Mahujaji milioni 24 wamefika Roma kwa Jubilei ya Matumaini
Baraza la Kipapa la Uinjilishaji limetoa data kuhusu idadi ya waamini ambao wamefika kwenye hija ya Jubilei kufikia sasa.
Vatican News
Zaidi ya miezi minane imepita tangu Baba Mtakatifu Francisko alipofungua Mlango Mtakatifu wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro tarehe 24 Desemba, kuanza rasmi Mwaka Mtakatifu wa Matumaini. Idadi ya mahujaji waliofika Roma kusherehekea Jubilei sasa imefikia milioni 24, kulingana na Baraza la Kipapa la Unjilishaji
Katekesi ya Papa tarehe 6 Septemba
Wakati huo huo, Jumamosi tarehe 6 Septemba 2025, saa 4:00 asubuhi, masaa ya Ulaya Papa Leo XIV atafanya Katekesi ya Jubilei katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, na wakati huo huo Mlango Mtakatifu utabaki umefungwa, lakini baadaye, utafunguliwa na washiriki wataweza kupita bila kurudi nyuma.
04 Septemba 2025, 09:10