杏MAP导航

Tafuta

2025.09.02 Borgo Laudato si' 2025.09.02 Borgo Laudato si' 

Borgo Laudato si’:Papa Leo XIV kuzindua sura mpya ya kiikolojia na kiroho

Mkurugenzi wa Usimamizi wa Mpango wa Ikolojia wa Borgo Laudato Si alionesha mpango huo,ambao Papa Leo XIV atauzindua rasmi,Ijumaa,Septemba 5,akieleza kuwa uko wazi kwa kila mtu bila kujali imani au uhusiano mwingine.Anatumaini kwamba watalii wanaotembelea Mazingira ya Kipapa,bustani na shamba wakati wa kipindi cha kiangazi lililokuwa la kipekee huko Castel Gandolfo wataondoka wakiwa wamehamasishwa na ujumbe wa kutunza Dunia Nyumba Yetu ya kawaida ya Pamoja.

Na Paul Samasumo – Vatican.

Jumba la Kipapa lililozungukwa na bustani nzuri huko Castel Gandolfo, lililo karibu kilomita 25 kusini mashariki mwa Roma, ni eneo kubwa la majengo na bustani zinazoangalia Ziwa Albano. Hapo awali, eneo hilo lilikuwa nyumba ya Mfalme Domitian, lakini baadaye lilinunuliwa na Kiti Kitakatifu na kihistoria likawa makazi ya Mapapa.

Papa Leo XIV na mpango wa Laudato si’

Juma hili, Papa Leo XIV atazindua rasmi sehemu kubwa ya mali ya Castel Gandolfo kama Mpango wa ikolojia wa Borgo Laudato Si. Mpango huo wa ekari 135 sasa utatoa, katika lugha mbalimbali, ziara ya kuongozwa ya saa moja ya bustani, mashamba, kituo cha elimu cha Laudato si’, mgahawa na soko kwa watalii na wageni wa kimataifa. Kituo cha elimu, kwa upande mmoja, kitakuwa wazi kwa wageni wa siku au wa kukaa kwa muda mrefu, vikundi vya majimbo na parokia, watawa, mapadre, Maaskofu, watoto wa shule, vyuo vikuu, jumuiya zilizo katika mazingira magumu na wajumbe wa mabaraza ya Maaskofu ambao wanaweza kutaka kuiga mfano huo.

Cha kufurahisha itakuwa kozi iliyoundwa mahsusi kwa ulimwengu wa biashara, zinazolenga Wakurugenzi Wakuu na viongozi wa tasnia. Hata hivyo, Mkurugenzi wa Usimamizi wa Borgo Laudato, Padre Manuel Dorantes, alisisitiza kuwa kila mtu anakaribishwa katikati humo. Mpango huu unaakisi maono ya Papa Francisko, ambaye kwa mara ya kwanza alifungua Jumba la Papa kwa umma na kuanzisha mpango huo mwaka 2023.

Papa Francisko alilenga kukuza elimu ya ikolojia kwa kuunda nafasi ya kujitolea kwa ajili ya mafunzo na kuongeza ufahamu kuhusu masuala ya mazingira. Wakati Ikulu ya Papa itasalia kuhifadhiwa kwa matumizi ya Papa, Vatican News iliambiwa na Padre Dorantes kwamba msimu wa kiangazi Papa Leo XIV alifurahi kushirikishana bustani na wageni. Papa alichagua kuchukua matembezi yake ya kila siku na kusali katika bustani wakati wa mchana, baada ya wageni kuondoka.

Borgo Laudato sì

Borgo Laudato sì

Mzabibu uowekwa kwa ajili ya Papa Francisko

Kwa njia nyingi, uwazi huu, wa Papa Francisko na Papa Leo XIV, ni uthibitisho wa ajabu kwa utayari wa Papa kushirikisha nafasi ya Castel Gandolfo na mazingira yake safi, ambayo hapo awali yalihifadhiwa kwa matumizi ya upapa tu. Wageni wa mali ya Castel Gandolfo sasa wanaweza kutembelea bustani na kusali mbele ya Mama, sanamu ya Bikira Maria-ambapo Mapapa mbalimbali inasemekana walipeleka mizigo ya Kanisa mbele ya Maria, mama wa Kanisa. Wageni, kwenye ziara, wataona magofu ya kale ya Kirumi ya Domitian, Wanajimu wa Vatican, shamba, sanamu na vitu vya sanaa adimu vilivyoenea kwenye mali hiyo.

Kulingana na Padre  Dorantes, shamba jipya, kubwa la mizabibu pia limetengenezwa, na kuchukua nafasi ya shamba dogo. Kwa ushirikiano na Chuo Kikuu  cha Italia, mzabibu mpya ambao uliowekwa wakfu kwa Papa Francisko umepandwa. Padre  Dorantes alikuwa na makadirio ya historia kwamba divai inaweza kuwa tayari kuwekwa kwenye chupa kama divai mnamo 2029. Katika majengo hayo, nyongeza mpya inayojengwa ina eneo la  duka ambalo litauza mazao kutoka shambani, pamoja na soko linalotoa bidhaa kama vile mafuta ya mizeituni, asali, maziwa na bidhaa nyinginezo. Wageni pia watapata fursa ya kushiriki katika shughuli kama vile kutengeneza jibini.

Fr Dorantes introduces the project

Padre Fr Dorantes akiwakilisha Mpango wa Borogo Laudato si

Kituo cha ujasiri wa kiroho cha mpango huo

Kiini cha mpango wa Borgo Laudato si’ ni maono ya Kanisa ya ekolojia fungamani kama yalivyofafanuliwa na Waraka wa Kipapa wa, Ni njia inayounganisha imani na utunzaji unaoonekana kwa Dunia na watu wake. Kanisa linatumaini kuwa mipango kama hiyo ya Laudato si itachipuka katika majimbo  ulimwenguni kote.

Kituo kipya cha Elimu ya Juu cha Laudato si’, kilichojengwa hivi karibuni kwenye mali hiyo, kinatarajiwa kubarikiwa na Papa Leo XIV siku ya Ijumaa tarehe 5 Septemba 2025. Kitakapofanya kazi kikamilifu, kitatoa kozi kuhusu Laudato si’, kilimo-hai, mazoea endelevu, na mafunzo ya uongozi wa ikolojia. Kwa hivyo, hali ya kiroho ya kituo hicho itasitawishwa kupitia kozi maalum zinazojibu hitaji la dharura la kutunza sayari yetu ya pamoja.

Mkurugenzi wa Usimamizi wa mpango wa Laudato si’, Padre Manuel Dorantes wa nchini Mexico ni padre wa Jimbo Kuu la Chicago nchini Marekani.

Borgo Laudato sì

Borgo Laudato sì

Borgo Laudato

Asante kwa kusoma makala yetu hii. Ili kubaki umesasishwa,unaweza kujiandikisha kwenye habari za kila siku kwa kubonyeza hapa: Just click here

04 Septemba 2025, 10:35