Kd.Parolin:Hali ya kutisha huko Gaza,acha mauaji nchini Ukraine
Na Alessandro De Carolis – Vatican.
Kwa sasa ni sauti ya kilio katika jangwa la tahadhari ya kimataifa, kwa sababu malengo ni tofauti. Sauti ya Vatican, ambayo tangu mwanzo wa mgogoro katika Ukanda wa Gaza imekuwa ikitoa wito wa kusitishwa kwa mapigano, mwanga wa kijani kwa ajili ya misaada ya kibinadamu, na kuanza kwa mazungumzo ya kujenga. Lakini ni mwangwi ambao kwa sasa unafifia, ilhali uchunguzi wa kweli, unaochoshwa na uchungu ni kwamba, licha ya mauaji ya kila siku "kwa sasa hakuna mazungumzo." Hayo ni maneno ya Kardinali Pietro Parolin, Katibu Mkuu wa Vatican, akizungumza kutokea katika Hospitali ya Kipapa ya Bambino Gesù ambako tarehe 5 Septemba 2025, alikwenda kubariki Picha ya Pier Giorgio Frassati, ambaye Papa Leo XIV atamtangaza kuwa Mtakatifu Dominika tarehe 7 Septemba pamoja na Carlo Acutis.
Mkasa unahitaji mazungumzo
Mwenzetu Daniele Rocchi wa shirika la habari la SIR alitoa muhtasari wa mambo yanayozingatiwa na Katibu Mkuu wa Vatican, hasa msisitizo wa mara kwa mara wa Papa "kwamba wahusika waanze tena mazungumzo, na kupitia mazungumzo," Kardinali Parolin anatumaini, "wanaweza kupata suluhisho kwa hali mbaya na ya kutisha huko Gaza." Sauti yetu, Kardinali anaendelea, "ni ile inayoendelea kupazwa kwa sababu tumefanya hivyo hapo awali. Tulifanya hivyo jana (Alhamisi, Septemba 4), kwa uamuzi mkubwa, pia na Rais wa Israel, na tunatumaini kwamba sauti hii, ikiunganishwa na ile ya jumuiya ya kimataifa, inaweza kuwa na athari fulani."
Kulinda wale ambao hawawezi kusafiri
Katibu Mkuu wa Vatican alizua swali kuhusu hali mbaya, kama ile ya Gaza yote, inayoshuhudiwa na parokia ya eneo hilo, ambayo imehifadhi mamia ya watu tangu kuzuka kwa uhasama. Wasiwasi kwao, alisema Kardinali Parolin, "ni wa juu kwa maana kwamba pia kuna walemavu wengi huko ambao hawawezi kuhamishiwa kwingine, hivyo tunatumaini kutakuwa na heshima kwa wale ambao wameamua kukaa huko na ambao hawana njia nyingine. Na kwamba ombi hili la kuwaheshimu na kuwalinda litazingatiwa."
Ukraine, Milango Wazi ya Vatican
Wazo la mwisho lilikwenda kwa upande mwingine wa vita vya Ulaya, huko Ukraine, ambayo nchi za muungano huo walio tayari wamethibitisha ahadi yao ya kudhamini usalama. Katika kesi hiyo, Katibu Mkuu wa Vatican na "msimamo wa Vatican ni kwamba mazungumzo yaanzishwe," na Papa Leo XIV mwenyewe, alikumbuka kuwa, "alikuwa ameifanya Vatican ipatikane kama mahali pa kufanyia mazungumzo haya." Hii kwa mujibu wa Kardinali Parolin "ni nia kubwa ya kusaidia kutafuta njia na njia zote za kukomesha mauaji haya,” alihitimisha.