杏MAP导航

Tafuta

2024.05.26 Wakati wa Misa katika Siku ya I ya Watoto Ulimwenguni. 2024.05.26 Wakati wa Misa katika Siku ya I ya Watoto Ulimwenguni.  (Vatican Media)

Vatican,Siku ya Watoto Duniani:Kamati inahamia Baraza la Kipapa la Walei,Familia na Maisha!

Katika andiko lililochapishwa tarehe 13 Agosti 2025,Papa Leo XIV anaamuru Baraza lililoanzishwa na Papa Francisko kuandaa matukio yaliyotolewa kwa ajili ya watoto kuwekwa ndani ya Baraza la Kipapa la Walei,Familia na Maisha.

Vatican News.

Baba Mtakatifu Leo XIV,  katika mkutano na Katibu Msaizidi kwa ajili ya Mambo ya Jumla ya Sekretarieti ya Vatican, Askofu Mkuu Edgar Peña Parra uliofanyika tarehe 6 Agosti 2025, aliamuru  Kamati ya Kipapa kwa ajili ya Siku ya Watoto duniani kuhamishia  ndani ya Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha. Kwa njia hiyo kutoka katika shirika linalotoa taarifa moja kwa moja kwa Baba Mtakatifu, Kamati ya Kipapa ya Siku ya Mtoto Duniani iliyoanzishwa 2024 Papa Francisko ili kuandaa na kuratibu kile kinachoitwa "Siku ya Mtoto Duniani", inahamishiwa katika Baraza la Kipapa la Walei Familia na Maisha. Katika taarifa hiyo inabainisha kwamba lazima: “kujulishwa kwa taasisi mbili zinazohusika ili kupanga mpito huo."

Historia yake

Ilikuwa tarehe 20 Novemba 2024, Papa Francisko alianzisha Kamati ya Kipapa ya Siku ya Watoto Duniani kwa barua ya mkono wake (chirograph). Kamati hiyo ina jukumu la kusimamia uhuishaji wa kikanisa na uandaaji wa  Siku ya Watoto Ulimwenguni katika tukio ambalo, baada ya Siku ya Vijana Duniani(WYD), ilileta pamoja watoto kutoka ulimwenguni kote kwa tukio la imani, muziki na ushuhuda. Toleo la kwanza lilifanyika tarehe 25 Mei 2024, kwenye Uwanja wa Olimpiki,  jijini Roma, mbele ya Hayati Papa Francisko na kuona ushiriki wa zaidi ya watoto 50,000 na vijana, ikiwa ni pamoja na wale kutoka maeneo yenye migogoro.

Huduma ya Kichungaji kwa Watoto

Waraka wa kuanzisha Kamati hiyo unasisitiza kwamba, Kamati ya Kipapa ina jukumu la kuratibu na kukuza mipango ya kamati za maandalizi ya kitaifa na kikanda, pamoja na kushirikiana na ofisi za kichungaji za Makanisa mahalia na Mabaraza ya Maaskofu ili Siku ya Watoto Duniani isibaki kuwa tukio lililojitenga na hivyo huduma ya kichungaji kwa watoto izidi kuwa ya kipaumbele. Kamati yenyewe iliandaa mkutano mapema Februari mwaka 2024  katika Ikulu ya Kitume ya Vatican iliyopewa mada: “Tuwapende na Tuwalinde” ili kuchunguza haki za watoto wadogo, ambao wanazidi kunyonywa na kunyanyaswa. Papa Francisko alihudhuria, pamoja na familia ya kifalme, wanasiasa, na wataalam wengi katika uwanja huo.

Sasa kila kitu kinaanguka ndani ya Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha, ambayo kazi yake ni kushughulikia masuala yanayohusiana na walei na familia, ambayo kwa hakika inajumuisha uchungaji na utunzaji wa watoto wadogo. Na ni Baraza hilo hili, linaloongozwa kwa sasa na Kardinali Kevin Joseph Farrell, inayoandaa Siku ya Vijana Duniani (WYD), ambayo awali iliratibiwa na "Sehemu ya Vijana" ya Baraza la Kipapa la Walei, ambalo mnamo mwaka 2016 - pamoja na mageuzi ya Baba Mtakatifu Francisko,  liliunganishwa katika kile kinachojulikana kwa sasa kama Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha.

13 Agosti 2025, 16:36