kubwa la matumizi ya kijeshi duniani kote,pamoja na silaha za uharibifu zinazozidi,mara nyingi kwa gharama ya uwekezaji katika maendeleo fungamani ya binadamu.

Vatican News

Badala ya kusonga mbele kuelekea amani, Ulimwengu unaonekana kusonga mbele, ukiwa na maendeleo yenye kuhuzunisha ya silaha zinazozidi kuharibu. Hayo yalisemwa tarehe 4 Septemba 2025 huko New York, Marekani na Askofu Mkuu Gabriele Caccia, Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican  katika  Umoja wa Mataifa, wakati wa kikao cha ngazi ya juu cha Baraza Kuu kilichoadhimishwa kwa Siku ya Kimataifa ya Kupinga Majaribio ya Nyuklia. Mwakilishi wa Vatican alisema: "Miaka themanini iliyopita,mlipuko wa silaha ya kwanza ya nyuklia ulifunua kwa Ulimwengu nguvu ya uharibifu isiyo na kifani. Tukio hili lilibadilisha mkondo wa historia na kuweka kivuli kirefu juu ya ubinadamu, na kuachilia matokeo mabaya kwa maisha ya mwanadamu na uumbaji. Matokeo mabaya ya tukio hili kubwa yamesababisha imani yenye matatizo kwamba amani na usalama vinaweza kudumishwa kupitia mantiki ya kuzuia nyuklia, dhana ambayo inaendelea kupinga mawazo ya kimaadili na dhamiri ya kimataifa."

Tangu jaribio la kwanza la nyuklia Julai 16, 1945

Askofu Mkuu  alikumbuka kwamba tangu jaribio la kwanza la nyuklia mnamo tarehe 16 Julai 1945, majaribio zaidi ya elfu mbili ya nyuklia yamefanywa katika angahewa, chini ya ardhi, baharini, na ardhini: "Vitendo hivi vimeathiri kila mtu, haswa watu wa kiasili, wanawake, watoto na watoto ambao hawajazaliwa. Afya na adhi ya wengi vinaendelea kuhatarishwa kimyakimya na mara nyingi bila fidia." Kwa sababu hiyo, aliongeza, Vatican inakaribisha kutafakari juu ya wajibu wa pamoja wa haraka ili kuhakikisha kwamba uzoefu wa kutisha wa siku za nyuma haurudiwi: "Inatia wasiwasi hasa kwamba, inakabiliwa na jukumu hili muhimu la pamoja, mwitikio wa kimataifa unaonekana kwenda kinyume.

Badala ya kupokonya silaha, zinaibuka chochezi na uhamasishaji wake

Badala ya kusonga mbele kuelekea upokonyaji silaha na utamaduni wa amani, tunashuhudia kuibuka tena kwa matamshi ya kichokozi ya nyuklia, ukuzaji wa silaha zinazozidi kuharibu, na ongezeko kubwa la matumizi ya kijeshi, mara nyingi kwa madhara ya uwekezaji katika maendeleo fungamani  ya binadamu na uendelezaji wa manufaa ya wote. Ni muhimu kushinda roho ya woga na kujiuzulu. Kama Papa Leo XIV alivyosema hivi karibuni kuwa: "Hatupaswi kuzoea vita! Hakika, ni lazima tukatae kama jaribu ushawishi wa silaha zenye nguvu na za kisasa" (Wawakilishi wa  Vatican kudumu Juni 18, 2025). Tamaa ya "ulimwengu usio na silaha za nyuklia," Askofu Mkuu Caccia aliendelea, "sio tu suala la umuhimu wa kimkakati na muhimu, lakini pia jukumu kubwa la maadili.

Ahadi inahitajika katika mazungumzo kuhusu mikataba ya upokonyaji

Ahadi hii inahitaji kujitolea upya kwa mazungumzo ya pande nyingi na utekelezaji thabiti wa mikataba ya upokonyaji silaha, pamoja na usaidizi madhubuti kwa jamii zinazoendelea kuteseka na matokeo ya muda mrefu ya majaribio ya nyuklia na silaha. Mwakilishi wa Vatican alihitimisha, kuwa “ Vatican inathibitisha tena umuhimu wa kuanza kutumika kwa Mkataba wa Marufuku ya Majaribio ya Nyuklia, pamoja na utekelezaji kamili wa Mfumo wa Kimataifa wa Ufuatiliaji na taratibu zake za uthibitishaji." Pia "inathibitisha tena uungaji mkono wake usio na masharti kwa Mkataba wa Kuzuia Silaha za Nyuklia," ikitoa wito wa "kuendelea kuimarishwa kwa kanuni ya kimataifa dhidi ya majaribio ya nyuklia ya milipuko kama hatua muhimu kuelekea amani ya kweli na ya kudumu." Ahadi hii inahitaji kujitolea upya kwa mazungumzo ya pande nyingi na utekelezaji thabiti wa mikataba ya upokonyaji silaha, pamoja na usaidizi madhubuti kwa jamii zinazoendelea kuteseka na matokeo ya muda mrefu ya majaribio ya nyuklia na silaha.

05 Septemba 2025, 15:15